IJUE NGUVU YA DAMU YA YESU SEHEMU YA PILI [2]
Katika sehemu ya kwanza tuliangalia angalu kwa kina mambo kadha wa kadha ikiwemo nguvu ya mambo yanayo tendwa na Damu ya Yesu, kwa kweli kwa wewe uliye tumia maarifa hayo utakuwa na ushuhuda wa Ki Mungu ndani yako. Na leo tutaangalia sifa iliyomo katika Damu, ninapo sema sifa iliyopo katika Damu namaanisha ya Damu yoyote ile, iwe niya mnyama au ndege. Ni mara nyingi mambo mengi ya kustaajabisha yanatokea hapa Dunia ambayo chanzo chake ki katika Damu.
Zipo sifa nyingi za Damu, lakini kwa somo letu la leo tutagusia kidogo baadhi ya sifa hizo, miongoni mwa sifa iliyomo katika Damu ni kama ifuatavyo ;-
- Damu inaogea, na kutamka neno lolote juu ya haki au kitu chochote inachokiona, Kwa mfano ukisoma habari za Kaini na Habili, Biblia inatueleza ya kwamba baada ya Kaini kumuua ndugu yake Habili, damu ya Kaini ilimulilia Mungu kutoka mavumbini ikimtaka Mungu ataende haki, sasa utaelewa kulia maana yake nini, yaani Mtu kaisha fariki na roho isha toweka , lakini bado tunatazama kitu damu inalia kutoka kutoka avumbini. Kumbuka kama Damu inalia inamaanisha inahuzunika, kama inahuzunika ina maana ya kwamba inasononeka, na kama inasononeka inamanisha inasifa zote za kuitwa kiumbe hai. Bwana Yesu asifiweee, unaposoma katika Biblia kwenye kitabu cha Mwanzo 4;9-10 "9 Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?. 10 Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi." Kutokana na Mstari huu tunatambua wazi ya kwamba Mungu alipokea ujumbe wa Habili kupitia Damu iliyo mwagika ardhini.
Na ndiyo maana hauruhusiwi kunywa damu ya mnyama, kwa sababu damu ni uhai, sasa fikiria kwa kina ya kwamba damu inaongea, alafu wewe umechinja mfugo na kunywa damu, na kwa mjibu wa Biblia damu huwa inawasiliana na Mungu, kwahiyo kama ulichinja mfugo na ukanung'unika alafu wewe ukanywa damu yake uwe na uhakika utakuwa na hatia juu ya damu hiyo. Oooh na ndiyo maana Mungu alitupatia viombe vyote tuvutawale, lakini katika kuvitumia kama chakula alisisitiza sana na kukataa juu ya matumizi ya damu yake. Oooo Bwana Yesu asifiowee, ngoja nikupitishe kwenye maandiko kwanza juu ya hili la Damu ya mifugo. Tunapo Soma Mambo ya walawi 17;13-14 "Mtu ye yote aliye wa wana wa Israeli, au wa hao wageni wakaao kati yenu, ambaye amemshika mnyama, au ndege ambaye huliwa, katika kuwinda kwake; atamwaga damu yake, na kuifunika mchanga. 14 Kwa maana kuliko huo uhai wa mnyama, hiyo damu yake ni moja na uhai wake; kwa hiyo naliwaambia wana wa Israeli, Msile damu ya mnyama wa aina yo yote; kwa kuwa uhai wa wanyama wote ni katika hiyo damu yake; atakayeila awaye yote atakatiliwa mbali." Kwahiyo kama Damu ni uhai, maana yake kunavitu inavyo wasilisha na kuvinena, na ndiyo maana katika sehemu ya kwanza tuliangalia namna ambavyo Damu ya Yesu inavyonena mema kuliko ile ya Habili, Ooo Bwana Yesu asifiwee, kunakitu kinatokea katika ulimwengu wa Roho pale unapo itamka Damu ya Yesu, kwa maana ni Damu yenye ushindi, ni Damu yenye uweza, kupia hiyo Damu mapepo yanikimbia, majini yanatimua, mizimu na miungu inatetemeka na kukimbi, O ooh haijalishi unapitia katika hatua gani ngumu za mashambulizi ya kipepo leo niko kukwambia ya kwamba ipo Damu ya Yesu inayo nena mema sana juu ya maisha yako, Mimi nasema wewe tamka tu kwa imani juu ya hii Damu nawe utaona matokeo ya kustahajabisha.
Kutokana na Mapepo kulijua hili hua yanasabisha ajali barabarani, ok ngoja nikufikilishe kidogo juu ya hili, ebu angalia na chunguza kwa makini baadhi maeneo yote ambayo ajali iliwai kutokea na damu ikamwagika, maranyingi utakuta mara kwa mara ajali zinakuwa zinatokea eneo lilelile, na hukuta watu wanashangaa kwa nini ajali ziwe zinatokea eneo lilelile kila mara. Ooo leo nataka nikwambie hii siri ambayo yamkini haukuwai kuifahamu ya kwamba popote inapo mwagika Damu hua kuna Ghadhabu inajivika eneo lile, hivyo kila watu wakipita eneo lile ambalo damu ilimwagika, unakuta ile damu inadai kuendelea kumwagika kwa damu nyingine hivyo kukuta ajali zinaendelea kutokea endeo lilelile. Sasa utakuta watu wa eneo lile wasipo tambua jinsi ya kuomba kwa kunyunyiza na kumwaga Damu ya Yesu katika eneo lile, utakuta ajali zinazidi kutokea, na tunaona watu wa dunia hii wakitumia matambiko ya kipepo kuizindika maeneo hayo wakiamini ya kwamba watapata pumziko. Oooh mimi leo nataka kukwambia kwamba pumziko la kweli li katika Yesu na wala si katika waganga wanao tumia nguvu za giza kutika kupoza mambo.
