IJUE NGUVU YA DAMU YA YESU SEHEMU YA KWANZA 1

Bwana Yesu asifiwe, nakusalimu katika jina la Yesu kristo aliye Bwana na Mwokozi wa maisha yetu. Nineema nyingine ya pekee mabayo Bwana ametupatia ili tukajifunze somo hili ambalo linamtukuza yeye kwa ajili ya utukufu wake, nikweli kabisa ya kwamba Heshima na utukufu zitamrudia yeye aliye tuokoa kwa Damu yake mwenyewe.

Leo napenda kukuletea somo litakalo kuwezesha kuvuka mishale yote unayo kutana nayo katika maisha yako ya hapa Duniani, somo letu linaitwa "NGUVU YA DAMU YA YESU".  Na mimi kama mwandishi wa makala hii ninakushauri uwe na Daftari la kuandika kile Roho mtakatifu atakufundisha na kukusemesha ndani yako.

Hili ni somo litakalo kusadia kuijua na kuitumia nguvu iliyomo ndani ya Damu ya Yesu na kuitumia katika kuishinda mishale yote ya Mwovu shetani.

Lengo la somo hili ni kukupatia uwezo wa kuitumia Damu ya Yesu katika maisha yako ya kila siku, hivyo jitahidi kusoma mpaka mwisho wa somo hili.

Katika maisha ya kawida ya hapa Duniani kumekuwa na kusikia habari nyingi kuhusu Damu ya Yesu, nikweli yamkini na wewe unaye soma makala hii umewai kusikia kuhusina na hili, ukweli kabisa ni kwamba Damu ya Yesu Kristo ipo na inatenda kazi kabisa na chanzo chake ni pale msalabani Kalvari ambapo alitukumboa watu wote wa lugha zote na kabila zote na jamii zote.

Katika somo hili tutajikita kuangalia nguvu iliyomomkatika Damu ya Yesu ambayo itakusaidia katika kumuomba Mungu ili akujibu haja za moyo wako.

DAMU YA YESU INANGUVU YA KUTENDA MAMBO YAFUATAYO;-

  1. Damu ya Yesu inatusafisha na kutuosha dhambi zetu zote, Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu, katika vitu ambavyo Mungu amejifunua kwetu katika nyakati hizi za leo ni juu ya ondoleo la dhambi zetu na kuwekwa huru kwa koshwa na kusafishwa. Kusafisha dhambi zetu zote  tumepokea kutoka kwa Yesu kristo kupitia Damu yake ya pekee aliyo imwaga pale Msalabani Kalvari, ooh Bwana Yesu asifiwee....
Ukisoma 1Yohana 1;7 neno la Mungu linasema "Bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashilikiana sisi kwa sisi na Damu ya Yesu, mwana wake, yatusafisha dhambi yote". Vile vile Ufunuo 1;5 nayo inatueleza kwamba,  "Tena zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi aliye mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia. Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu yake". Kwahiyo unapo tubu tu dhambi zako Mungu anakusafisha na kukuosha kabisa kwa Damu ya Yesu, Hiajalishi umetenda kosa unaloliona kubwa kiasi gani, Damu ya Yesu inauwezo wa kusafisha kabisa.

 2. Damu ya Yesu kristo inatutakasa. Kutakaswa maana yeke ni kutengwa kwa ajili ya kusudi maalumu la Bwana, kwahiyo unapo  mwamini tu Yesu krito unatakaswa kwa Damu yake, Yaani unatengwa ili kulitumikia kusudi la Mungu la kukuleta hapa duniani. Tunapo lisoma neno la Mnugu linatuambia kwamba, Waebrania 10;19 " Kwa ajili hii Yesu naye, ili awatakase watu kwa damu yake mwenyewe, aliteswa nje ya lango ".

