VITA YA KUOA NA KUOLEWA JUU YA WATU WENYE NIA YA KUFANYA MAPENZI YA MUNGU KATIKA MAISHA YAO

Bwana yesu asifiwe mpendwa,

                                                                                                                           

Nakusalimu katika jina la Yesu kristo  aliye Bwana na mwokozi wa maisha yetu.




Karibu katika makala yetu hii ya AMKA UKUE KIROHO   ambapo leo tunakwenda kujifunza jinsi ya kupata mchumba aliye kusudiwa na Mungu kwako,  kwa kijana ambaye anapenda kuhishi maisha ya kumtukuza Mungu lazima awe na maono ya kupata mke ambaye atakuwa furaha kwake kwa kulitimiza kusudi la Mungu.

Kumekuwa na kiu kubwa kwa vija wanao mjua Mungu juu ya  kupata Mke mwema. Nawengi wamekuwa wakihitaji mafundisho ya karibu kuhusiana na hili maana hawapendi kukosea katika suala la kuoa au kuolewa.

 Nikweli kabisa ya kwamba ili uweze kutimiza mapenzi ya Mungu lazima umtegemee Mungu kwa kila jambo, kwa hiyo unapo fikia wakati wa kuoa  au kuolewa unatakiwa kuwa karibu sana na Mungu ili akupatie mke ambaye atatimiza kusudi la Mungu katika maisha yako. Katika somo letu la leo ninakushirikisha ujumbe huu ambao Mungu aliweka ndani ya mtumishi wake Mwl M.Mwambeso ili awashirikishe vijana jinsi ya kufanya pale wafikiapo wakati wa kuoa au kuolewa. 

Karibu tuanze sote katika somo hili;-

Ujumbe huu ni muhimu sana kwa vijana wote ambao hawajaoa au kuolewa katika ujana wao wa kumtegemea Mungu kwa kila jambo,  na ninatamani karibu kila kijana aliyeokoka aupate ujumbe huu wa muhimu sana katika maisha yake ili iashi kwa kufanya mapenzi ya Mungu.
Ninaposema kufanya mapenzi ya Mungu ni zaidi ya kutumika, kwasababu unaweza ukatumika na usifanye mapenzi ya Mungu. Unaweza ukatumikia wanadamu au dini yako na usimtumikie Yesu katikati ya wanadamu kama alivyofanya Sauli kabla hajakutana na Yesu katika barabara ya Dameski.
Shetani hana shida na watu wanaotumikia dini kama dini na sio Yesu Kristo. Shetani hana shida na watu waliookoka na hawana mpango wa kumzalia Mungu  matunda katika maisha yao kupitia wokovu wao

Shetani ana vita na wale waliookoka na Wanataka kumuishia Kristo kupitia wokovu wao. Shetani ana vita na wale waliookoka na Wanataka kutembea kwenye ramani yamaisha ambayo Yesu amewachorea wakati anawaleta Duniani bali Shetani ana vita na wale waliookoka na wanataka kubeba majibu ya watu wengine katika kizazi hiki. Shetani ana vita na wale waliookoka na wanataka kuacha alama chanya ambazo zitakumbukwa daima katika kizazi hiki.  Kwahiyo, watu wa namna hiyo *WANA VITA YA TOFAUTI* na watu wengine katika eneo la kuoa au kuolewa kwasababu shetani anajua vizuri kuwa hawa watu wakipata watu sahihi wa kuishi nae wataharibu vitu vingi katika Ufalme wake kupitia combination yao. Eneo la kuoa au kuolewa ni eneo ambalo lina nafasi kubwa sana  ya kuamua hatima ya maisha ya Mtu kupitia nia aliyonayo juu ya kufanya mapenzi ya Mungu katika maisha yake na kuacha alama chanya ambazo zitakumbukwa na vizazi vingi vijavyo kulingana na mipaka ya alichoitiwa na Mungu hapa chini ya jua.

 Hadi nilipofika katika utumishi wangu nimeshuhudia vijana wakijuta na kukata tamaa, nimeshuhudia huduma nzuri za watu zikifa, nimeshuhudia watu wakiacha wokovu kabisa katika maisha yao. Usifanye mchezo kijana hata kidogo.

  • Usije ukafikiria kuwa shetani anafurahia furaha uliyonayo.

  • Usije ukafikiria kuwa shetani anafurahia kuona unamzalia Bwana Yesu matunda kupitia wokovu wako.

