UJENGE MSINGI WAKO WA IMANI KATIKA YESU NA SI KATIKA DINI


Bwana yesu asifiwe mpendwa, nakusalimu katika jina la Yesu aliye Bwana na mwokozi wa maisha yetu.

Karibu katika makala yetu hii ya AMKA UKUE KIROHO ambapo leo tutakwenda kuangalia jinsi ya kuijenga imani yako katika kristo na si katika dini. Namshukuru Mungu kwa ajili yako maana ni kwa neema tu hata upate nafasi hii ya kusoma somo hili ambalo lina leta utukufu kwa Mungu. Hivyo andaa moyo wako kwa ajili ya kupokea kile ambacho Roho Mtakatifu atakusemesha ndani yako katika kukuvusha katika somo hili.

Katika maisha ya yetu hapa Duniani, tumezaliwa ili kulitimiza kusudi la maisha yetu ambayo yanatengenezwa na mwokozi wetu Yesu kristo.

Leo hii maeneo mengi ya Dunia kumekuwa na dini tofauti tofauti, lakini mimi katika somo hili fupi, sitaki kujikita sana katika dini au madhebu ya wengine bali natajikita katika dini au dhehebu lililo Takatifu linalo mwabudu Mungu aliye hai, kupitia Yesu krito aliye tukomboa kwa Damu yake mwenyewe.

Katika maisha ya wokovu ya hapa duniani, tunakutana sana na changamoto mbalimbali za kihuduma na kiimani. Ambapo kupitia changamoto hizo wapo watu wanao fanikiwa kuzishinda na wengine kusindwa. Mojawapo ya changamoto hizo ni Dini na sheria za Dini , ni ukweli usiopingika ya kwamba dini nyingi  na madhehebu ni mengi yanayo hubiri injili ya Kristo na kuwasaidia watu kumjua yeye, lakini miongoni mwa dini hizo kumekuwako na mkazo wa mafundisho ya watu kuihofia na kuigogopa dini waliyo nayo kuliko kumwogopa Mungu. Maranyingi watu hao wako tayari kutenda dhambi zozote wanazoweza kutenda huku wakiogopa Dhehebu lao au kanisa lao kuliko kumwogopa Mungu. Watu wengi misingi ya maisha yao ya kiroho imejengwa juu ya  dini na dhehebu na sio juu ya YESU KRISTO 

Aliyejengwa juu ya  dini huiona dini ni ya thamani kuliko YESU KRISTO Mwokozi. Kumbuka Dini yaweza kufa au kupotea lakini Yesu yeye habadiliki milele hata milele, unatakiwa msingi wako uujenge katka Kristo na si katika dini au dhehebu.

Mtu aliyejengwa juu ya dhehebu huliona dhehebu lake ni thamani kuliko hata Wokovu.
Mtu aliyejengwa juu ya dini  anaweza akamuona Mchungaji/Askofu wake au Mwanzilishi wa dhehebu lake ni wa muhimu kuliko hata Biblia.
Waliojengwa msingi wao wa kiroho katika dini au dhehebu  Huwaogopa wanadamu kuliko MUNGU. Anaweza akafanya dhambi huku akijificha  Mchungaji au kiongozi wake asimuone. Mtu huyo hamwogopi MUNGU Bali hujaribu kujificha kwa wana Kanisa, huyo hajui kama MUNGU alishamuona kabla ya wote kumuona.
Ndugu zangu, ni muhimu kujua kwamba Bwana YESU hakuleta dini ila alileta Wokovu.
Bwana YESU alileta mfumo wa maisha matakatifu yanayompendeza MUNGU ili tuwe tayari kwa ajili ya uzima wa milele
Matendo  4:12 "Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo."
Usipoishi maisha matakatifu ya Wokovu wa KRISTO, hata kama unazingatia sheria za dini na dhehebu hutaweza kuingia uzima wa milele.
Dini na dhehebu vinaweza kujaa misimamo na misimamo mingine ni kinyume na Neno la MUNGU kwa wakati huu.
Dhehebu linaweza kukupa sheria na kujifunza tu kwa mwanzilishi wa dhehebu na kumnyenyekea sana na kumtii sana hata ukawa kama mwabudu sanamu tu.
Dhehebu linaweza kuleta msimamo lakini Wokovu unaekekeza utakatifu katika KRISTO na kisha uzima wa milele.
1 Petro 1:14-15" Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu; bali kama yeye(YESU) aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;"
Kama dhehebu halifundishi kweli ya KRISTO   ni heri kutafuta na kujiunga Kanisa ambalo lina hubiri Wokovu na utakatifu bila woga.
Kumbuka ukifanya yaliyo ya KRISTO wewe uko ndani ya KRISTO.
Ukifanya yanayomchukiza KRISTO wewe uko nje ya KRISTO.
Ukimkosa YESU KRISTO umekosa vyote.
Dhehebu na dini usiviweke sana rohoni hata ukamsahau Bwana YESU.
Kuna watu wakristo wakisikia mtu anaisema vibaya Biblia na yeye anaweza kuwasapoti lakini akisikia mtu anakosoa kitu kidogo kuhusu dhehebu lake anaweza hata akachukua jiwe kumpiga aliyekosoa dhehebu.
Kwa haraka haraka unagundua Kabisa kwamba moyo wa huyo ndugu umejengwa juu ya dhehebu na sio juu ya Neno la MUNGU.
Ni tafakari fupi.
Ubarikiwe sana.