Fungua pamoja na mimi kitabu kile cha Hesabu, kuna kitu cha ajabu kimeongelewa hapa kinacho husiana na Sheria ya Damu, Hesubu 35;33 ''.... kwa kuwa damu huitia nchi unajisi; wala hapana sadaka itoshayo kwa ajili ya nchi, kwa ajili ya damu iliyomwagwa ndani yake, isipokuwa ni damu ya huyo aliyeimwaga.'' kwa pale Damu inapo mwagika ardhini hua hakuna sadaka nyingine ambayo huweza kuizidi hiyo damu isipo kuwa sadaa ya damu ya yule aliyo imwaga, sasa hapo tulikuwa tunatembea chini ya sheria ya agano la kale, lakini kwa sasa tunayo Damu ya Yesu ambayo yenyewe hua haishindwi chochote, pale inapo tokea ghazabu yoyote ile wewe mwaga tu Damu ya Yesu amabayo ndiyo suluhisho la mambo yote.
Ninao ushuhuda kwa ajili yako, nakumbuka miaka kadhaa iliyo pita niliwai kukutana na vita ngumu sana, ambayo ilihusisha mapambano ya kiroho baina yangu na nguvu za giza, nakumbuka katika ndoto hiyo kulitokea pepo moja ambalo lilikuwa limetuwa kuniangamiza na kunitowesha Duniani kabisa, kipindi napigana hiyo vita niliomba sanaa, hatima lilishindwa na kukimbia baada ya kutoweka kwa hilo pepo, lilikuja lingine amabalo lilionekana linanguvu nyingi zaidi ya lile la kwanza, nilianza kuomba kwa juhudi sana huku nikishindana nalo, nilitumia muda mrefu sanaa mpaka nika anza kuchoka kimwili na hatimaye likatoweka na kukimbia mbio. Baada ya lile la pili kukimbia lilikuja lile kubwa lao ambalo ndilo lilikuwa linawa agiza wengine, nilivyo kuja kiukweli niomba sana kwa sababu lilonekana kuwa na nguvu kubwa sanaa, nilikemea mnoo kwa kutumia Jina la Yesu na Moto wa Yesu lakini halikuonyesha kushituka hata kidigo, baada ya maombi mengi nilichoka mno na kukata tamaa na kuona kuwa nimeshindwa, lakini baada ya kukata tamaa nilisikia sauti ikihimiza niombe kwa kutumia Damu ya Yesu na ikanisisitiza nisikate tamaa, baada ya kuomba kwa kukemea kwa kutumia Damu ya Yesu, lile pepo lilipiga kelele na kuondoka, lilinisemesha kuwa lilishindwa pamoja na washirika wake, lilizidi kusema kuwa lilitumwa kuniua na lilitokea nchi ya Nigeria lakini limeshindwa lenyewe pamoja na washirika wenzake.
Bwana Yesu asiwe mpendwa, lengo la ushuhuda huhu sikupinga maombi mengine bali nikukuongezea mbinu ya kiamaombi wewe kama mwombaji ya kwamba katika maombi yako, ipo nguvu ya ajabu inayo toka katika Damu ya Yesu, ambayo nguvu hiyo huwa haikwamishwi na chochote, na maranyingi inapo shuka hua inatenda mambo mazuri sana.
Kwa wewe unaye kutana na changamoto mbalimbali za kiroho na kimwili, leo napenda kukuambia ya kwamba ipo nguvu ya ajabu sana pale unapo itaja Damu ya Yesu, Kumbuka yeye ndiye aliye utoa uhai wale kwa ajili yabmaisha yetu, na akaimwaga Damu yake kwa ajili ya ondoleo la Dhambi zetu, hivyo mateso yako ameyaona na yupo karibu kukusaidia, cha Muhumu wewe zidi kumwomba tu na kuimani Damu yake ya thamani.
Na kwa wewe ambaye haujamkabidhi Yesu maisha yako kuwa bwana na Mwokozi wa maisha yako, unatakiwa unatikiwa kumkabidhi yeye maisha yako ili ayalinde na kuyatunza.
Siku za mwisho zinakaribia Yesu karibia anarudi dalili tayari zinaonyesha, kwa hiyo hatuna muda wa ziada wa kujiandaa bali muda ulio kubalika ndio huu na nawala useme kuwa utaokoka tu mbeleni, mambo ya mbeleni hauyatambui. kumbuka Kkufumba na kufumbua tu Mwana wa adamu yuaja, na akija atakuja kulichukua kanisa lake, ambalo ndio wale wote walio mpokea yeye kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao.

Comments
Post a Comment