ZITAMBUE AHADI ZA MUNGU KATIKA KUKUHAKIKISHIA ULINZI WAKO.

Bwana yesu asifiwe mpendwa,
Nakusalimu katika jina la Yesu aliye Bwana na mwokozi wa maisha yetu.
Karibu katika makala yetu hii ya AMKA UKUE KIROHO ambapo leo tutakwenda kuangalia ahadi za Mungu alizo tuhaidi katika kutuhakikishia ulinzi na usalama wa maisha yetu. Namshukuru Mungu kwa ajili yako maana ni kwa neema tu hata upate nafasi hii ya kusoma somo hili ambalo lina leta utukufu kwa Mungu. Hivyo andaa moyo wako kwa ajili ya kupokea kile ambacho Roho Mtakatifu atakusemesha ndani yako katika kukuvusha katika maeneo mbalimbali unayo kutananayo ambapo mengine ni  hatarishi kwa imani yako na maisha yako. Karibu tuanze sote tuanze sote katika somo hili ;-
Tunapo soma Biblia katika maeneo mengi tofauti tofauti huwa tunakutana na ahadi za Mungu za kumfanya mtu aishi kwa kumtegea yeye, zipo ahadi nyingi sana ambazo Mungu ametuhaidi lakini leo tunaenda kuangalia ahadi inayo husu ulinzi wetu. Tunapo kuwa hapa Duniani tunakutana na mambo mbalimbali ambayo mengi yao ni hatarishi kiasi kwamba tusipo kaa karibu na Mungu tunaweza kuumia au hata kupoteza maisha kabla ya wakati ulio kusudiwa na Mungu katika maisha yetu.
Tunapo soma agano la kale na agano jipya katika Biblia Mungu anatuhakikishia ulinzi endapo tukimtegemea yeye. Katika Yohana 14:13-14 “Nanyi mkiomba neno lolote kwa jila langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya mwana. Mkiomba neno lolote kwa jina langu, nitalifanya.” Tunapo soma katika Yohana tunatambua ya kwamba Yesu anatuhaidi tumuombe neno lolote kwa jila lake, na anasema kuwa hilo tukalo muomba atalifanya ili Mungu atukuzwe ndani ya mwana. Kumbuka kuna mambo mengi ya kuomba ambayo unayahitaji ili Mungu akutendee lakini tunapo utazama msitari huu tunaona tukiambiwa kuwa  “Nanyi mkiomba neno lolote” Biblia haijatupa mpaka wa kuombea bali inasema nanyi mkiomba neno lolote kwa jina langu hilo nitalifanya. Sasa tunapo tazama kichwa cha somo letu kinahusu Ulinzi hivyo tutaenda kuzungumzia ulinzi kwa undani zaidi, sasa kwakuwa tunaongelea ulinzi naomba katika Yohana 14:13-14, kutokana na somo letu twaweza kuondoa kipngele cha “neno lolote” na kuweka neno ulinzi ili kuendana na somo letu.
Kama ukiondoa neno lolote na kuweka ulinzi, itasomeka hivi “Nanyi mkiomba ulinzi kwa jila langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya mwana. Mkiomba neno lolote kwa jina langu, nitalifanya.” Kwahiyo kama tunavyo jua ya kwamba neno la Mungu li hai hivyo Yesu anapo haidi ulinzi katika neno lake kwa kutupa nafasi ya kuomba neno lolote huwe na uhakika kuwa ataufanya ulinzi huo ili ahimalishe mahusiano yako nayeye. Katika mstari huu  tulipo ondoa neno lolote na kuweka ulinzi imetuhakikishia ya kwamba kama Mungu amesema tumuombe neno loloote kwa jina leke atatenda. Na sisi katika neno lolote tumeamua kuomba ulinzi maana ndilo hitaji letu kwa hiyo tuwe na uhakika yakwamba atenda kama alivyo haidi ili Baba atukuzwe nadani ya Mwana yaani Yesu.
Katika ahadi ya ulinzi Mungu amewahakikishia watumishi wake ulinzi ambao hauna kikomo katika wakati wowote, kwa hiyo mtu anapo mwamini Mungu atatembea na ahadi hiyo ambayo itamfanya aishi kwa imani na kwa uhakika ya kwamba Mungu yuko pamoja naye katika maeneo yote anayo pitia.
