JINSI YA KUJUA KAMA UMETENDA DHAMBI
Bwana yesu asifiwe mpendwa, nakusalimu katika jina
la Yesu aliye Bwana na mwokozi wa maisha yetu.
Karibu katika makala yetu hii ya AMKA UKUE KIROHO
ambapo leo tutakwenda kujifunza kwa njia ya maswali na majibu.
SWALI:
(a) Nitajuaje
kama nimetenda dhambi
(b) Nifanyeje
ili niweze kuishi maisha matakatifu katika
KRISTO
Answer
(a) Maana ya dhambi?
(a) Maana ya dhambi?
Ni kuvunja
sheria za Mungu., na maagizo yake imeandikwa, 1Yohana 3:4 "kila
atendaye dhambi afanya uasi." 1Yohana
5:17 yasema Kila lisilo la haki ni
dhambi na dhambi iko isiyo ya mauti."
*Dhambi, ni msukumo wenye nguvu ambao unatufanya sisi tupende
kuziendea njia ambazo ni kinyume kabisa na mapenzi ya Mungu. Kwa hiyo, badala
ya kubarikiwa kwa kuyafuata mapenzi ya Mungu, tunaadhibiwa kama tutaishi kwa
kuzifuata na kuishi kwa kufuata tamaa za Shetani, ambazo ndizo dhambi. Njia na
matendo ya Shetani ni kinyume kabisa na zile za Mungu. Mungu anazichukia dhambi
(Mithali 6:16-19). “kuna vitu sita anavyo vichukia Bwana, naam,
viko saba vilivyo kwake. Macho ya kiburi, ulimi wa uongo, na mikono imwagayo
damu isiyo na hatia, moyo uwazao mawzo mabaya, miguu iliyo myepesi kukimbilia
maovu, shahidi wa uongo asemaye uongo, naye apandaye mbegu za fitina kati ya
ndugu.”atendaye dhambi ni wa Ibilisi; (au Shetani) kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo.
(1Yohana 3:8).” Atendaye dhambi ni wa
ibilisi; kwa kuwa ibilisi utenda dhambi tangu mwazo. Kwa kusudi hili mwana wa
Mungu alidhihirishwa,ili azivunje kazi za ibilisi.”
MAMBO/ ISHARA ZITAZO DHILISHA
KUWA UMETENDA DHAMBI:
Ø
Kukosa Amani ndani ya moyo:
mtu aliye tenda dhambi siku
zote anakuwa ni mtu aliyekosa amani mbele ya uso wa Mungu. Kwani moyo wake na
nafsi inakuwa katika hali ya mashindano. Mfano ulio rahisi mototo mdogo akiwa
ametenda kosa kwa kujua au kwa kututojua pengine hata kwa bahati mbaya. Mtoto
huwa anakosa amani na kufikria atasema nini kwa Baba au mama pia anakuwa mtu wa
mawazo juu ya adhabu hatakayo pewa. “kuna siku moja nilimfanyia mtu utani wa
kawaida sana lakini akawa amechukia sana. Ghafla baada ya muda nikajikuta nami
nimekosa amani , nikamwendea na kumwomba msamahaa”
*Nawe ukiona huna
amani jaribu kukaa na kutafakari kuona je kuna mahari hukutenda haki?
Ø
Aibu kutawala ndani yako:
Dhambi inamfanya mtu kuwa na
aibu ndani ya moyo wake. Tuna jua ya
kuwa ishara ya kwanza ya Adamu na Hawa kugundua kuwa wamemtenda Mungu dhambi ni
pale aibu ilipo tawala ndani yao. Nakisha kukimbia kwenda kujificha Soma (Mwanzo 3:8-14). “ ...
Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia huko wapi? Akasema nalisikia sautinyako
bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha...” Dhambi kamwe
haiwezi kujificha itajidhirisha tu kwa
namna yeyote hile.
