KABLA YA KUOA JIFUNZE KUPITIA USHUHUDA HUU ILI UYATIMIZE MAPENZI YA MUNGU
Bwana yesu asifiwee, nakusalimu katika jina la Yesu aliye Bwana na mwokozi wa maisha yetu.
Karibu katika makala yetu hii ya AMKA UKUE KIROHO ambapo leo tutajifunza kwa kutumia ushuhuda huu nilio upata mahali flani. Mara yingi kumekuwa na watu wanao kuwa na wito wa kumtumikia Mungu. Na wanapo fika wakati wa kuoa wanashindwa kufanya maamuzi sahihi mwisho wake wanaishi kwa kujuta na kuangaika ndani ya huduma yao. Kupitia ushuhuda huu tunatakwenda kujifunza mambo flani, karibu katika ushuhuda huu;-
Ni asubuhi ya jumapili mchungaji akijiandaa na ibada.
"Nakuona uko hauna utulivu hivi Unakwenda wapi?aliuliza mkewe akiwa kitandani bado.
Ha! Mke wangu wewe si mama mchungaji, hujui kama leo ni ibada?
Mama akapokea;
Umeshaanza mambo yako!,wewe si unajua hali niliyonayo inahitahi uangalizi mkubwa utaniambiaje habari za ibada
Mh!mke wangu....ndio kwanza mimba yako ina wiki 28,kweli kuna sababu ya mimi niahirishe kwenda ibadani kuhudumia watu?
Mchungaji mchungaji mchungaji.... Wewe unafundisha waumini kuhusu kujali wake zao kumbe unafundisha vitu vilivyokushinda hata wewe, vilivyo nje na uwezo wako mnafiki wewe!
utaniachaje na hali hii! Sasa tusilumbane mimi nimekataa nataka ubaki hapa nyumbani huko kanisani waambie viongozi wako waendelee...
"Sikiliza mke wangu ,usitake kuniondolea amani moyoni mwangu katika hii siku... nimekuvumilia saana na manyanyaso yako humu ndani, Mwana mke unajisikia furaha kuniendesha mimi, tendo la ndoa unipangie sawa, hata kanisani unipangie who are you?, kwanini unanilazimisha kutamka kwamba sioni sababu ya kuwa na mke?.
kumbuka, ulinikuta Nina wito tayari natumika, ukumbuke pia sio wewe uliyeniita, na hukuwepo nilipokuwa naitwa!!
Nikwambie tu ukweli, ninaenda kanisani na hakuna baya lolote litakalokupata nitakuombea ila niruhusu niende kanisani please!
He he he nimesema sitaki! hayo maombi ya kuniombea mimi sitaki nakutaka wewe hapa ndani!!!alijibu tena huyo mama mchungaji kwa sauti ya juu.
Mchungaji alijibu kwa upole
"sasa nimtii Mungu au wewe? maana Mungu amenipa Neno kwa ajiri ya kanisa na wewe hutaki huoni kama unapingana na MUNGU, utakuwa na usalama kweli baada ya mimi kutokufanya la Mungu nifanye lako?,
bwana eeh Mungu mwenyewe anasema katika Timotheo wa kwanza 5:8; Mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini. Kwa hiyo wewe mchungaji ni mbaya kulikowapagani wenyewe,usitake kunitisha eti napi ngana na Mungu huo ujumbe wa Neno uliopewana Mungu waambie wazee wako wa kanisa ila sitaki uondoke hapa nyumbani
Mchungaji akajibu;
Nimekusikia ila sijakuelewa, ninaingia kuoga saa hii niende kanisani.....
Akachukua taulo akaingia bafuni.
Mama haraka haraka akaamka kitandani akakusanya nguo zote za mchungaji akachukua na dishi kubwa akaziloweka akamimina na sabuni ya unga akamwambia binti wa kazi fua haraka haraka hizi nguo. Binti akaanza kufua lakini akijiuliza mbona ni safi tu hazijavaliwa?
