NGUVU YA MTAZAMO KATIKA MAGUMU UNAYO YAPITIA
Bwana Yesu asifiwe mwana wa Ufalme, nakusalimu katika jina la Yesu kristo aliye Bwana na Mwokozi wa maisha yetu. Namtukuza Mungu kwa ajili ya kukupatia nafasi hii Muhimu kwa ajili ya kujifunza somo hili litakalo kuvusha kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Usomapo somo hili nakuomba kupitia Roho mtakatifu uwe na Kalamu na Daftari kwa ajili ya kuandika kile ambacho Roho wa Mungu atakusemesha ndani ya somo hili.
Lengo la somo hili; ni kukupatia msukumo wa kumtazamMungu ndani yako akiwa msaada wa kukuvusha katika magumu yote unayo yapitia.
Na katika somo hili tuweka msingi wetu na kile kitabu cha Mithali 23:1a "Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo..."
Bwana Yesu asifiwe Mwana wa Mungu aliyeko juu mbinguni na Duniani kwa watu wote, katika maisha ya hapa Duniani katika safari yetu ya maisha tunakutana na changamoto mbalimbali ambazo kwa hakika pasipo msaada wa Bwana twaweza anguka. Yamkini msomaji wangu unaye soma makala hii lipo eneo ambalo umekwama na umejitahidi kwa hali zote kutafuta msaada na haujaupata, napenda tu kukusihi ufuatilie somo hili hadi Mwisho maana lipo kwa ajili ya maisha yako. Ni mfululizo wa somo lihusulo imani kwa njia ya mtazamo wako wa Ndani juu ya Mungu unaye mwamini na kumtumikia.
Unapo kisoma kile kitabu cha Mhubiri 3:1-8 unatazama majira mbalimbali ambayo kila mwana Damu yeyote yule huyapitia, nitanukuu baadhi yake, Mhubiri 3:1-4 "Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu. Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung'oa yaliyopandwa; ... Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza..." Mfalme Sulemani kupitia kitabu chake cha Mhubiri anatueleza wazi juu ya nyakati na majira ambayo mwanadamu yeyote yule lazima ayapitie. Suala linakuja kwenye Mstari wa nne pale mwanadamu anapo pitia magumu afanye je katika kipindi hicho.
Yamkini Umeteseka sana au unapitia kipindi ambacho ni kigumu sana katika eneo ulilopo na unahitaji kumuona Mungu akikuvusha salama sawasawa na mapenzi yake, Napenda tu nikutie moyo ya kwamba wewe si wa kwanza kupitia Magumu kama hayo bali wapo walio pitia zaidi tena wengine yakukatisha tamaa zaidi yako, baadhi yao waliweza kuvuka na wengine hawakuweza kuvuka, sasa wewe nakuombea Kwa Mungu uwe ni miongoni mwa wale watakao vuka salama na kuwa ushuhuda kwa wengi.
Mara nyingi watu wanapo kutana na changamoto mbali mbali katika maisha yao huwa wanajawa na hofu na kukata tamaa, baadhi yao huliona tatizo ni kubwa kuliko vitu vyote, na wengi wao hujiona kuwa wao ndiyo wa kwanza na Dunia nzima ndio wenye changamoto, unatakiwa ufahamu Kwamba kwa hali zote unazo zipitia ipo nguvu kubwa itakayo kusaidia wewe kuvuka ambayo imejificha ndani ya Mtazamo wako juu ya changamoto ya ugumu unao upitia,
Kumbuka Mithali 23:1 a "Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo..." kile unacho kiona ndani ya Nafsi yako juu ya msaada wako katika ugumu huo ulionao ndio utakavyo kutokea, Mithali inatueleza ya Kwamba aonavyo nafsini mwake ndivyo alivyo, Ndani ya Nafsi ndimo ilimo Akili na fikra zote, kwa hiyo Biblia inavyo ongelea Vitu vinavyo jengeka ndani ya nafsi maana yake inalekeza fikra,mawazo au akilini mwako. Unapo litazama tatizo ndani yako kwa jicho la kuvuka uwe na uhakika kwamba ipo nguvu itakayo jengeka ndani yako ya kukuwezesha kupiga hatua ya ushindi, Nahapo ndipo utajua kwa nini neno la Mungu linasisitiza ya kwamba aliyemo ndani yenu ni mkuu kuliko aliye katika Dunia ( 1yohana 4:4).
