IJUE NGUVU YA MAOMBI YA IMANI PASIPO MASHAKA SEHEMU YA 1
Bwana yesu asifiwe, nakusalimu katika jina la Yesu aliye Bwana na mwokozi wa maisha yetu.
Karibu katika makala yetu hii ya AMKA UKUE KIROHO ambapo leo tutakwenda kujifunza kuhusu Maombi ya imani pasipo shaka.
Maombi ni mawasiliano baina ya pande mbili, Maombi kwa MUNGU ni mawasiliano baina ya mwanadamu na Mungu ambayo huimarika katika majawabu yatokayo kwa Mungu.
Lengo la somo hili ni kuhimarisha mawasiliano yako na Mungu katika maombi.
Katika somo hili tutaenda na Yakobo1;5-7 "Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa. Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yoyota; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililo chukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku. maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana"
Maombi ya imani ni yale yasiyo kuwa na shaka ndani yake, sio shaka tu bali shaka ya aina yoyote maana ukiomba kwa shaka kamwe hauta pokea kwa Bwana.Kumbuka maana ya "imani ni kuwa na uhakika wa mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyo onekana"( Waebrania 11;1.), na kumbuka kwamba maana ya uhakika ni kutokuwa na mashaka au wasiwasi wa aina yeyote, na uhakika unakuthibitishia ya kwamba kile unacho kiomba au kitarajia ni lazaima kipo au kinakuja. Nandio maana katika Yakobo 1;5-7 inasema na aombe kwa imani pasipo mashaka kwa kua imani ni uhakika.Ukiwa na masha katika maombi tambua moja kwa moja ya kuwa hauna imaani , na kama hauna imani usitegemee kupokea majibu kutoka kwa Bwana maana Bwana huwajibu wale wanao mwamini katika maombia yao.
Uombapo usiombe kwa mashaka maana mashaka ni kama wimbi na sifa ya Wimbi ni kufuata mwelekeo a upepo unako elekea, hivyo kama upepo ukivuma kutoka maskazini kwenda mashariki wimbi hufuata na kama upepo ukigeuza kutoka kaskazini kwenda kusini wimbi nalo hufuata ndivyo alivyo mtu wa mashaka, kwahiyo mtu wa tabia kama hizi katika maombi asizani ya kuwa atapokea kwa Bwana. ooo Bana Yesu asifiweee...
Maombi yenye imani pasipo mashaka ni kama kutembea huku ukienda sehemu unayo ifahamu, kwa mfano mtu anaye tembea kwenda kwao anapo pafahamu uwe na uhakika hawezi kupotea hata siku moja hii ni kwa sabau anafahamu anapo kwenda. Ndivyo yalivyo na mambi yasio na shaka kwa kuwa humfanya mtu atembee huku akitegemea kupokea kile alicho kiomba kwa Bwana. Ooo haleluyaaa.
Unatakiwa uombe kwa imani pasipo mashaka maana mashaka, mashaka yatakufanya usipokee. Mimi sijui ni wakristo wa ngapi ambao huandika maombi yao huku waki yawekea vema kwa yale yanayo jibiwa, ila ninacho kifahamu ni kwamba wenge huwa wanaomba juujuu tu huku wakizani ya kuwa Mungu amesha wajibu kumbe bado wanaishai pasipo kuona maokeo ya kile wanacho kiombea, na hii nikutokana na kutokuamini kwao.
Nasema kwa sababu ya kutokuwa na imani kwa sababu kama wangeomba kwa imani nilazima wangepokea kuotoka kwa Bwana. Kumbuka si kuomba tu kwa ajili ya mapepo na wachawi bali Biblia katika Yakobo inatueleza ya kuwa hata ukipungukiwa na hekima napo unatkiwa kwenda kwa Mungu ili akupatie hekima ipitayo hekima zote za kibinadamu, ili uipokee hekima hiyo au lolote uliombalo unacho takiwa kufanya ni kuomba kwa imani timilifu.Na ndio maana Biblia katika Wagalatia 3;7 ina thibitisha yakuwa wale walio na imani hao ndio wana wa Ibrahimu, kumbuka katika agano jipya tunazipata ahadi za Mungu alizo mwahidi Ibrahimu kupitia Yesu kristo kwa njia ya imani.
U napo isoma Biblia unatambua ukweli kabisa ya kwamba Ibrahimu aliitwa baba wa imani na kuwa rafiki wa Mungu kwa sababu ya kuamini, hivyo hata wewekama unahitaji kuwa rafiki wa karibu wa Mungu ni lazima utembee kwa kumwamini yeye kwa kila ulitendalo na kila umwombalo, kumbuka sio kuamini kwa wasiwasi bali kuamini kwa Imani timiifu isiyo na mashakandani yako.