Katika Biblia tunamsoma  mtumishi wa Mungu Daniel na jinsi alivyo tembea na ahadi za Mungu za kumhakikishia ulinzi na akaweza kupona katika tundu la Simba. Biblia inatueleza ya kwamba Simba wale ambamo Daniel alitupwa walikuwa na njaa kari, lakini Bwana aliwafunga midomo yao ili wasimdhuru Daniel. Nidhairi ya kwamba imani ya Daniel katika kumuamini Mungu ilikuwa ya uhakika maana kama isinge kuwa ya uhakika asingeweza kukataa maagizo ya watesi wake bali angekubali ili aendelee kuishi pasipo kudhurika. Lakini kwa Daniel ilikuwa kinyume na watesi wake ambao walikuwa wakimuwazia mabaya. Ukweli ni kwamba waliweza kumtupa kwenye tundu la simba wenye njaa kali lakini Simba hao hawakufanya lolote kwa Daniel.
Ni ulinzi wa ajabu sana ambao Mungu huwazungushia wale wamchao kwa lengo la kuwa epusha na watesi wao. Vilevile katika Biblia tunasoma habari za vijana watatu ambao ni Shadraka, Meshaki na Abednego ambao walikataa kuiabudu sanamu ya Mfalme Nebukadreza.  Biblia inatueleza ya kwamba vijana hao walikuwa wakimwamini Mungu na ulinzi alio wahaidi na ndiyo maana walikuwa tayari kumgomea Mfalme kwa kutokushirikiki kuisujudia sanamu. Baada ya kukataa walia andaliwa tanuru kubwa ya moto mkali ili wakateketee huko. Tunapo soma kitabu cha Daniel 3:1…. Tunaona majibizano kuhusiana na wao kukataa  kuibudu sanamu ya mfalme. Na Mfalme alipo waambia kuwa atawatupo katika tanuru ya moto walimjibu pasipo hofu ya kwamba Mungu wao anaweza kuwaokoa na moto huo. Hii ni imani ya kipee walio kuwa nayo vijana hawa. Hua nashwangazwa na jinsi walivyo jibu katika Daniel 3:17 ya kwamba “kama ni hivyo Mungu wetu tunaye mtumikia aweza kutuokoa na tanuru iloe iwakao moto.”
Kwa kufanya hivyo walimthibitishia Mfalme ya kwamba Mungu wanae mtumikia ni mkuu kuliko moto huo wanao uandaa kwa ajili  yao. Ukweli ni kwamba walitupwa kwenye lile tanuru la moto mkali lakini hakuna hata aliye ungua unyayo au unywele wake,  bali wali furahia neema ya Mungu katika moto kubwa walio kuwemo na hatimaye wakatoka wakiwa salama.  Mfalme alipo ona matendo makuu ya Mungu juu ya Shadraka, Meshaki na Abednego alishangaa sana na akaielekeza imani yake kwa Mungu wa kina Daniel. Yamkini umepitia magumu mengi kiasi kwamba unaona  ya kuwa Mungu hakujibu maombi yako, leo napenda kukutia moyo ya kwamba Mungu wetu ni mwema sana na pale anapo haidi hua anatena. Hakuna sehemu yoyote alipo wahacha  watumishi wake  waaibike bali aliwashindia  katika mambo magumu na wao walifurahi na kumtukuza yeye.
Katika maisha yako ya wokovu wako hapa Dunia unatakiwa kumwamini Mungu katika ahadi zake za ulinzi juu ya maisha yako. Na kitu unacho takiwa wewe ni kuomba tu na kuamini maana katika maombi ndio kunamajibu ya mambo yote. Tulivyo anza somo hili tuliona jinsi Yesu alivyo tuambia ya kwamba tuombe neno lolote kwa jina lake hilo atalitenda. Katika hatari yoyote unayo kutana nayo katika maisha yako unatakiwa kumuita Mungu ili aje akutetee na hakika yake nimkwamba unapo muita hua nanashuka na