Ipo nguvu ya pekee sana pale unapo pata msaada Flani wenye kukuvusha mapito yote unayo yapitia, Hiajalishi ni mambo ya uchumi, kuachwa na Mpendwa, kuachwa na mwenza wako uliye Mpenda sana, Biashara yako Kudorola,Magojwa na vifo katika familia yenu, Kuteswa na Nguvu za giza au kukwama katika masomo yako. Katika hali zote unazo zipitia unatakiwa uwe lmara na kumtazama Mungu akikuvusha hali hizo.
Nakumbuka miaka Flani nilipo anza kuokoka yapo magumu niliyoyapitia kwa nyanja zote za maisha, kabla sijafahamu juu ya Mtazamo Juu ya uweza wa Mungu niliweza kujiona kuwa sifai, niliona kuwa shetani ananionea na niliona watu wote kuwa si wema kwangu maana hawakuweza kutatua shida zangu, nilainza kulaumu ndugu zangu kuwa ndio chanzo na sikutambua kuwa ni kipindi tu ninapitia, Lakini baada ya kutambua kuwa Mungu anaweza kuninyanyua kutoka hali hiyo niliongeza msukumo wa maombi na shukrani juu hata ya hayo magumu niliyo yapitia, huwezi amini kila changamoto niliyo mtanguliza Mungu kama mweza wa yote niliweza kuvuka salama, zipo zilizo chukua Muda mrefu lakini nilimuona Mungu akinivusha.
Hata wewe hapo ulipo hilo tatizo na changamoto unayo ipitia sio kubwa ya Kumshinda Mungu, unatakiwa Umuone Mungu akikuvusha, na mtazamo wako wa ndani utahimalisha imani yenye kuleta matokeo makubwa maishani mwako.
Tunapo Mtazama Mtumishi Mungu Yeremia katika Yeremia 1, tunaona Mtazamo wake juu ya huduma aliyo pewa na Mungu, Yeremia baada ya kupewa wito wa kuwa nabii wa mataifa, licha ya kwamba yeye ndani yake alijiona kuwa Mtoto na asiye weza kusema chochote Yeremia 1:6, lakini tunapo usoma ule mstari wa 7 na wa 8 katika sura hiyo hiyo Mungu anamkataza kujitazama kama Mtoto na akamwambia kabisa asiogope juu ya yote maana yupo pamoja naye ili amuokoe, Ulisha wai jiuliza nini alikuwa analenga juu ya Yeremia?, Mungu alikiuwa analenga Kufunguka kwa Fikra zake ndani yake ili zimtazame yeye kama mweza wa yote katika kumfanikishia Huduma aliyo pewa,
Haijalishi una maadui wakubwa kiasi gani ama ni mtoto kiasi gani lazima kwa hali zote amuone Mungu mweza wa yote . Oooo Bwana Yesu asifiwe, nilazima uwe na fikra pana ndani yako juu ya Mungu kukuvusha ili upelekapo maombi juu ya shida na changamoto ulizo nazo umuone akikupigania na kuvusha.
