ASILI YA MWANADAMU KIBIBLIA (Biblical Anthropology) 1
Bwana yesu asifiwe, nakusalimu katika jina la Yesu aliye Bwana na
mwokozi wa maisha yetu.
Karibu katika makala yetu hii ya AMKA UKUE KIROHO ambapo leo Tutakwenda
kuanza somo mbalo si wengi wanalifahamu sana, Linalo itwa "ASILI YA
MWANADUMU KIBLIA", katika somo hili utajifunza vitu vingi sana kuhusiana
na asili na uumbaji wa Mungu, hivyo nakushauli uwe na daftali kwa ajili ya kuandika
kile ambacho Mungu atakusemesha kupitia somo hili, lakini pia mjulishe na
umpatie mwenzako unaye ona kuwa atanufaika na mafundisho hayo. Na Mungu wangu
aliye hai na akubariki.
Somo letu hili ambalo
linahusu asili ya mwanadamu kulingana na neno la Mungu ambalo ndilo chanzo cha
yote na ndilo mwisho wa yote katika maisha yetu, bila kujali kama sisi
tunalikubali au laa.
Ni somo muhimu sana kwa sababu linatupa maana halisi ya mwanadamu kwa sababu
tulivyofundishwa kule shuleni tuliambiwa kwamba mwanadamu alitokana na sokwe,
na wanasayansi huwa wanamtaja mwanadamu kuwa kwenye ufalme/jamii ya wanyama
(Animal kingdom).Lakini si kweli kwamba sisi ni ufalme mmoja na wanyama, hatupo
kabisa kwenye viwango vyao kwa sababu sisi ni viumbe wa kipekee ambao tumeumbwa
kuusimamia uumbaji mwingine wote wa Mungu.
Ndiyo maana wanadamu
wengi duniani tangu zamani kwa kutokujua asili yao na utambulisho wao, wamekuwa
wakiishi kama wanyama na kwa sasa mnashuhudia wenyewe maadili yalivyoharibika
kila sehemu na watu wanaishi kama wanyama kabisa.
Hili ni somo muhimu sana ambalo siyo mimi na wewe tu uliyeokoka tunapaswa
kujua haya, bali hata wengine wasiyookoka kwa sababu wakijua haya watarudi kwa
Yesu haraka mno kulingana na tofauti kubwa iliyopo kati ya uongo wa wanadamu
kuhusu mwanadamu dhidi ya kweli ya Mungu kuhusu mwanadamu.
Kila mwanadamu
anayejitambua na anayetaka kwenda mbali zaidi na kuishi maisha ya faida hapa duniani
lazima ajiulize maswali yafuatayo;
1. Mimi ni
nani? (utambulisho wangu)
2.
Nimetoka wapi? (chanzo changu ni nini?)
3. Kwa
nini nilizaliwa hapa duniani? (Kusudi la maisha yangu)
4.
Ninaweza kufanya nini? (kipawa/kipaji/karama/uwezo)
5.
Ninaelekea wapi? (hatma yangu ni nini)
Ukiweza kupata majibu ya
haya maswali vizuri hapo utaweza kuishi maisha ya faida na yenye maana zaidi
duniani, na hata ukifa bado alama yako itaachwa na utabaki unakumbukwa vizazi
na vizazi.
katika somo hili tutakwenda
kuyajibu haya maswali yote matano, na naamini Mungu anakwenda kukupa ngazi
nyingine ya maisha baada ya hili somo letu.
TUANZE KUYAJIBU,
“Mungu akasema, Na
tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na
ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa
kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa
Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba” MWANZO 1:26
Ukiangalia Mungu
alivyomuumba mwanadamu utashangaa namna ilivyo tofauti na viumbe wengine kwa
sababu ya uthamani Mungu aliyouweka kwa mwanadamu.
Mungu alipokuwa akiumba vitu vingine vyote alikuwa akitamka tu vikatokea;
kwanza aliumba mbingu na nchi na maji kisha akaanza kuongea na maji akisema
itoe viumbe vyote vya majini, kisha akaiambia ardhi itoe mimea na wanyama
wanaotembea juu ya nchi.
