IJUE FAIDA YA KUISHI NDANI YA KRISTO.
Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu, nisiku nyingine tena tuliyo pewa na Mungu kwa ajili ya kujifunza neno lake la uzima, na pia namtukuza Mumgu kwa ajili yako kwa kukupatia muda huu wa pekee sana ambao ni wa muhimu sana katika maisha yako. Najua ni kwa neema tu ya Mungu ndio maana umepata kibari cha kusoma makala hii ya AMKA UKUE KIROHO. Na mimi kama mwindishi wako nakukaribisha sana, lakini cha zaidi napenda kukuomba uandae daftari lako na kalamu kwa ajili ya kuandika vile vyote ambavyo Roho wa Mungu atakusemesha ndani yako kupitia somo hili, ambalo linakichwa cha somo kinachoitwa KUISHI NDANI YA KRISTO.
Lengo la somo hili ni kuhimalisha mahusiano yako na Mungu, ukiwa ndani ya Yesu Kristo.
Bwana Yesu asifiwe Mwana wa aliyeko juu, ni matumaini yangu ya kwamba kupitia somo hili utawafundisha na wengine kuishi ndani ya Yesu
Maisha ya Mkristo niya thamani sana katika Dunia hii na katika Mbingu kwa maana huambatana na shuhuda nyingi zenye kutia moyo na kufariji. Maisha ya Mkristo yanakutana na Changamoto nyingi sana zikiwemo za kiuchumia, kijamii na kisiasa, Tunapo isoma Biblia tuna tambua ya kwamba si kila Mtu aliye mtumikia Mungu alianza moja kwa moja akiwa amefanikiwa. bali wengi wao walianza na maisha ya shida na taabu huku wakimtegemea na kumuamini kama Bwana na mwokozi wa maisha yao.
Maisha ya Mkristo yanapokuwa ya taabu sana, baadhi yao hujitenga na uso wa Mungu huku wakikimbilia kwa shetani na kusau kuwa mapito yao niya muda kitambo tu.
Kwa hapa Tanzania natiwa moyo sana na Mtumishi wa Mungu Mwl Christopher Mwakasege, ambaye huelezea ya kwamba kipindi ana anza huduma alikuwa na hali ngumu sana ya kifedha kiasi kwamba hata viatu vya kuvaa na kubadili haikuwa Rahisi sana kwake, Mwakasege kwa sasa ni Mtumishi Mkubwa sana wa Neno la Mungu Nchini Tanzania, ambaye kupitia yeye watu wengi wameweza kuupokea wokovu kupitia yeye, na taabu za kiuchumi alizokuwa nazo kwa zamani kwasasa haizipo tena Mungu kaisha muinua sana kiuchumi na kihuduma.
Kwa nini nimetoa ushuhuda huu? nimeeleza ushuhuda huu ili kukutia Moyo wewe unaye kutana na changamoto mbalimbali katika maisha yako ya kwamba Mungu ni mwema sana, kupitia changamoto hiyo unayo ipitia, unatakiwa kuelekeza uso wako kwa Bwana ili akuinue kama alivyo wainua wengine.
Na siri ya kuinuliwa kwako na kuvushwa mapito yako, haipo sehemu nyingine isipokuwa Ndani ya Yesu. Na ndio maana katika somo hili nimelipa kichwa cha habari kinacho itwa Faida ya kuishi ndani ya Yesu.
Kuna siri Kubwa sana ndani ya Neno la Mungu kwa wale wote wanao mtegemea yeye na kuimwamini huku wakivumilia shida na taabu wanazo kutananazo , mwisho wa siku huishi maisha yenye furha na amani huku wakisahau shida na taabu.
Ukikaa ndani ya Yesu unakuwa na uwezo wa kumwomba Mungu neno lolote na akakujibu kwa sabaubu ndivyo alivyo hahidi katika neno lake, ambalo vilevile linatuambia ya kwamba yeyeb hulioangalia neno lake apate kulitimiza.
Hii ni faida ya pekee sana ya kwamba tukiwa ndani ya Yesu Mungu anakuwa ni Baba yetu kwa huyo twalia Aba yaani Baba.
Siri ya kutendewa au kujibiwa maombi yako imo ndani ya Yesu, Tunaposioma katika Yohana 15;7 neno la Mungu linatuhakikishia kwamba '' Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa''
Bwana Yesu asifiweee..., sikia ninyi mkikaa ndani yangu maana yake ni kwamba unatakiwa kukaa ndani ya Yesu wakati wote, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ina maanisha kwamba maagizo aliyo kuachia Mungu ukiyahifadhi, hapo ndipo unaambiw ya kwamba ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa, sikiliza neno ombeni mtakalo linakupatia uhuru ya kwamba ukiwa ndani ya kristo kuna vitu ambavyo Mungu anatambua ya kuwa watoto wake wanavihitaji, hivyo neno ombeni lolote linakupatia haki kwa Mungu kujibiwa ombi lako lolote lile lililo mapenzi yake. Oooh Bwana Yesu asifiweee....