Nifunzo la muhimu sana pale unapo watazama watumishi wa Mungu watatu, yaani Shadraka, Meshaki na Abednego hata wakati wa mateso yao walimuona Mungu ndani yao akiwavusha, wasomaji wa Biblia wanafahamu kabisa juu ya kisa hiki ya kwamba iliwekwa sanamu ili taifa zima lisujudu, na zikawekwa adhabu ngumu za papo kwa papo ya kwamba yeyote asiye sujudia ile sanamu ni lazima kutupwa katika tanuru liwakalo moto, " Ndipo Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakajibu, wakamwambia mfalme, Ee Nebukadreza, hamna haja kukujibu katika neno hili. Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto; naye atatuokoa na mkono wako, Ee mfalme. Bali kama si hivyo, ujue, Ee mfalme, ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako, wala kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha."(Danie 3:16-18). Nimaneno mazito sana waliyo yatumia watu hawa, kipindi wenzao wanaona adhabu ya Mfalme haihepukiki kwa vyovyote, kina Shadraka wao ndani yao waliona Mungu akiwavusha, na ndiyo maana uki fuatilia kisa hiki utaona maajabu ambayo Mungu aliwatendea watu hawa katika magumu na changamoto walizo kutana nazo ya kwamba hata moto ulio chochewa mara saba kwao hakikuwa kiwazo.
Haijalishi unapitia taabu gani wewe Mtazame Mungu tu kama jemedali Mkuu wa kukuvusha nawe utaupokea utukufu wake katika pito lako. Hata Daniel katika maandiko tunatazama ya kwamba msimamo wake ndani yake ndio ulio msaidia hata kulishinda jaribu gumu la kutupwa ndani ya tundu la simba, si rahisi kuona unatupwa kwenye wanyama wakali kama hao huku ukiendelea na msimamo wako na Mungu unaye mtumikia bali ina hitaji ujasili wa kutosha unao anzia ndani yako.
Ilikuwa ni hali ngumu sana kwa viongozi wa Israeli kipindi cha uongozi wa Mussa na Haruni pale walipo tuma wapelezi kwenda kuipeleza nchi ya kaanani, Biblia inatueleza wazi juu wa matumaini ya wana wa Israeli Mungu, lakini pale wapelezi walipo rudi na kuleta taarifa mbaya katika Kundi za kuwatia hofu, taifa zima isipo kuwa wachache tu walimunung`unikia Mussa na Haruni, na kujiona Nafsi zao kama Mapanzi,
Kumbuka tulipo anzia unapo zungumzia juu ya Nafsi unagusa mtazamo, kwa maana nyingine walijitazama kama wadogo kiasi cha mapanzi na wakaanza kupiga kelele na kulaumu usiku kutwa kiasi cha kumfanya Mungu achukie, lakini taarifa hizohizo zilikuwa tofauti na Fulsa kwa Imani na Mtazamo wa Yoshua mwana wa Nuni na Kalebu wao licha ya kuona wengi wakihofu, wao walimuona Mungu akiwavusha hata katika nchi hiyo ilao watu, ukiendelea kufuatilia kisa hiki utatambua kuwa Mungu alikasilika na kuachilia adhabu juu yao kwa sababu ya mitazamo mibaya.
Usicho kijua juu ya akili ni kwamba pale unapo tazama upenyo wa Mambo katika akili, unachilia imani yenye kuwezesha nguvu ya Roho Mtakatifu katika kukusaidia kuvuka katika Magumu yako, Neno Usiogope kwenye Biblia lime shamili sana, Mungu anataka tusiogope kwa sababu yeye alisha jitoa kwa ajili ya maisha yetu, na Neno lake linazidi kutusisitiza tunyenyekee juu ya mkono wake kwa maana yeye ajishulisha sana na mambo yetu.
Hakuna Mtu aliye Mkimbilia Mungu kwa kuhitaji msaada na Mungu aka muacha, hii ni kwa sababu yeye anajishulisha sana na mambo yetu, Unacho takiwa wewe kufanya katika mapito unayo yapitia ni kuendelea kumtama Mungu kama msaada wa Magumu yako.