  • Usije ukafikiria kuwa shetani anakutazama vizuri juu ya vitu vya thamani ambavyo MUNGU ameweka ndani yako. Yaani vita ni kubwa sana kiasi ambacho unahitaji msaada mkubwa wa Mungu mwenyewe ili uweze kuvuka. Nikuulize swali. "Hivi unajua kuwa shetani anaweza akakutanisha na mwanaume au mwanamke ambaye anajua vizuri kuwa mtakuwa anagombana kila kuitwapo leo, na mtatumia muda wenu mwingi kwa ajili ya kusuluhisha ugomvi wenu badala ya kutumia muda huo kumzalia Mungu matunda. Hivi unajua kuwa shetani anaweza akakutanisha na mwanaume au mwanamke ambaye anajua vizuri kuwa atakuja kuua huduma yako siku zijazo, hata kama kwasasa anaonekana yuko vizuri sana kiroho?.

MAMBO MUHIMU YATAKAYOKUSAIDIA KUVUKA KWA USHINDI JUU YA VITA HII YA KUOA NA KUOLEWA;-   

  1. Mpe Mungu nafasi ya kwanza katika maamuzi yako juu ya kuoa au kuolewa. Vijana wengi wanataka baadhi ya maeneo ya maisha yao wampe Mungu nafasi ya kwanza lakini maeneo mengine hasa eneo la kuoa au kuolewa waamue wenyewe kwa kutumia akili zao na wanamuwekea Mungu mipaka. Haiwezekani mtu akataka kufanya mapenzi ya Mungu katika maisha yake halafu akakataa kuruhusu Mungu ashike nafasi ya kwanza katika maamuzi yake.

  Faida za kumpa Mungu nafasi ya kwanza;

  • Mungu aonae sirini anaijua vizuri mioyo ya watu wake jinsi ilivyo kwa ndani. 1Samweli 16:7"Bwana akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. *Bwana haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali Bwana huutazama moyo".

  • Mungu anajua vizuri mtu ambaye anaweza kuchukuliana nawe katika madhaifu yako. Sio kila mwanaume au mwanamke aliyeokoka anaweza akabeba madhaifu yako na wewe unaweza ukabeba madhaifu yake.

  • Mungu anajua ipasavyo mwisho wa  kila mtu. Mungu anajua vizuri huyo mtu unaetaka kuoana nae atakufa lini, ndio maana nasema ruhusu mapenzi yake ndio yatimizwe na  makusudio yako yanyamaze kimya. Huyo mtu akifa mapema, usianze kumlaumu Mungu wakati umekataa ushauri wake. Gharama yake ni kubwa sana. Viwango vya rohoni;  Haijalishi yuko vizuri sana kiroho kwasasa, bado Mungu anajua vizuri baada ya miaka kadhaa ijayo atakuwaje,  ndio maana nakushauri kuwa usishindane na Mungu pale anapokupa maelekezo ya kuoana na mtu ambaye hajafikia viwango vya juu sana kiroho maana huwezi kujua Mungu ameona atakuwaje huko mbeleni, *ILA* hakikisha kweli Mungu mwenyewe ndio amekusudia.Pata muda mzuri wa kutulia Kwa BWANA na kufanya maombi kwa kufuata mwongozo wa Roho  Mtakatifu. Ni jambo la hatari sana kwa mtu yoyote anayetaka msaada wa Mungu katika eneo la kuoa au kuolewa halafu akaingiwa na roho ya kufanya maamuzi ya haraka haraka kwa kukimbizana na muda. Gharama yake ni kubwa sana.
  1.   
  2. Pata muda mzuri wa kuombea jambo hilo. Ni bora uchelewe kuoa/kuolewa lakini ufanye maamuzi sahihi kwa kuoa/kuolewa ndani ya kusudi la Mungu. Washirikishe watu ambao unaona wanaweza wakashirikiana na wewe katika kuliombea jambo hilo. Usijifanye wewe ni muombaji sana kumzidi Mtume Paulo ambaye yeye alikuwa ni muombaji sana lakini bado alihitaji msaada wa maombi kutoka kwa watu wengine(Warumi 15:30,31). Usijifanye wewe ni mtu wa kukesha sana  kwenye maombi kumzidi Yesu, kwa maana hata yeye alikuwa anakesha sana kwenye maombi lakini bado alihitaji msaada wa maombi kutoka kwa wakina Petro,Yakobo na Yohana. *Ushauri*;Kijana, Kama muda wako wa kuingia kwenye mahusiano haujafika bado, basi nakushauri kuwa anza kuweka akiba ya maombi kwa kuliombea jambo hili taratibu ili huko mbeleni usiwe na pressure kubwa kwa kukimbizana na muda na ukafanya maamuzi yasiyo sahihi.   
  3. Iwapo Mungu amekusadia na umeingia kwenye mahusiano ambayo yako kwenye kusudi lake, basi tengenezeni ratiba ya kuombea future yenu/maisha yenu yajayo. Kumpata mtu ambaye Mungu amekusudia uishi nae usije unafikiri kuwa vita yako na shetani imeisha.Shetani ataendelea kupambana nanyi ili awavuruge. Msipokuwa na ratiba ya kuombea future yenu nawaambia kuwa shetani atawavuruga kweli kweli na msipoangalia mnaweza mkafanya maamuzi ya kuvunja mahusiano ambayo yako kwenye kusudi la Mungu.