Mchungaji ile kuingia chumbaji anapaka mafuta, anachana nywere anaangalia nguo zilipokuwepo anashangaa hakuna, anaangalia kwenye sanduku anashangaa empty.... Anamwangalia mkewe ndio kwanza kajif anya kama amelala huku moyoni akimcheka.
Mchungaji aliishiwa pozi, akabaki na taulo peke yake basi, akaangalia track suit akakuta ipo ya chini tu ile ya juu imelowekwa.
Akaingia ndani ya chumba chake cha maombi akalia mbele za Mungu akasema "hivi Mungu ,ulinipa huyu mwanamke ili aniumize awe kikwazo kwa kazi yako?
Mungu akamjibu "SIKUKUPA MIMI HUYO MWANAMKE,BALI WEWE NDIYE ULIYEMPENDA KWA HIYO USINIINGIZE KWENYE HUO UGOMVI NA MKEO.
Alipokuwa akisemezana na MUNGU mlangoni kuna mzee wa kanisa akawa anagonga mlango amekuja kuuliza vipi mchungaji haonekani mpaka muda huu?,
binti wa kazi akamwita mama, mama akamwambia binti amjibu mzee wa kanisa kuwa, mchungaji hatofika endeleeni na utaratibu kahubiri wenyewe.
Kule kwenye chumba cha maombi mchungaji hakutoka na taulo lake huku akiwa na amejifungia. usiku ulipoingia akagongewa ili ale akamwambia binti sintokula mpaka wiki nzima asiandae chai wala chakula chochote.
Kwa siku hizo zote ilikuwa chumba cha maombi tu akakataa mpaka kuoga maji wala kupiga mswaki... simu zote alizima hakupatikana. Aliendelea kuhojiana na Mungu kama mwajiri wake Mkuu, nini hatima ya utumishi wake? nini hatima ya ndoa yake?
Siku ya saba akaingia bafuni na taulo lake akachukua mswaki akamwambia binti amuandalie uji laini ili afungue, akaingia chumbani kwake akamsalimia mkewe shalom!
Mkewe akajibu,
Leo ndiyo unajua kusalimia siku zote hukujua maana ya salamu? eti maombi....!
Hayo maombi mnayoingia kwa kuzira chakula sijui mnasoma biblia za wapi!?? Mtu una kinyongo moyoni,hakuna amani moyoni kwa mkeo, hayo ni maombi feki hayana majibu mnamsumbua tu Mungu wakati ana kazi nyingi za kufanya.
sasa kwa taarifa yako umejikondesha bure bosi pole kwa hilo.
Mchungaji hakujibu Neno badala yake akachukua track suit akavaa na kupaka mafuta akaenda mezani kupata uji.
Baada ya kunywa uji akataka ajipumzishe lakini akaona akwepe kelele za mke ndani akaondoka kwenda kanisani ofisini kwake akajilaza huko.
Usiku hakurudi kesho yake alirudi mchana ,jioni akaondoka na baadhi ya nguo ili jumapili imkutie huko huko kanisani....
na hayo ndiyo yalikuwa ni maisha yake mpaka baada ya miezi miwili baadae siku mkewe anapata uchungu anakimbizwa hospital na yeye akiwepo lakini bahati mbaya alifariki.
Ni baada ya maji ya mimba yajulikanayo kama ‘ amnioni, ’ kuingia kwa bahati mbaya katika mfumo wa damu ya mama alipokuwa akijifungua...madaktari walifanikiwa kuokoa mtoto peke yake
Tatizo hili linajulikana kama Amniotic Fluid Embolism ambapo Maji ya mimba yanapoingia katika mfumo wa damu, husafirishwa na mishipa ya damu hadi kwenye moyo na katika mapafu na kusababisha mzio hatarishi ambao humfanya mzazi kushindwa kupumua na moyo hushindwa kufanya kazi.