Alipofika kumuumba
mwanadamu hakusemesha kitu kingine chochote bali alijisemesha mwenyewe
akisema, “na tumfanye mtu kwa sura na mfano wetu” kumbe sisi
wanadamu ni tofauti kabisa na viumbe wengine na tena asili yetu inatoka kwa
Mungu kabisa.
ANAPOSEMA KWA SURA NA MFANO WAKE;
Kwa sura ya Mungu
anamaanisha vitu vitatu muhimu sana;
1.
Asili ya Mungu –
maana yake sisi ni roho kama Mungu naye alivyo Roho tena yenye uzima ndani yake
na Kamwe hamna mauti ndani yake.
2.
Tabia ya Mungu –
kile anachokipenda Mungu nasi tukipende, kile anachokifukia na sisi tukichukie
3.
Maadili ya Mungu –
uwezo wa kuyajua mema na yatupasayo na kuyaishi hayo
Lakini pia Mungu akasema
tumuumbe mwanadamu Kwa mfano wake maana yake niKufikiri kama anavyofikiri,
kutenda kama yeye (to behave like him)
Mfano, unapoona hali ni
giza mahali Fulani huwa unatamka nuru au unaatamkaa tena giza, Mungu yeye
alitamka nuru alipoona giza. Lazima na sisi tutende kama yeye.
UHARIBIFU ULIYOTOKEA KWA MWANADAMU.
Kama tulivyoona
utambulisho na asili ya mwanadamu kwamba imetokana na Mungu kwa sababu ameumbwa
kwa sura na mfano wa Mungu.
Lazima tujiulize kwamba
ni kitu gani kilichotokea hata mwanadamu akapoteza tabia ya Mungu na maadili ya
Mungu hata asili Mungu?
Uharibifu huu ulitokea
bustani ya Edeni pale Adamu na Eva waliposhindwa kulishika neno la Mungu na
kulitii badala yake wakamsikiliza Shetani wakadharau maagizo ya Mungu.
Hapo ndipo mwanadamu alianza kupoteza asili ya Mungu, tabia na ,madili ya
Mungu moja kwa moja kwenye maisha yake, akaanza kufanya mambo ambayo
yanamwangamiza mwenyewe tena akaleta kila aina ya uharibu kwa dunia nzima.
Baada ya haya ndipo mwanadamu akapoteza kabisa hadhi na ile nafasi aliyokuwa
nayo mbele za Mungu, akafukuzwa bustanini kabisa.
“kwa hiyo Bwana
Mungu akamtoa katika bustani ya Edeni, ailime ardhi ambayo katika hiyo
alitwaliwa” Mwanzo 3:23
Ni muhimu sana kujua
tulichopoteza bustani ya Edeni ndipo utaelewa kilichomleta Yesu kwa sababu Yesu
alikuja kurejesha kile Adamu alichokipoteza bustanini na kumfanya afukuzwe.
Nataka kabla
hatujaenda mbele zaidi nikurudishe nyuma kidogo tuweze kuangalia tena namna
mwanadamu alivyoumbwa; Hii ni muhimu sana kwasabu hili somo lina husu asili ya
mwanadamu
Kama ujuavyo mwanadamu ni roho anayo nafsi lakini anaishi kwenye kasha
linaloitwa mwili.
Kwa hiyo mwanadamu anao
UTU WA NJE ambao ndiyo mwili na UTU WA NDANI ambao ni roho yake pamoja na nafsi
yake.
Ukisoma biblia yako kwa makini utashangaa kwamba Mwanzo sura ya kwanza
unamuona Mungu akiongea kuhusu mpango wake wa kumuumba mwanadamu lakini pia
Biblia ikaeleza kwamba alifanikiwa kuwaumba mwanamume na mwanamke, kwenye hiyo
hiyo sura ya kwanza.