kukutetea. Anasema katika Isaya 59:1 ya kwamba “Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake sio zito, hata lisiweze kusikia” hivyo unapo omba anakusikia na kwa kua mkono wake sio mfupi atakuokoa na maadui zako wote. Bwana Yesu asifiwe , oooh Haleluyah, mkono wa Mungu ni imara sana katika kukutetea. Kama aliweza kumtete Daniel, Shadraka, Meshaka na Abednedo na kwako anaweza kukuokoa na adui zako, nao watasimulia matendo makuu ya Mungu katika maisha yako. Na hakika watakuwa mashahidi wako katika kuutukuza utukufu wa Mungu alio kutendea mambo makuu.
Tunapo soma katika kitabu kile cha Isaya 43:1-2 tunaona ahadi inayo sema hivi “…Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu. Upitapo maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haita kugharakisha; uendapo katika moto hauta, huta teketea, wala wala mwale wa moto hauta kuunguza”. Hii ni ahadi inayo kutia moyo ya kwamba upitapo katika maji mengi hayata kugharakisha na uendapo katika moto hauta kuunguza wala mwale wa moto haita kuunguza. Chukua andiko hili na linganisha na mapito ya Shadraka, Meshaka na Abednego kipindi wanatupwa katika tanuru la moto, utagundua kwamba ahadi hii ya Mungu ilitimia katika maisha yao maana hawakuungua. Na huu ndio ulio ulinzi wa Mungu ya kwamba tukiomba neno lolote kwa jina lake atatenda na pale tunapo kutana na hatari yeye yuko pamoja nasi katika kututetea. Haijalishi umetupwa katika tanuru la moto mkubwa kiasi gani yeye yuko pamoja na wewe katika kukulinda na kukutetea,  wala miale ya moto haita tuunguza.
Katika Yeremia 1:10-19 neno linasema “Angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya Ufalme ili kung’oa, na kubomoa na kuharibu, na kuangamiza, ili kujenga na kupanda. Nao watapigana nawe lakini hawatakushinda maana mimi niko pamoja nawe, asema Bwana ili akuokoe”. Mkazo wangu katika mstari huu uko katika mstari wa 19 alipo sema ya kwamba Nao watapigana nawe lakini hawatakushinda”. kwa hiyo wewe waache tu adui zako wanao pigana nawe maana hakikika ni kwamba hawata kushinda.
Katika Isaya 54:17 neno la Mungu linasema “Kila siraha itakayo fanyika juu yako ahita fanikiwa, na kila ulimi untakao inuka juu yako katika kuhukumu, nitauhukumu kuwa mkosa…asama Bwana”.
Kumbukumbu la torati 28:7 neno linasema “Bwana atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako, watakutokea kwa njia  moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba”.
Yeremia 15:21 neno la Mungu linasema “Nami nitakuokoa na mikono ya watu wabaya, name nitakukomboa na mikono ya watu wenye kutisha”.
Zaburi 34:7 neno linasema “Malaika wa Bwana hufanya kituo; akiwazunguka wale wamchao na kuwaokoa”.
Zakaria 2:5 neno linasema “Kwa maana mimi, asema Bwana nitakuwa ukuta wa moto kukunzuka pande zote, name name nitakuwa huo utukufu ndani yake”. Hizi ni baadhi ya ahadi alizo kuahaidi Mungu katika kukuhakikishia ulinzi, tambua ya kwamba kila unacho kifanya Mungu yuko pamoja nawe, amesema atakuwa ukuta wa moto kukuzungukuka, amesema kuwa usiogope kwa ajili ya adui zako maana yeye yuko pamoja nawe ili nakuokoe, amesa ya kuwa hata kama adui zako wakikutokea kwa maelewano ya njia moja kwa lengo la kukuzuru yeye atawapiga mbele yako nao watakimbia pasipo maelewano tena kwa nia saba.