Mpedwa wokovu wa kweli ni katika kristo na si katika madhebu, kumbuka ya kwamba madhehebu yaweza kuwa na mapungufu lakini Yesu wetu hana mapungufu, ukimfuata yeye utapata uzima wa milile. Kumbuka yeye ndiye Mungu wetu, aliye tukumboa kwa Damu yake mwenyewe.
Hakuna upendo mkuu na wa kujitoa kama huu alio ufanya Yesu kristo, ukimfua yeye atakulinda na kukuponya maradhi yako yote, ukimfuata yeye utaishi vizuri hapa Duniani na Mbinguni utaenda.
Kumbuka nyakati hizi tulizo nazo za sasa ni za kuweka bidii kumtafuta Mungu maana ni nyakati za Mwisho.
Ni Yesu pekee ndiye awezae kukuokoa na kukufanya uiepuke kuzimu aliyo andaliwa kwa moto mkali kwa ajili ya Shetani na wafuasi wake.
Kumbuka Mungu hakuiandaa kuzimu kwa ajili yako bali kwa ajili ya shetani na wafuasi wake. Nakushauri umfuate Yesu ili upate uzima wa milele ambao utakuwa faida kwako.
Kama uko tayari kumpokea Yesu ambatana nami katika maombi haya, Omba kwa imani na kumaanisha na Yesu Kristo atakuponya na kukupokea.

Kama uko tayari kumurudia Mungu  tamka maneno haya yafuatayo kwa kumaanisha. Sema "Eeh Bwana Mungu, ninakuja mbele yeko, mimi ni mwenye dhambi, nimekutenda dhambi kupitia matendo yangu,  kusema kwangu, kuwaza kwangu na kwa dhambi zakujua na za kutokujua, Eeh Bwana Yesu ninaomba unisamehe, nisafishe kwa Damu yako ya thamani, nifute kuwenye kitabu cha hukumu na uniandike kwenye kitabua cha Uzima wa milele, Eeh Bwana Yesu nakuja mbele zako kuanzia siku ya leo nifinyange moyo wangu, nafsi yangu na roho yangu kama upendavyo wewe, Amina. mpendwa kama umesali sala hii fupi kwa kumaanisha tayari umeupokea wokovu, unatakiwa utafute kanisa lililo karibu yako lenye kumuabudu Mungu wa kweli na uungane nao kwa ajili ya kukua kiroho. vile nakuomba ujitahidi kuepuka maisha ya Dhambi, maana ni dhambi pekee ndiyo itakayo kutenga na uso wa Mungu.Nakutakia maisha mema ya wokovu,Wako mpendwa katika KristoDaniel Mbugu.Kwa mwendelezo wa mafundisho zaidi ya neno la Mungu tembelea  AMKA UKUE KIRIHO. www.amkaukuekiroho1.blogspot. Na kwa ushauri kuhusiana na maisha ya wokovu tuma ujumbe katika email yangu. www.mbugudaniel@gmail.com. Au wasiliana nami kwa kutuma ujumbe kwenda  kwajia ya sms au whatsApp kwa 0758505174/0655505173. Mungu akubariki.

Comments

Popular Posts