IJUE NGUVU YA MAOMBI YA IMANI PASIPO MASHAKA SEHEMU YA 3

Bwana yesu asifiwe, namtukuza Mungu kwa ajili yako kwa siku hii ambayo amekupatia kibahari cha kuendelea kusoma mafundisho yake aliyo yaweka moyoni mwangu kwa ajili yako. Najua ni neema tu mpaka kufikia hatua hii ya kutembelea  ukurasa huu wenye kuleta utukufu kwa Mungu.

Nakukaribisha katika makala yetu hii ya AMKA UKUE KIROHO ambapo leo tutaendelea na somo letu la"IJUE NGUVU YA MAOMBI YA IMANI PASIPO MASHAKA  SEHEMU YA 3. Karibu na Mungu awe pamoja na wewe.

Katika sehemu ya kwanza na ya pili tuliangalia na kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo maombi kwa njia ya imani, sitoweza kurudia tena bali ninakusihi wewe ambaye haukupata muda wa kusoma, waweza kurudia na kusoma ili uwe na mwendelezo mzuri.

Imani katika maombi ndiyo inayo tengeneza mipaka katika yako na shetani na kukufanya ung'are katika ulimwengu wa Roho. Kumbuka Mungu anapo taka kukujibu ni lazima anangalia imani yako katika kile unacho kiombea na kupitia imani hiyo huweza kuleta majibu ya maombi yako. Katika hili leo tutakwenda kujifunza aina mbili za imani katika maombi;-

             AINA  MBILI ZA  IMANI KATIKA MAOMBI
Katika aina hizi mbili za maombi tutangalia jinsi ambavyo maombi ya imani yanavyo leta matokeo ya ulicho kiomba. Nikweli kabisa ya kwamba katika maombi tuna imani mbili zenyekuleta majibu ya maombi yako, ambazo ni;-

  1. Imani ya kuomba ili Mungu asikie maombi yako
  2. Imani ya kupokea ili Mungu  akupe majibu ya maombi yako


      1. Imani ya kuomba ni ile unayo ielekeza mbele za Mungu moja kwa moja wakati wa kuomba huku ukiamini ya kwamba Mungu anasikia, na  imani hii ndiyo huweza kuambatana na nguvu kubwa ya Roho mtakatifu kutoka ndani ya Mtu kulingana na mzigo alio nao katika kile anachokiombea, hii ndiyo inayo sukuma maombi kiasi cha kushusha mzigo wote ambao mtu anakuwa nao.
Tunapo soma katika  Yakobo, neno linasema Yakobo 1;5-6 " Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapae wote kwa ukarimu... ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yoyote, maana mwenye shaka ni kama wimbi la Bahari lililo chukuliwa na upepo, na kupeperusha huku nahuku. Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana."  oooh Bwana Yesu asifiwe, kutokana na yakobo hapa tunatambua ya kuwa unapo kwenda mbele za Mungu na ukamkaribia katika maombi ni lazima uombe kwa imani pasipo mashaka, maana ukisha kuwa na mashaka usidhani ya kuwa utapokea kutoka kwa Bwana. Ooo haleluyah..

Suala si kuomba tu bali ni aina gani ya maombi unayo yapeleka mbele za Bwana, kumbuka si kila maombi unayo yaomba yatajibiwa bali kujibiwa kwako kunategemeana na nguvu ya imani uliyo iweka ndani yake wakati wa kuomba, na si imani tu bali iwe  imani thabiti katika Kristo Yesu,  ooh Bwana Yesu asifiwe...

 Unatakiwa unapo mkaribia Bwana uwe na imani kwa kile unacho kiombea na hii itakufanya uombe kwa uamininifu na kuleta majibu yako mbele za Mungu. Watu wengi hushindwa kuupokea muujiza wao walio utarajia kwa sababu ya kuomba juu juu tu pasipo imani, kumbuka neno linasema pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu, na  kama haumpendezi Mungu huwe na uhakika ya kwamba maombi yako unayo yaomba yatakuwa kama wimbi la bahari linalo peperushwa huku na huku na usitegemee kupokea kutoka kwa Bwana.

    2. Imani ya kupokea ili Mungu akupatie majibu ya maombi, katiika yako,  ni ile ambayo unaielekeza Mbele za Mungu huku ukitarajia kupokea kile ulicho kiomba kwa uhakika, na hii ndiyo imani inayo leta matokeo ya majibu yako kutoka ulimwengu wa Roho kuja ulimwengu wa Mwili ili uweze kumtumaini Bwana katika maombi yako uliyo yaomba. Tunapo soma katika Marko mtakatifu, Neno la Mungu linatueleza kuwa, Marko 11;24 "Kwa sababu hiyo nawaambia, yoyote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mmeyapokea, nayo yatakuwa yenu". Bwana Yesu asifiwe... unacho takiwa ni kuamini kile ulicho kiomba na usubirie majibu kutoka kwa Mungu,  kumbuka Mungu ni mwaminifu naye huliangalia neno lake ili akapate kulitimiza, hivyo kama amehaidi ya kuwa ukiomba na ukamwamini utapata, uwe na uhakika lazima utapata majawabu ya unachomkiomba.  Nakusihi ndugu yangu ya kwamba unapo omba usiwe na mashaka Kwa Mungu ya kwamba hakusikii bali amini tu kupokea majibu ya maombi yako, na ukisha amini subiria upokee kutoka kwa Bwana, na ukweli ni kwamba lazima utapokea kile ulicho kiomba. OooBwana Yesu asifiwe........

