KUISHI MAISHA MATAKATIFU

Bwana Yesu asifiwe mpendwa,

Nakusalimu katika jina la Yesu kristo aliye Bwana na mwokozi wa maisha yetu.
 


Karibu katima makala yetu hii ya wokovu, ambapo leo tutaenda kujifunza jinsi ya kuishi maisha matakatifu na yenye kumpendeza Mungu. Nakushauri mpendwa usomapo ujumbe huu jitahidi kufika mpaka mwisho utakusaidia kukuvusha kutoka sehemu moja kwenda nyinge. Karibu sana 

   Lengo la somo hili:- ni kumufanya mkrito atambue maisha yanayo mpendeza Mungu na aamue kuishi maisha yenye kumpendeza Bwana katika maisha yake yote ya hapa duniani. Maisha matakatifu niyale maisha ambayo mkristo anaishi pasipo kutenda dhambi au kama ikitokea ametenda dhambi anakuwa mwepesi wa kuingia katika toba na kumuomba Mungu amusamehe. Tunapo soma maandiko katika sehemu mbali mbali za Biblia utakuta Mungu anawaasa watoto wake waishi maisha matakatifu. Kabla hatujaingia kwenye somo ngoja tutazame baadhi ya maandiko yanayo sisi tiza  juu ya utakatifu:-

Mambo ya malawi 11:45

"Kwa kuwa mimi Bwana, niliye waleta kutoka Misri, ili kwamba niwe Mungu wenu ; basi mtakuwa watakatifu, kwa kuwa mimi ni mtakatifu"

 Mambo ya malawi 19:2"Nena na mkutano wote wa wana wa Israel, uwaambie mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi Bwana, Mungu wenu ni mtakatifu"  Mambo ya malawi 20:26"Nanyi mtakuwa watakatifu kwangu mimi, kwa kuwa mimi Bwana ni mtakatifu, nami nimewatenga ninyi na mataifa, ili kwamba mwe wangu"

Bwana Yesu asifiwe mpendwa katika Bwana, kutokana na baadhi ya maandiko hayo tulio yaona yanatuonyesha jinsi Mungu alivyo kuwa anawasisi tiza wana wa Israel wawe watakatifu, tena alikuwa anongezea wawe watakatifu kwakuwa yeye yaani Mungu ni Mtakatifu. Kwamaana hiyo basi tutakuja kutambua ya kuwa Mungu ni mtakatifu hivyo anataka wale wanao mfuata waishi maisha matakatifu kama jinsi yeye alivyo. Utaka tifu tunaweza kuangalia katika maana tofauti tofauti, lakini mimi napenda kuelezea utakatifu kama ifuatavyo:-

  • Utakatifu maana yake ni kutengwa kwa ajili ya kusudi maalumu la Mungu.
  • Maisha matakatifu ni maisha ya kumpendeza Mungu, ni maisha ambayo hayana mchanganyo wa dhambi ndani yake, na mara nyingi watu wanao ishi maisha matakatifu hua wako makini sana na Mungu wanaye mwabudu na kumtumikia na pale wafanyapo Dhambi dhamira yao ya ndani huwa sunta na kuwafanya wasogee kwa Mungu katika toba ya kweli. Sisemi kwamba hawatendi dhambi kabisa , hapana bali pale watendapo dhambi hua wanakuwa wepesi kupiga magoti na Kumwomba Mungu awasamehe makosa yao.
  • kwanini basi tuishi maisha matakatifu?, tunaishi maisha matakatifu ili kumpendeza Mungu na kuishi sawasawa na makusudi yake ya kutuweka duniani.
 Katika kutambua jinsi ya kuishi maisha matakatifu ni vyema tukajua vitu vinavyo sababisha mtu kutokuwa na maisha matakatifu.

        Kitu kinacho sababisha kutokuwa na maisha matakatifu ni Dhambi, dhambi ndio ambayo huondoa utakatifu  kwa mwanadamu na ndo kitu ambacho Mungu  hakipendi. Kumbuka Mungu hamchukii mtu bali anachukia maovu anayo yatenda ambapo maovu hayo huitwa dhambi

Dhambi maana yake ni uasi yaani kwenda kinyume na matakwa ya Mungu aliyo kuagiza, katika somo hili tutaangalia madhara ya dhambi jinsi yanavyo mfanya mtu aukose utukufu wa Mungu na kuishi maisha yasiyo kuwa na nguvu za kimungu ndani yake. Yafuatayo ni madhara ya dhambi katika maisha ya mwanadamu:-