Tatizo hili pia husababisha damu kupoteza uwezo wake wa kuganda na kumsababishia mama anayejifungua tatizo la kupoteza damu nyingi kwa kuvuja bila kikomo.
Ndilo lililokuwa limempata mama mchungaji...
Kwenye yale mazishi mchungaji alilia akasema mke wangu we nenda tu.....najua hayo ndiyo mapenzi ya MUNGU, NA kama utakuweko mbinguni nitakukuta lakini wacha mimi nitimilize mwendo wangu.
Sitaki kuendelea kuzungumza kilichoendelea baada ya mazishi lakini mchungaji anaendelea kuchapa kazi na haonyeshi kama ako na nia tena ya kuoa yule mtoto alimpa jina la "ASANTE"
TUWAOMBEE WATUMISHI WA MUNGU
Mitume,manabii,wainjiristi,waalimu na wachungaji waimbaji pamoja na wake zao, mapito yao ni makubwa hujui tu! Ukiwa katika maombi yako binafsi kumbuka kumbeba baba yako wa kiroho,na Mungu ataanza kukushirikisha mengi anayopita......
Kumbuka nyuma ya kila mafanikio yupo MWANAMKE na nyuma ya kila uharibifu yupo MWANAMKE pia.
Nikisimulia haya usiseme ni Story Ila ni kweli kabisa
Mambo niliojifunza katika ushuhuda huu
- Waweza kuwa unatamani kumtumikia Mungu lakini Mke wako akawa kikwazo kwako, kwa maana ukimuona mke wa mchungaji alikuwa kikwazo kwake tena alikuwa akitumia Biblia kama kielelzo cha kuipinga huduma yake.
- Unaweza kuoa mke ukazani ametoka kwa Mungu kumbe ametoka ndani ya tamaa yako mwenyewe, ukisoma ushuhuda huu utamuona mtumishi wa Mungu akimuuliza Mungu na kumlaumu juu ya mke wake aliye mpatia. Na Mungu anamjibu kwa kumwambia kuwa huyo mke hakutoka kwa Mungu bali ni mtushi tu ndiye aliye mpenda.
- Suala la ndoa ni la Kuomba kwanza kabla ya kuchukua maamzi ya tamaa ya Mwili.
Mambo ninayo taka kukushirikisha katika maamuzi yako ya kuoa au kuolewa.
- Jambo la kwanza kabla ya kuoa au kuolewa unatakiwa umwombe Mungu ili awe msaada kwako kwa maana yeye ndiye anaye jua mtu atakaye kufaa katika maisha yako, kumbuka suala la ndoa nila muhimu sana kwa kuwa linaleta amani katika maisha ya mtu, vilevile suala la ndoa laweza kuwa kikwazo na likakufanya usiwe uumie maisha yako yote ya ndoa. Kwa hiyo ili uepukane na hili unatakiwa umwombe Mungu kwanza.
- Waweza kutumia hekima za kibinadamu kutafuta mtu sahihi kwako wa kufunga naye ndoa na ukaishia kuumia, ni Mungu pekee ndiye akupaye yule anaye kufaa. Mitali 19;14 "Nyumba na mali ni ulithi apatao mtu kwa Babaye; Bali mke mwe busara, mtu hupewa na Bwana". kutokana na kifungu hiki ni wazi kabisa ya kwamba mke mwenye busala mtu hupewa na Bwana.
Nakutakia safari njema ya kutimiza makusudi yako ya kumpata Mwenzi wako wa maisha
Mpendwa njia rahisi ya Mungu kushugulika na mahitaji yako ni kumtegea yeye yaani kuokoka, kama bado hauja mwamini Yesu au ulikuwa umeokoka na ukarudi nyuma Sali paoja nami sala hii ya toba na Mungu atakusamehe na kuku safisha Dhambi zako zote. Hakikisha unapo omba toba hii omba kwa kumaanisha na umalizapo usirudie dhambi tena bali mfuate Mungu ili ajidhihirishe katika maisha yako kwa uweza wake wote.
Comments
Post a Comment