Hizi ni aina mbili za maombi ya imani ambazo zitakupatia matokeo chanya sana katika maisha yako endapo utajinyenyekeza mbele za Mungu, na hakuna ambaye alimfuata Mungu katika maombi ya imani akabaki kama alivyo. Tunapo isoma biblia tunatambua imani walizo kuwa naz kina o Shadrack, meshack na Abednego ya kwamba walikataa kuibadu sanamu na walipo tishiwa kulushwa katika tanuru la Moto wao waliendelea kuwa na msimamo wao wa kuto isujudia sanamu, kwanini? kwa sababu walikuwa na uhakika na Mungu wao, na kutokana na hili waliweza kumuna Mungu akiwatetea na kuwapigania katika moto Mkali wa tanuru. Ndivyo na wewe unavyo takiwa kuwa na imani thabiti kiasi cha kuhamisha milima na kupokea majibu ya maombi yako kabla hata hayaja onekana katika macho yako ya nyama. Kumbuka Imani ni kuwa na uhakika, hivyo unavyo kwenda mbele za Mungu uwe na uhakika ya kwamba anakusikia na atakujibu kile ulicho kiomba, Ooo Bwana Yesu asifiwe....

Hakuna shaka katika maombi, na usiwe na shaka kwa sababu aliye kuahidi ni mwaminifu atatimiza ahadi yake katika kila ombi utakalo liomba kwa imani, ili mradi tu liwe linaendana na mapenzi ya Mungu. Na hiyo ndiyo kiu yangu ya kwamba umtafute Mungu kwa kiwango hiki cha imani timilifu ili uyasimulie makuu yake  katika maisha yako, Kumbuka unapo jibiwa maombi imani yako kwa Mungu inaongezeka na kuhimarika katika Yeye.

Maombi ya imani ni lazima yanaleta majibu, hivyo usijaribu  kusema kwamba Mungu hayasikii maombi yako kwa maana ameahidi ya Kwamba sikio lake sio zito hata lisisikie maombi yetu, wala mkono wake si mfupi hata ushindwe kutuokoa. Ooo Bwana Yesu asifiweee..

Ili ufaikiwe katika maombi ni lazima uombe kwa imani iliyo timilifu na ya uhakika, maombi kwa Mungu ni ;-

  • Mungu akusaidie kuomba kwa imani itakayo kupatia matokeo chanya.
  • Mungu akupe uimara wa kumtumikia na kumuabudu yeye katika Roho na kweli.
  • Mungu akupe imani ya kuhamisha milima kiasi cha wewe kuthibitisha ushindi kwa macho yako ya nyama.
  • Bwana akupandishe kwa imani ili usizame na upande viwango vikubwa  mno katika maisha yako.
  • Mungu akuinue katika kuishi na wewe kwa uhakika pasipo mashaka,
  • Na kupitia somo hili la imani ulilo jifunza kuanzia sehemu ya kwanza hadi ya tatu, Mungu aweke mzigo mkubwa wa kukufanikisha huku ukitembea kwa imani kama Ibrahimu'

Namshukuru Mungu kwa  ajili ya kukuwezesha kusoma somo hili kuanzia mwanzo hadi mwisho, nimemuomba Roho Mtakatifu atende kitu ndani yako cha kiutumishi na cha mafanikio katika ulimwengu wa Roho.  Lakini Mpendwa ninao ushauri juu yako ya kwamba Mungu ni mzuri sana katika maisha yetu hasa tunapo mkiri Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yetu, hivyo kama hauja mkiri Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako au kwa kifupi watu wengi husema kuokoka, kama hauja okoka naomba ufuatishe sala hii kwa imani na Mungu atakuokoa na kupandikiza ndani yako uwezo wa kuishinda dhambi huku ukimtumainia yeye. Kumbuka unapookoka tu Mungu anajishughulisha na wewe katika kukupigania kwa kila uombalo na ulitafutalo, hivyo nakushauri usome huku ukiomba kwa imani;-



Sema "Eeh Bwana Yesu, ninakuja mbele yako, mimi ni mwenye dhambi, nimekutenda dhambi kupitia matendo yangu,  kusema kwangu, kuwaza kwangu na kwa dhambi za kujua na za kutokujua, Eeh Bwana Yesu ninaomba unisamehe, nisafishe kwa Damu yako ya thamani, nifute jina langu kwenye kitabu cha hukumu na uniandike jina langu kwenye kitabua cha Uzima wa milele, Eeh Bwana Yesu nakuja mbele zako kuanzia siku ya leo nifinyange moyo wangu, nafsi yangu na roho yangu kama upendavyo wewe, maisha yangu yote nakukabidhi wewe uyaongoze kwa Roho wako Mtakatifu, naomba na kuamini kupitia Jina la Yesu kristo aliye Bwana na mwokozi wa maisha yangu. Amina. 

Mpendwa kama umesali sala hii fupi kwa kumaanisha tayari umeupokea wokovu, unatakiwa utafute kanisa lililo karibu yako lenye kumuabudu Mungu wa kweli na uungane nao kwa ajili ya kukua kiroho. 

vile nakuomba ujitahidi kuepuka maisha ya Dhambi, maana ni dhambi pekee ndiyo itakayo kutenga na uso wa Mungu. Nakutakia maisha mema ya wokovu na Mungu akubariki, 
                         Wako mpendwa katika Kristo, 
                           Daniel Mbugu.
Kwa mwendelezo wa mafundisho zaidi ya neno la Mungu tembelea  AMKA UKUE KIRIHO. www.amkaukuekiroho1.blogspot. Na kwa ushauri kuhusiana na maisha ya wokovu tuma ujumbe katika email yangu. www.mbugudaniel@gmail.com. Au wasiliana nami kwa kutuma ujumbe kwa njia ya sms au whatsApp kwa 0758505174/ 0655505173. Mungu akubariki.


Comments

Post a Comment

Popular Posts