Katika maombi ipo siri ya ajabu sana ambayo imefichika katika Imani, kwa kile unacho taka Mungu akujibu jitahidi sana kuomba kwa imani maana pasipo imani kamwe haiwezekani kumpendeza Mungu, siri hii itakusaidia sana kama utaiweka katika uhalisia wa vitendo.
Katika maisha ya wokovu nimeona majibu ya maombi yangu yakijibiwa kwa haraka sana pale nilipo kuwa nikiomba kwa imani hivyo mpendwa kama unataka kujibiwa maombi yako usihangaike kutafufuta jawabu ingine tofuti na kuomba kwa imani maana katika imani ndimo kuna majibu tosha ya maombi yako.
Kitu kingine ninacho kushirikilisha ni kuhusu kuishi kikamilifu katika maisha ya wokovu maana kuna nguvu ya kipekee sana inayo chochea maombi ya imani nayo inatoka katika Roho Mtakatifu ambaye huwa ndani ya wale wote wanao ishai maisha ya kumtegemea Mungu pasipo kufuata tamaa za mwili, hivyo unapo ishi maisha matakatifu Roho Mtakatifu atakusukuma kuomba kwa mzingo na kwa imani katika maombi yako yote haswa yaliyo mapenzi ya Mungu kwako.
Na njia ya kuishi maisha matakatifu ni kuokoka, kama bado hauja mpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa Maisha yako nakuomba usali kwa kumaanisha katika sala hii inayo fuata na ukisha maliza utakuwa umeokoka na kuishi kwa mapenzi ya Mungu.
Sema "Eeh Bwana Mungu, ninakuja mbele yeko, mimi ni mwenye dhambi, nimekutenda dhambi kupitia matendo yangu, kusema kwangu, kuwaza kwangu na kwa dhambi zakujua na za kutokujua, Eeh Bwana Yesu ninaomba unisamehe, nisafishe kwa Damu yako ya thamani, nifute jina langu kuwenye kitabu cha hukumu na uniandike kwenye kitabua cha Uzima wa milele, Eeh Bwana Yesu nakuja mbele zako kuanzia siku ya leo nifinyange moyo wangu, nafsi yangu na roho yangu kama upendavyo wewe, Amina.
Mpendwa kama umesali sala hii fupi kwa kumaanisha tayari umeupokea wokovu, unatakiwa utafute kanisa lililo karibu yako lenye kumuabudu Mungu wa kweli na uungane nao kwa ajili ya kukua kiroho.
Mpendwa kama umesali sala hii fupi kwa kumaanisha tayari umeupokea wokovu, unatakiwa utafute kanisa lililo karibu yako lenye kumuabudu Mungu wa kweli na uungane nao kwa ajili ya kukua kiroho.
vile nakuomba ujitahidi kuepuka maisha ya Dhambi, maana ni dhambi pekee ndiyo itakayo kutenga na uso wa Mungu.Nakutakia maisha mema ya wokovu,Wako mpendwa katika KristoDaniel Mbugu.Kwa mwendelezo wa mafundisho zaidi ya neno la Mungu tembelea AMKA UKUE KIRIHO. www.amkaukuekiroho1.blogspot. Na kwa ushauri kuhusiana na maisha ya wokovu tuma ujumbe katika email yangu. www.mbugudaniel@gmail.com. Au wasiliana nami kwa kutuma ujumbe kwenda kwajia ya sms au whatsApp kwa 0758505174/0655505173. Mungu akubariki.
Somo hili litaendelea kataika sehemu ya pili, karbu sana
Mungu akubariki mtumishi
ReplyDeleteUbarikiwe pia
DeleteAmina kaka mimi nibinti napenda maisha ya wokovu ila na shindwa sielewi kwanini
ReplyDeleteNitafute kwenye namba 0758505174 nikwambie cha kufanya , Kumbuka pekeyako hauta weza ila kwa Msaada wa Roho mtakatifu utashinda ya dunia na kuishi maisha matakatifu
DeleteBarikiwa sana na Mungu mtumishi kwa neno zuri lenye ujumbe mzuri
ReplyDeleteAmeni Ameni barikiwa sana Na kazi nzuri
ReplyDeleteMungu wa mbinguni akutunze na akuhifadhi
ReplyDeleteAmina amina Mwalimu.
ReplyDeleteAmen mtumishi
ReplyDelete