  1. Kupungukiwa na utukufu wa Mungu, Biblia inatueleza ya kuwa Mungu ni mtakatitifu na amejawa na utukufu mwingi, hivyo utakapo tenda dhambi utakuwa umepunguza utukufu wa Mungu kwako, faida ya utukufu wa Mungu ni kwamba unapo kufunika unakufanya uishi maisha ya mng'ao na yenye kumpendeza Mungu. tunapo soma katika kitabu kile cha Warumi 3:23. "Kwa sababu hiyo wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utuku wa Mungu" . Kutokana na andiko tunatambua kuwa unapo tenda dhambi tu unapungukiwa na utukufu wa Mungu.                              
  2. Mungu kutoyasikia maombi yako, katika Biblia unapo soma kitabu cha Yohana 9:31"Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi, bali mtu akiwa ni mcha Mungu na kufanya mapenzi yake, humsikia huyo". Kutokana na nadiko hili tunatambua ya kuwa ni dhahili Mungu hapendani na mwenye dhambi kiasi kwamba yuko tayari hata kuacha kuya sikia maombi yake. Katika maisha yetu ya wokovu tunategemea sana maombi ambayo ndiyo hutupa upenyo wa mambo yetu na kutulinda kutoka kwa maadui zetu, hivyo unapo tenda dhambi utakuwa umejitenga na uso wa Mungu na nakuwa hasikii maombi yako.                                                                                      
  3. Kuwa mtumwa wa dhambi, mtu anapo tenda dhambi anakuwa mtumwa wa dhambia, neno mtumwa humaanisha kuto kuwa na uhuru wa kujitegemea wewe mwenyewe na hivyo kutumikishwana nguvu nyingine iliyoko juu. Ndivyo ilivyo na dhambi inapokuwa ndani ya mtu humfanya mtu huyo kuishi maisha ya utumwa katika maisha yake. Katika Yohana 8:34 "Yesu akawaambia amini, amini nawambieni, kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi". Hakuna maisha ya taabu sana kama ya utumwa, unapo soma historia ya nchi yetu ya Tanzania kuhusiana na jinsi watumwa walivyo kuwa wanafanyishwa kazi pasipo kuwa na muda wa kutosha wa wao kupumzika ndipo utakapo tambua vizuri neno utumwa lilivyo beba maana na uzito kubwa wenye mateso ndani yake, ni ukweli usio pingika ya kuwa maisha ya dhambi ni ya utumwa ambapo mtu hutamani kuacha na anashindwa kujinasua kwa sababu ya kushikiliwa na dhambi hivyo kukuta anakuwa mtumwa wa dhambi anayo itenda.
  4. Mauti, dhambi ndiyo inayo sababisha kifo, unapo soma kitabu cha mwanzo na kuangalia jinsi Mungu alivyo kuwa amewahaidai Adamu na Hawa maisha mazuri yenye furaha na amani, lakini baada ya ahadi zake aliwataka wasitende dhambi kabisa na akawahaidi ya kuwa pale watakapo tenda dhambi kwa kula mti ule wa katikati hakika watakufa. Ndicho kilicho tokea ya kwamba baada ya Adamu na Hawa kutenda dhambi walisababisha mauti ambayo mpaka sasa inasumbua dunia nzima, kwa sasa kila sehemu utakapo pita utakuta watu wanalia kwa sababu ya mpendwa wao kuondoka. Ukisoma katika Warumi 6:23 "Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali kalama ya Mungu ni uzima wamilele katika kristo Yesu Bwana wetu" mauti inayo ongelewe hapa ni kuukosa uzima wa milele

Mpendwa ni heri uwe moto au baridi maana Biblia inasema ukiwa uvugu vugu Mungu atakutapika, kutapikwa kunako ongelewa hapa ni kwamba siku ya mwiso ajapo mwana wa Adamu hauta uona ufalme wa Mungu. Biblia inatuambia ya kwamba siku hiyo ya mwisho hakuna mtu wa kujitetea, hivyo neema tulio nayo ni sasa katika kuishi maisha matakatifu na yenye kumpendeza Mungu.

Mpendwa mtu asikudanganye kamwe hakuna urafiki kati ya dhambi na Mungu, ukitenda dhambi tambua kabisa ya kwamba unajitenga na utukufu wa Mungu, kumbuka unacho kipanda sasa ndicho utakacho vuna. Jehanamu haikuandaliwa kwa ajili ya mwanadamu bali iliandaliwa kwa ajili ya shetani hivyo unapo tenda dhambi unampa shetani uhalali wa kukumiliki na kukuvuta katika kuingia katika ziwa lile liwakalo moto.