  3. Damu ya Yesu kristo inatupa uzima. Tunapo yasoma maandiko yanatueleza ya kwamba, Yohana 6;53 "Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni,  Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu ". Uzima unao ongelewa hapa ni uzima wa Ki Mungu na neno linasema,  Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu., kwahyo kinyume chake ni kwamba, Mkiula mwili wake mwana wa adamu na kuinywa Damu yake, mnauzima ndani yenu, ooh Bwana Yesu asifiwe, nguvu pekee ya Yesu kupitia Damu yake mwenyewe ndiyo inayo yupa uzima, Yaani uzima ulionao unapatika katika Damu ya Yesu na si pendinepo, Haleluyah....

  4. Damu ya Yesu kristo inatusogeza karibu na Mungu, Kumekuwa na watu mbalimbali wenye kiu ya kumjua na kusogea karibu na Mungu na wamekuewa wakijuliza maswali mbalimbali ya kuwa watawezaje kuwa karibu na Mungu, namimi leo nipo kukupatia ukuweli wa mambo ya kwamba ukitumia Damu ya yesu kristo kwatika Maisha yako nilizima utauona utukufu wa Mungu juu ya maisha yako, cha Muhimu ni kuiita Damu ya Yesu kwa imani yote iliyothabiti ndani yako.

Tukisoma neno la Mungu linatueleza ya kwamba Waefeso 2;13Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa damu yake Kristo." Kuwa mbali maana yake ni kwamba ulikuwa umetengwa na Mungu kwa ajili ya dhambi ulizo mkuwa nazo au zilizo kuwa zikikutumikisha lakini kwa sasa kupitia Damu ya Yesu uwekwa karibu na Mungu. Ooo ni neema ya pekee sana uliyo ipata kupitia Damu ya Msalaba ya Yesu.

   5. Damu ya Yesu kristo inatupa uhakika wa kupaingia patakatifu.  Waebrania 10;19Basi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu ". Ujasili maana yake ni kwamba hatuna hofu tena ya kuwa karibu na Mungu, wala kutoingia mbinguni kwa sababu ya Damu ya Yesu kristo,  kwahiyo Damu ya Yesu ndiyo inayo tufikisha mbinguni, hakuna njia nyingine itakayo kuokoa na jehanamu ya milele isipokuwa Nguvu ya Damu ya Yesu kristo. Na ndiyo maana wale walio waombaji wanaifahamu siri hii ya kwamba pale wanapo jitakasa na kumwomba Mungu huku wakiitumia Damu ya Yesu huwa wanakuwa na ujasili wa kuomba sana kwa Mzigo na kwa ujasili. Na hii ndiyo taofauti yetu sisi pamoja na wale watu wasio mwamini Kristo, napenda kukuambia mpemdwa ya kwamba imo nguvu, nguvu, nguvu ya ajabu sana Damuni mwa Bwana Yesu.

  6. Damu ya Yesu inanena mema na kuhimalisha agano.  Neno la Mungu linatueleza kuwa, Waebrania 12;24 "na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili. ". Danu ya Yesu ndiyo inayo nena mema juu ya shida zako unazo kutana nazo, na  muda mwingine shetani na jeshi lake waweza kuwa wamenena mabaya na laana juu yako na ukawa unaishi kwa kuteseka sana, lakini ashukuriwe Mungu kwa ajili ya Damu ya Yesu pale unapo iita huwa inatamka kitu chema juu ya maisha yako na kufuta mabaya yote yaliyo nenwa juu yako.  Oooo Bwana Yesu asifiweeee...

  7. Damu ya Yesu kristo inatuongezea neema na amani.  1Petro 1;2 " kama vile Mungu Baba alivyotangulia kuwajua katika kutakaswa na Roho, hata mkapata kutii na kununyiziwa damu ya Yesu Kristo. Neema na amani na ziongezwe kwenu. ".

  8. Damu ya Yesu kristo inatulinda na kutushindia wakati wa vita. Unapo kutana na vita yoyote katika maisha yako, tambua ushindi upo pale unapo iita Damu ya Yesu, haijalishi ni vita katika elimu yako, uchumi wako, mahusino yako na hata huduma yako, unapo iita Damu ya Yesu kristo inanena mema na kukushindia na kuangamiza mishale yote ya yule mwovu iliyo kuinukia kupia nyanja zote za maisha yako.  Ufunuo 12;11Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa. ".