Ahadi za Mungu mara nyingi zinatimia kwa wale wamchao na kumwabudu, unatakiwa kukaa sana karibu na Mungu ili yeye akuimarishie ulinzi wake. Kitu kibaya ambacho Mungu hapendi ni dhambi. Dhambi huondoa utukufu wa Mungu juu yako na kukuacha mtupu. Kama ukitenda dhambi uanatakiwa kuwa mwepesi wa kuomba toba mbe za Mungu ili akusemehe.
Yamkini unasoma ujumbe huu ukiwa na hofu kubwa ya matatizo yanayo kusumbua, sikiliza nikwambie ya kwamba hakuna neno gumu kwa Mungu, haijarishi unasumbuliwa na wachawi,waganga,majini na manyanyaso ya shetani yakila aina unacho takiwa ni kuomba tu .
Katika maombi Mungu atakuatana na adui zako na kuwateketeza kwa moto wake ulao, kama vile alivyo iteketeza miungu baali kipindi cha nabii Elia.
Mpendwa njia rahisi ya Mungu kushugulika na mahitaji yako ni kumtegea yeye, kama bado hauja mwamini Yesu  au ulikuwa umeokoka na  ukarudi nyuma Sali paoja nami sala hii ya toba na Mungu atakusamehe na kuku safisha. Hakikisha unapo omba toba hii omba kwa kumaanisha na umalizapo usirudie dhambi tena bali mfuate Mungu ili ajidhihirishe katika maisha yako kwa uweza wake wote.
Kama uko tayari kumurudia Mungu  tamka maneno haya yafuatayo kwa kumaanisha. Sema "Eeh Bwana Mungu, ninakuja mbele yeko, mimi ni mwenye dhambi, nimekutenda dhambi kupitia matendo yangu,  kusema kwangu, kuwaza kwangu na kwa dhambi zakujua na za kutokujua, Eeh Bwana Yesu ninaomba unisamehe, nisafishe kwa Damu yako ya thamani, nifute kuwenye kitabu cha hukumu na uniandike kwenye kitabua cha Uzima wa milele, Eeh Bwana Yesu nakuja mbele zako kuanzia siku ya leo nifinyange moyo wangu, nafsi yangu na roho yangu kama upendavyo wewe, Amina. mpendwa kama umesali sala hii fupi kwa kumaanisha tayari umeupokea wokovu, unatakiwa utafute kanisa lililo karibu yako lenye kumuabudu Mungu wa kweli na uungane nao kwa ajili ya kukua kiroho.
Nakutakia maisha mema ya wokovu,
Wako mpendwa katika Kristo
Daniel Mbugu.
Kwa mwendelezo wa mafundisho zaidi ya neno la Mungu tembelea  AMKA UKUE KIRIHO. www.amkaukuekiroho1.blogspot. Na kwa ushauri kuhusiana na maisha ya wokovu tuma ujumbe katika email yangu. www.mbugudaniel@gmail.com. Au wasiliana nami kwa kutuma ujumbe kwenda  kwajia ya sms au wattspp kwa 0758505174/0655505173. Mungu akubariki.


Comments

  1. ninaanza kuiona ng'ambo yako katika huduma

    ReplyDelete
    Replies
    1. Asante ndugu, kwa kunitia moyo katka huduma hii ya Mungu

      Delete
  2. Glory to Almighty God. The anointing of Holy Ghost be upon you.

    ReplyDelete
  3. Mtumishi Mungu akubariki sana sana

    ReplyDelete
  4. Ubarikiwe Sana mtumishi kwa kristo Yesu, 🤝.

    ReplyDelete
  5. Be blessed and happy God's sevant

    ReplyDelete
  6. Barikiwa Sana Mtumishi
    Nimevushwa kwa mafundisho haya

    ReplyDelete
  7. asante kwa ujumbe wa neno la Mungu

    ReplyDelete
  8. Nmepata kitu Mungu azidi kukuza huduma yako mtumishi

    ReplyDelete
  9. Mtumishi ubarikiwe sana na nimejifunza mengi Shalom

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular Posts