 *✝Bwana Yesu akubariki sana.*
Ni maombi yangu kwa Mungu Alie Hai ili akusaidie katika maamuzi yako ya kuoa na kuolewa ili ushinde vizuri hiyo vita na umzalie sana matunda katika kizazi hiki._
 Naibariki Nchi yangu Tanzania, nawabariki vijana wote wanao mtegemea Mungu ulimwenguni kote.Amen
 Ujumbe huu umeandaliwa chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu na mtumishi wa BWANA YESU *Mwl Mandela Mwambeso.*_
_0752 197065_
_0784 136816_
_Email:mwambeso80@gmail.com_
_Ministry facebook page: *Mwalimu Mandela Mwambeso/Glory to God International Ministry*_
 Washirikishe watu wengine ujumbe huu maeneo mbali mbali  Kama ambayo wewe umetumiwa ili uwasaidie katika kuvuka vizuri daraja hili*. 

Nakushauri kama umelisoma somo hili na ukaona una uhitaji wa Mungu kukusaidia katika maisha ya ujana wako, unatakiwa utendee kazi kile ulicho jifunza ili uwe miongoni mwa Vijana wachache walio mtegemea Mungu katika maisha yoa ya wokovu na wakanufaika na msaada wake. Kumbuka kuwa "...Mke mwenye busara mtu hupewa na Bwana." Mithali 19;14. Kwa hiyo kama unataka Mke mwenye busara ya kuifanikisha familia yako ki mwili na kiroho wewe mtegee tu Mungu maana yeye ni msaada wetu.

Mpendwa njia rahisi ya Mungu kushugulika na mahitaji yako ni kumtegea yeye, kama bado hauja mwamini Yesu  au ulikuwa umeokoka na  ukarudi nyuma Sali paoja nami sala hii ya toba na Mungu atakusamehe na kuku safisha Dhambi zako zote. Hakikisha unapo omba toba hii omba kwa kumaanisha na umalizapo usirudie dhambi tena bali mfuate Mungu ili ajidhihirishe katika maisha yako kwa uweza wake wote.

Kama uko tayari kumurudia Mungu  tamka maneno haya yafuatayo kwa kumaanisha. Sema "Eeh Bwana Mungu, ninakuja mbele yeko, mimi ni mwenye dhambi, nimekutenda dhambi kupitia matendo yangu,  kusema kwangu, kuwaza kwangu na kwa dhambi zakujua na za kutokujua, Eeh Bwana Yesu ninaomba unisamehe, nisafishe kwa Damu yako ya thamani, nifute kuwenye kitabu cha hukumu na uniandike kwenye kitabua cha Uzima wa milele, Eeh Bwana Yesu nakuja mbele zako kuanzia siku ya leo nifinyange moyo wangu, nafsi yangu na roho yangu kama upendavyo wewe, Amina. mpendwa kama umesali sala hii fupi kwa kumaanisha tayari umeupokea wokovu, unatakiwa utafute kanisa lililo karibu yako lenye kumuabudu Mungu wa kweli na uungane nao kwa ajili ya kukua kiroho.Nakutakia maisha mema ya wokovu,Wako mpendwa katika KristoDaniel Mbugu.Kwa mwendelezo wa mafundisho zaidi ya neno la Mungu tembelea  AMKA UKUEKIRIHO. www.amkaukuekiroho1.blogspot. Na kwa ushauri kuhusiana na maisha ya wokovu tuma ujumbe katika email yangu. www.mbugudaniel@gmail.com. Au wasiliana nami kwa kutuma ujumbe kwenda  kwajia ya sms au wattspp kwa 0758505174/0655505173. Mungu akubariki


Comments

Popular Posts