Yapo mambo mengi sana amabyo ukimwomba Mungu kupitia Damu ya Yesu utaona anakujibu, kitu cha kuzingitia ni kwamba unapo itamka Damu ya Yesu katika maisha yako unatakiwa uwe na imani ya kutosha juu ya hiyo Damu na hapo ndipo nutaona miujiza mikubwa sana katika maisha yako, na hakika na wewe utaungana na miongoni mwa watu watakao yatukuza matendo makuu ya Mungu.

Mpendwa msomaji yamkini ni mara yako ya  kwanza kusoma makala hii na kupata elimu ya uweza wa Mungu kama ninavyo kushudia na hauja okoka yaani hauja mwamini na kumkabidhi Yesu maisha yako kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako. Napenda kukusihi ya kwamba lipo tumaini la haki na lenye uweza wa kutuingiza mbinguni na kutuepusha na moto wa milele ambao watenda maovu wataenda kutupwa huko, tumaini hilo li katika Yesu, pale tu unapo mwamini na kuchukua hatua na kuacha matendo yako maovu utapokea kipawa cha Roho mtakatufu kitakacho kuwezasha kuuona utukufu wa Mungu.

Kama bado hauja okoka na unahitaji kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako na ili uitumie Damu ya Yesu katika Ulinzi wako na katika maisha yako sali sala hii inayo fuata kwa imani na utakuwa umeokoka.

Sema "Eeh Bwana Mungu, ninakuja mbele yeko, mimi ni mwenye dhambi, nimekutenda dhambi kupitia matendo yangu,  kusema kwangu, kuwaza kwangu na kwa dhambi zakujua na za kutokujua, Eeh Bwana Yesu ninaomba unisamehe, nisafishe kwa Damu yako ya thamani, nifute jina langu kuwenye kitabu cha hukumu na uniandike kwenye kitabua cha Uzima wa milele, Eeh Bwana Yesu nakuja mbele zako kuanzia siku ya leo nifinyange moyo wangu, nafsi yangu na roho yangu kama upendavyo wewe, Amina. 

Mpendwa kama umesali sala hii fupi kwa kumaanisha tayari umeupokea wokovu, unatakiwa utafute kanisa lililo karibu yako lenye kumuabudu Mungu wa kweli na uungane nao kwa ajili ya kukua kiroho. 

vile vile nakuomba ujitahidi kuepuka maisha ya Dhambi, maana ni dhambi pekee ndiyo itakayo kutenga na uso wa Mungu.Nakutakia maisha mema ya wokovu,Wako mpendwa katika KristoDaniel Mbugu.Kwa mwendelezo wa mafundisho zaidi ya neno la Mungu tembelea  AMKA UKUE KIRIHOwww.amkaukuekiroho1.blogspot. Na kwa ushauri kuhusiana na maisha ya wokovu tuma ujumbe katika email yangu. www.mbugudaniel@gmail.com. Au wasiliana nami kwa kutuma ujumbe wa maandishi kwenda  kwajia ya sms au whatsApp kwa 0758505174/0655505173. Mungu akubariki.

Somo hili litaendelea kataika sehemu ya pili, karbu sana



Comments

  1. great teachings be blessed servant of God

    ReplyDelete
  2. Ni kweli kabisa Damu ya Yesu inatakasa.. Very Great sermon!

    ReplyDelete
  3. Kwakweli Mungu akubariki na awabariki kwa kuelimisha inavotakiwa na kama MNA group WhatsApp ingekuwa vyema sana 0763721735

    ReplyDelete
  4. Kwakweli Mungu akubariki na awabariki kwa kuelimisha inavotakiwa na kama MNA group WhatsApp ingekuwa vyema sana 0763721735

    ReplyDelete
  5. Hakika nimebarikiwa na somo hili ๐Ÿ™๐Ÿผ

    ReplyDelete
  6. Ubarikiwe nimejifunza kitu kuzuri mnoo

    ReplyDelete
  7. Mungu wa Mbinguni na awabariki sana Sanaa๐Ÿ™

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular Posts