YESU KRISTO NI MSINGI WA UZIMA WA MILELE


Bwana yesu asifiwe mpendwa, nakusalimu katika jina la Yesu aliye Bwana na mwokozi wa maisha yetu.

Karibu katika makala yetu hii ya AMKA UKUE KIROHO ambapo leo tutakwenda kuangalia msingi wetu wa kuurithi uzima wa milele. Namshukuru Mungu kwa ajili yako maana ni kwa neema tu hata upate nafasi hii ya kusoma somo hili ambalo lina leta utukufu kwa Mungu. Hivyo andaa moyo wako kwa ajili ya kupokea kile ambacho Roho Mtakatifu atakusemesha ndani yako katika kukuvusha katika somo hili.

Yesu kristo ni kiunganishi kati ya sisi wanadamu na MUNGU Muumba wetu.Pasipo  Yesu hakuna uzima wa milele, kwa hiyo ili ufike mbinguni ni lazima umtazame Yesu kama njia ya kukufikisha kwa Mungu.

Maisha ya Duniani ni mafupi sana yaliyo jaa taabu na shida za kila namna, kwahiyo ndani ya hizo shida za Duniani ni Mhimu kumtazama Yesu kuwa daraja lako la kukuvusha kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Kumbuka kuwa yeye ndiye aliye kufa msalabani kwa ajili yetu, hivyo tunapo utafuta uso wake na yeye anatuonyesha upendo wake waziwazi. Nandio maana katika Yohana 14;6 anasema "...mimi ndimi njia ya kweli na uzima; Mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi" .  Kwa hiyo kama unataka kuingia mbinguni unacho takiwa ni kuitafuta njia itakayo kufikisha mbinguni, na hakuna njia nyingine ya n kukufikisha Mbinguni zaidi ya Yesu kristo.Na ndio maana katika yohana hapo juu anatumbia ya kwamba yeye ndio njia yan kweli na uzima.

Ukitaka uhusike na Mungu basi husika na Yesu kristo.

Ukitaka uhusike na uzima wa milele aliouandaa MUNGU basi husika na Wokovu wa YESU KRISTO.
1 Yohana 5:11-12 " Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba MUNGU alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe. Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa MUNGU hana huo uzima".

Kama ni dini tu na madhehebu vilikuwepo tangu  zamani sana lakini viliwafanya wanadamu wasiwe waenda mbinguni.
Mfano hai ni dhehebu la mafalisayo au dhehebu la masadukayo. Hawa walikuwa ni dini na dhehebu zenye mafundisho ya kiroho lakini hazikuwa katika kweli ndio maana MUNGU alimleta YESU KRISTO ili kwa mara moja ya milele watu wanaotaka kwenda uzima wa milele basi wamfuate YESU KRISTO na injili yake.
Yuda 1:3 "Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu".

Waenda uzima wa milele tulikabidhiwa imani ya uzima Mara moja tu kwa YESU KRISTO kufa msalabani ili kutuokoa. Dini za kabla ya hapo na baada ya hapo zilizo kinyume na Bwana YESU hayo ni mapando ya shetani ili kuwapeleka watu jehanamu.
Ndugu unamhitaji YESU KRISTO kuliko unavyohitaji kitu kingine chochote.
Unamhitaji YESU kuliko hata dini na dhehebu.
YESU hakuja kuleta dini(Maana zilikuwepo) Bali habari njema za Ufalme wa MUNGU ili mwanadamu kwa kupitia YESU KRISTO aungane na MUNGU na aungane na ahadi za MUNGU, ahadi juu zaidi ni ya uzima wa milele.
Ndugu nakuomba uelewe kwamba ukiamua kuhusika na YESU KRISTO ndio umechagua kuhusika na MUNGU aliyeziumba mbingu na Dunia.
Kumpokea YESU KRISTO na kumtii kama Mwokozi ndio kumpendeza MUNGU.

YESU alikuja kwa faida yako Mwanadamu.
Mpokee kama Mwokozi wako ili uhusike na uzima wa milele.
Yohana 3:16-18 " Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU."

Mpendwa katika Kristo ninakukaribisha katika maisha ya wokovu, maisha ambayo watu tunaishi kwa uaminifu na kwa Furaha, kumbuka hakuna njia nyingine itakayo weza kukusaidia ili uuone Ufalme wa Mbingu, isipom kuwa Toba. Nitoba tu ndiyo itakayo kupa kibali cha wewe kuokoka, nakushauri mfuate huyu Yesu ili ayabadilishe maisha yako, akufanye kama apendavyo yeye.

Kwa Yesu ndio kuna uzima, kwa wewe unaye hitaji kumpatia Yesu maisha yako omba pamoja nami maombi haya, omba kwa imani na kwa kumaanisha ndani ya moyo wako, na Mungu atakusamehe na kukupokea katika wana wa pendo lake.  

 Sema "Eeh Bwana Mungu, ninakuja mbele yeko, mimi ni mwenye dhambi, nimekutenda dhambi kupitia matendo yangu,  kusema kwangu, kuwaza kwangu na kwa dhambi zakujua na za kutokujua, Eeh Bwana Yesu ninaomba unisamehe, nisafishe kwa Damu yako ya thamani, nifute jina langu kuwenye kitabu cha hukumu na uniandike kwenye kitabua cha Uzima wa milele, Eeh Bwana Yesu nakuja mbele zako kuanzia siku ya leo nifinyange moyo wangu, nafsi yangu na roho yangu kama upendavyo wewe, Amina. mpendwa kama umesali sala hii fupi kwa kumaanisha tayari umeupokea wokovu, unatakiwa utafute kanisa lililo karibu yako lenye kumuabudu Mungu wa kweli na uungane nao kwa ajili ya kukua kiroho. vile nakuomba ujitahidi kuepuka maisha ya Dhambi, maana ni dhambi pekee ndiyo itakayo kutenga na uso wa Mungu.Nakutakia maisha mema ya wokovu,Wako mpendwa katika KristoDaniel Mbugu.Kwa mwendelezo wa mafundisho zaidi ya neno la Mungu tembelea  AMKA UKUE KIRIHOwww.amkaukuekiroho1.blogspot. Na kwa ushauri kuhusiana na maisha ya wokovu tuma ujumbe katika email yangu. www.mbugudaniel@gmail.com. Au wasiliana nami kwa kutuma ujumbe kwenda  kwajia ya sms au whatsApp kwa 0758505174/0655505173. Mungu akubariki.

Comments

Popular Posts