Unapo soma 2Wakoritho 5;17 neno linatueleza vizuri kabisa ya kuwa ''Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya" mara nyingi watu wanapo uacha utuwao wa kale wa kutenda uovu na kuanza kupiga hatua kwenda kwa Bwana, utakuta shetani anawakumbusha dhambi zile walizo zitenda kana kwamba hawajasamehewa, sikiliza neno la Mungu linalo tushuhudia ya kwamba, hata imekuwa mtu akiwa ndani ya Yesu Kristo amekuwa kiumbe kipya, ya kale yote yamepita, na tazama yamekuwa mapya, ooh ni neno lenye kututia Moyo maishani mwetu wa kwamba ukisha okoka Mungu anamfanya kuwa kiumbe kipya kwa kuoshwa na kufutiwa Dhambi zake zote kwa Damu ya Yesu, hivyo cha kufanya kwa wewe ambaye umekwisha kumwamini Yesu unatakiwa Kuishi ndani ya Kristo kwa kutenda yale Yote yalio mapenzi ya Mungu, na yale yalio mapenzi ya Mungu yanapatikana kwa kusoma Neno la Mungu ambalo ndiyo taa ya miguu yetu. Oooh Bwana Yesu asifiweeee. Unatakiwa kuishi kama mwana wa Mfalme ukiwa ndani ya Yesu maana yeye ndiye atakaye kuwa kuiongozi wako huku akikulinda na kukuhakikishia yote mema yakupasayo, maana anakuwazia mema, na anajishughulisha sana na mambo yetu, Oooh halaluyaaaa.
Na ndiyo maana inatakiwa kufuata Biblia inavyo sema ya kwamba ''Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote..." Wakolosai 3;16. Kwa nini neno la Kristo likae kwa wingi ndani yenu, kwa sababu katika neno hapo ndipo kuna ahadi za Mungu za kukutia nguvu na kukufanya uendelee kusonga mbele, Oooh hata kama majaribu yatakuja makubwa kama Mlima , yaani ukiwa ndani ya Yesu kristo utakuwa na amani na Furaha kubwa sana yenye kukufanya uvuke hayo mapito unayo yapitia kupitia neno la Mungu alilo liweka ndani yako, Oooh Bwana Yesu asifiweeee....
Biblia inazidi kutueleza ya kwamba "Ninyi, watoto wadogo, mwatokana na Mungu nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia". Ebu pigia mstali lile neno linalo sama kwamba yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia kwenye daftari lako. Oooh Bwana Yesu asifiwe, unatakiwa utambue ya kwamba yeye aliyomo ndani nyenu ni mkuu sanaa kiasi kwamba anazidi yeye aliyopo katika ulimwengu huu, ina maanisha ya kwamba ukiwa ndani ya Yesu unakuwa na uwezo mkuu sana kiasi kwamba hata ukikutana na changamoto za kipepo zitokazo kwa yule adui amabye ni Ibilisi na Shetani ni lazima utashinda, si kwa uwezo wako, bali yeye aliyomo ndani yako ndye aliye mkuu zaidi ambaye ni Roho Mtakatifu uliye mpokea baada ya kumwamini Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako. Na ndiyo maana Biblia inaeleza ya kwamba aliye mpokea yeye anao huo ushuda.
Oooh mimi sijui umekwama wapi bali napenda kukupatia ujumbe huu wa leo alio kuletea Roho mtakatifu ya kwamba unatakiwa kukaa ndani ya Yesu, ambamo ndani yake hakuna majuto kabisa, na ukisha muweka ndani yako upataiwa uwezo wa kuishi maisha matakatifu ambayo yatakufanya uione hiyo mbingu mpya nan nchi mpya iliyo andaliwa kwa ajili ya wateule wa Bwana walio andaliwa na Mungu kwa kusudi la kuhurithi ufalme wa Mbinguni. Basi na mimi nasema ya kwamba "atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu" Efeso 3;20.
Imo nguvu ya ajabu sana pale unapo mwamini Yesu na kukaa ndani yake, unatakiwa ukae ndani ya Yesu ili uhurithi Ufalme wa Mbunguni, kwa wewe uliye okoka napenda kukutia tu moyo ya kwamba Yesu yu karibu kuja, na unatakiwa ujiandae kwa ajili ya ku urithi ufalme wa Mungu, na kwa wewe ambaye haujaokoka unatakiwa kumpatia Yesu maisha yako na uweze kuishi ndani ya Yesu. Nakusihi sana ufanye hivyo kwa maana hakuna muda mwingine, muda tulionao ndio huu ulio kubaliwa na Bwana. Ebu fanya hivyo ili uendelee kuishi maisha matakatifu.
KUISHI NDANI YA YESU |

Comments
Post a Comment