Ø
Upendo wako na Mungu unapungua:
Kuna mtumishi mmoja aliwahi
kusema “ ukiona upendo wako na Mungu umepungua basi na ujichunguze moyoni
mwako”. Dhambi inaondosha upendo baina ya mtu
na Mungu. Mungu alikuwa na upendo mwingi sana dhidi ya mwanadamu, lakini
mara baada ya mwanadamu kumtenda Mungu dhambi upendo wake kwake ulitoweka na kisha
kumfukuza katika bustani ya EDEN (
bustani ya uzima wa milele) na kasha kumpa adhabu.
ü
Utaona
kushindwa kutimiza mapenzi ya Mungu siku zote (kaa ukijua ya kuwa tayari dhambi
imekwisha tawala ndani yako)
ü
Mahusiano
yako na Mungu kuanza kufifia au kutoweka taratibu (dhambi inakawaida ya kuaribu
husiano uliopo kati ya mwanadamu na Mungu).
Ø
Kushindwa kuona/ kupokea Baraka zako kutoka kwa Mungu:
Dhambi inakwaida ya kuzuia;
kufunga au hata kuaribu baraka za mwanadamu, ukiona upokeia baraka yoyote,
mambo yako hayaendi, kila ulifanyalo ufanikiwi. Rudi kaa chini na utafakari ni
wapi ambapo hujaweka mambo sawa na kisha
uweze kuweka mambo yako sawa kwa kufanya toba na kumrudia Mungu.
Ushuhuda:
Kuna mama mmoja aliwahi kuugua kwa kipindi kirefu sana
na kuzunguka zunguka takribani kila mahali kutafuta matibabu na halifanya hivyo pasipo mafanikio yeyote na
kisha kupelekwa nje ya nchi lakini nako hakupata matibabu yeyote ya kumwezesha
kupona. Baadae alikumbuka kuna dhambi aliwahi kutenda “ ya kumsema vibaya
mchungaji. Basi yule mama alirudi na kisha kumtafuta huyo mchungaji na kumwomba
msamahaaa na hazikupita siku nyingi mama hakawa mzima.
(b) MAMBO
YA KUFANYA ILI HUWEZE KUISHI MAISHA MATAKATIFU:
Ø
Maombi
Ø
Kumwamini
Mungu
Ø
Kumtii
Mungu
Ø
Kumpinga
shetani na Mambo yake yote
Ø
Kumpokea
Yesu KRISTO kuwa Bwana na mwokozi wako
Ø
Kupokea
ujazo wa Roho Mtakatifu
Ø
Kusoma
neno la Mungu
(Yakobo 4:7-8). “Basi mtiini Mungu. Mpingeni shetani, naye atawakimbia.
Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye
dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.”
(Mathayo
4:1-10). “...kisha ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha
miliki zote za ulimwengu, na fahari yake, akamwambia, hay yote
nitakupa,ukianguka kunisudujia. Ndipo Yesu akamwambia nenda zako shetani kwa
maana imeandikwa msujudie Bwana Mungu wako, umwabudi yeye peke yake.”
·
Mahali
pengine Bible inasema “Kama watoto wa
kutiimsijifananishe na tamaa zenu za kwanza, za ujinga wenu bali kama yeye
aliyewaita alivyomtakatifu, nanyi iweni watakatifu katika mwendendo wenu wote.
( 1petro 1:14-16)
Yako mambo mengi
ambayo kwa namna moja ama nyingine yanaweza kukusaidia kuishi maisha matakatifu
katika KRISTO:
ü
Epuka
mazingizara ambayo yatakupelekea kutenda dhambi “Biblia yangu inaniambia katika
Mithali 1;10 “Mwanangu wenye dhambi
wakikushawishi wewe usikubali”
ü
Kuwa
mtu mwenye msimamo na imani ulio nayo usiruhusu dhambi ikutawale.
ü
Kuwa
mtu mwenye bidiii katika kuhudhuria semina, mbalimbali za neno la Mungu,
mafundisho, nyumba za ibada ( kanisani) hii itakusaidia.
*********** UBARIKIWE******
@Imeandaliwa na
Ev, Mwl Linus Siwiti
0766466209/0652303709
Email:
linussiwiti12@gmail.com
Comments
Post a Comment