Ujue tunapo jitoa muda wetu kwa ajili ya kukufundisha haya na kukuandikia makala tambua kabisa kuwa Mungu ameliweka kusudi ndani yako ambalo unatakiwa kulitimiza, na ndiyo maana Roho Mtakatifu amekupitisha katika makala hii uisome.
Majaribu ni mtaji wa kukuwezesha wewe kupiga hatua, hata katika magumu na mitihani ya kila namna bado Mungu yupo kwa ajili yetu, anajishugulisha sana na maisha yetu na hana kingine cha kumfanya asitusikie sisi tumuitapo, Kumbuka sisi katika Kristo tumefanyika wana wa yeye aliyeko juu na ndiyo maana ninasema hakuna namna ya yeye kuacha kutusikia na kutujibu maombi yetu, kumbuka ya kwamba sisi ni wazao wa teule na walithi pamoja na Kristo kupitia Damu ya Yesu, na hiyo Damu ndiyo imetuunganisha na Mamlaka ya Kimungu.
Muite Mungu, Mtazame yeye ndani ya magumu yote, ishinde hofu ambayo inaletwa na adui ya kukufanya usifike hatima ya ushindi wako, narudia kukuhakikishia tena ya kwamba yeye ni mwaminifu sana na kwake hakuna majuto, hata kama majibu yata kawia lakini yeye atabaki kuwa Mungu na msaada kwetu kwa kuwa ipo siku atatufuta machozi,usilie kwa yote yanayo kuumiza wewe mwambie Mungu atete na wale wote wanao tena na wewe, apigane na wanao jipanga kupigana na wewe,
Na hakuna siraha itakayo inuka juu yako na ikapata kufanikiwa, wala ndimi zote zinazo kulaani zitahukumiwa kuwa mkosa, na huu ndiyo uhakika tulio nao ya kwamba tukiomba neno lolote sawasawa na mapenzi yake atatujibu.... Ooooo Bwana Yesu asifiweeee..
Yeye ni mzura sana, ni Mkombozi wa maisha yetu, alisha maliza yote msalabani Kalvary kwa ajili yetu na ndiyo maana mapepo, majini, mizimu na roho zozote zenye uove kama hazitatuweza kama tukiwa ndani yake yeye.
Yesu ni mshindi juu ya maisha yetu, hauwezi jua raha ya wokovu Mpaka umejitoa kikamilifu kwa Mungu na kutubu na kuacha uovu wako wote, na haijalishi umeumizwa kiasi gani, kamwe usilipize kisasi maana hiyo si kazi yako kisasi ni juu ya Bwana. Mungu hua hapendi kabisa kutuona tunahangaika, hata kama tumo ndani ya Mateso yeye huwa anatengeneza malango wa kutokea.
Mkumbuke Ayubu licha ya mke wake kumkimbia na kumtaka amkane Mungu afe lakini Ayubu alimuona Mungu na kumtegemea kama msaada na akayashinda yote, hata kama unalia upo wakati wa kufutwa machozi ndani ya Mungu, kumbuka hata miaka iliyo liwa na Dumadu na nzige yeye amehaidi kuilejesha yote kama utamwamini...Oooh Bwana Yesu asifiweeeee...
Unasema nifanyeje ili niyaone haya, unacho takiwa ni kukaa karibu na Mungu na umwamini yeye tu peke yake, yeye ni nguvu yetu, hata unapo pita kwenye bonde la uvuli wa Mautin yeye bado ni msaada kwako, hata kama ukitengwa na Dunia nzima bado yeye atakufuta machozi na kukupatia raha na amani ya moyo wako... Halleluyaaaaa......
Ooooh shuhuda ninazo nyingi juu ya Yesu huyu ya kwamba anaokoa na anaponya, si kwa kusema tu bali tumeziona shuhuda na matendo yake makuu katika maisha yetu na maisha ya wengine.... Ili uzipate hizi nguvu na hizi baraka ni lazima uokoke yaani umkabidhi Mungu maisha yako yote na umtazame kama msaada wako
Comments
Post a Comment