Mpendwa katika maisha yako ya wokovu kipindi ukiwa hapa Duniani jitahidi sana kuishi maisha matakatifu, Biblia inatueleza kuwa mshahara wa dhambi ni mauti , kumbuka neno mshahara huwa linatokana na kutenda kazi flani na kupewa malipo, hivyo unapo tenda dhambi unakuwa unategemea malipo ambayo ni kuitumikia jehanamu iliyo andaliwa kwa ajili ya shetani. Biblia inaendelea kutuambuia ya kwamba Nafsi itendayo dhambi ndiyo itakayo kufa. Biblia inaendelea kuelezea ya kwamba siku hiyo kitakuwa ni kilio kikuu kwa wale walio kuwa mbali na Mungu.

Kwanini uishi maisha ya dhambi na ukaangamie katika ziwa lile liwakalo moto usio kuwa na kikomo. Chunga sana matendo yako mpendwa,  amua leo kumfuata kristo, wokovu ni bure na maamuzi sahihi ni yale unayo yafanya leo hii baada ya kuisikia sauti ya Roho mtakatifu pindi inapo kuhimizi utubu. 

Mpendwa kwakua bado uko hai mpaka sasa tambua lipo kusudi la Mungu lililo kufanya uendelee kuishi, hivyo kata shauri na mfuate Yesu. Biblia inantuambia ya kwamba tunao uhakika wa kupaingia patakatifu kwa Damu ya Yesu Kristo. Ni Damu ya Yesu pekee ndiyo itakayo tutakasa na kutuweka huru kutoka katika utumwa wa dhambi na mauti ya kuikosa mbigu, kumbuka hakuna muda wa ziada wa wewe kuupokea wokovu isipomkuwa sasa pindi unapo kuwa hai. Mpendwa usiseme utaokoka kesho maana kesho hautambui ni nikipi kitakacho tokea, wokovu ni sasa katika Kristo  Yesu aliye Bwana na mwokozi wa Maisha yetu, yeye ndiye atakaye tutenga na mauti.

Kama uko tayari kumurudia Mungu  tamka maneno haya yafuatayo kwa kumaanisha. Sema "Eeh Bwana Mungu, ninakuja mbele yeko, mimi ni mwenye dhambi, nimekutenda dhambi kupitia matendo yangu,  kusema kwangu, kuwaza kwangu na kwa dhambi zakujua na za kutokujua, Eeh Bwana Yesu ninaomba unisamehe, nisafishe kwa Damu yako ya thamani, nifute kuwenye kitabu cha hukumu na uniandike kwenye kitabua cha Uzima wa milele, Eeh Bwana Yesu nakuja mbele zako kuanzia siku ya leo nifinyange moyo wangu, nafsi yangu na roho yangu kama upendavyo wewe, Amina. mpendwa kama umesali sala hii fupi kwa kumaanisha tayari umeupokea wokovu, unatakiwa utafute kanisa lililo karibu yako lenye kumuabudu Mungu wa kweli na uungane nao kwa ajili ya kukua kiroho. 

     Nakutakia maisha mema ya wokovu,

            Wako mpendwa katika Kristo 

                      Daniel Mbugu.

Kwa mwendelezo wa mafundisho zaidi ya neno la Mungu tembelea  AMKA UKUE KIRIHO. www.amkaukuekiroho1.blogspot. Na kwa ushauri kuhusiana na maisha ya wokovu tuma ujumbe katika email yangu. www.mbugudaniel@gmail.com. Au wasiliana nami kwa kutuma ujumbe kwenda  kwajia ya sms au wattspp kwa 0758505174/0655505173. Mungu akubariki.

Comments

  1. Ubarikiwe sana mwanangu mpendwa na mtumishi wa Mungu Alie Hai. Songa mbele zaidi katika huduma yako na hiyo ndiyo furaha yangu.

    ReplyDelete
  2. Ubarikiwe sana mwanangu mpendwa na mtumishi wa Mungu Alie Hai. Songa mbele zaidi katika huduma yako na hiyo ndiyo furaha yangu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Asante Mtumishi wa Mungu na mwalimu wangu Mwambeso

      Delete
    2. Ubarikiwe mchungaji

      Delete
  3. Mungu akubariki kwa Somo lako linye nguvu

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular Posts