MWANZO 1:27 “Mungu
akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke
aliwaumba”
Katika sura ya pili utaona Mungu akimfinyanga mwandamu kutoka kwenye
mavumbi ya ardhi na kumpuizia puani pumzi ya uhai mtu akawa nafsi hai.
MWANZO 2:7 “Bwana
Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu
akawa nafsi hai”
MAANA YAKE NI NINI?
Kumbe Mungu katika
sura ya kwanza tunaona akimuumba mwanadamu UTU WA NDANI na baadaye katika
sura ya pili akaumba UTU WA NJE wa mwanadamu.
Ile baada tu ya kumfinyanga kutoka kwenye mavumbi ya ardhi akampulizia
puani pumzi ambayo ndiyo roho yenyewe ambayo ndiye mwanadamu halisi.
Kwa hiyo kumbe mwanadamu
siyo mwili wake ambao unaonekana tu kwa nje, mwanadamu mwenyewe yupo ndani
ambaye ni roho.
Sasa Mungu akampa mwanadamu nafsi ili aweze kutafsiri mambo ya kimwili
kupeleka rohoni na kuyatafsiri mambo ya mwilini kwenye rohoni.
Mwili umeundwa na vitu
vikubwa vitatu ambavyo ni damu, nyama na mifupa.
Nafsi imebeba
mambo makubwa matatu ambayo ni ufahamu, hisia na maamuzi.
Lakini kwenye roho yako imebeba vitu vitatu vya muhimu ambavyo ni
dhamiri, ibada na utambuzi, Mungu akitupa neema tutavisoma kwa undani mbeleni.
Sasa naamini unaweza
ukaelewa wewe ni nani hasa au umetokea wapi kiasili kabisa; kama umenifuatilia
kwa makini utagundua kuwa wewe ni ile PUMZI YA MUNGU ILIYOTOKA NDANI YA MUNGU.
Kwa tafsiri nyingine ni kwamba wewe umeshiriki sehemu ya uhai ya Mungu
ndiyo ikakufanya wewe kuwa mwanadamu.
Mtu mmoja aliwahi
kusema hivi; “Siku kuu mbili za maisha yako, ya kwanza ni siku ile
siku ulipozaliwa na ya pili ni siku utakapojua kwanini ulizaliwa”
Hapo ndipo unaanza mchakato wa kujitambua wewe ni nani baada ya Yesu
kukurudisha bustanini, na baada ya kujitambua (kujua kusudi lako) lazima ujue
namna ya kuyaongeza thamani.
Kusudi kamili la maisha ya mtu kwakweli linanzia pale anapookoka, maana ndipo tunasema
amerudishwa kwenye asili yake ya zamani kama tulivyoona kwenye kipindi
kilichopita kwamba mwanadamu baada ya kukosea alipoteza nafasi yake.
Ile nafasi ndiyo kusudi la maisha ya mtu, na namna pekee ya kuipata ni
kwa kuokoka (kumpa Yesu maisha yako) kisha ndipo inapofuatiwa na michakato
mingine.
2WAKORITHO 5:17 “Hata
imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita
tazama! Yamekuwa mapya”
WAEFESO 1:11-13 “na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa
tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri
la mapenzi yake. Nasi katika huyo tupate kuwa sifa ya utukufu wake, sisi
tuliotangulia kumwekea Kristo tumaini letu. Nanyi pia katika huyo
mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha
kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu”
MAISHA YA KUSUDI NDIYO MAISHA YENYE THAMANI DUNIANI.
Maswali ya msingi kujiuliza,
- Je, Unadhani maisha unayoishi sasa yana thamani kwa
watu (jamii yako na dunia kwa ujumla) kwa kiasi gani?
- Je, unadhani maisha yako kwa miaka yako uliyonayo sasa,
kwa Mungu yana thamani kiasi gani?
- Je, Unadhani una umuhimu wa kuendelea kuishi duniani
kwa sababu gani?
- Je, Mungu na wanadamu wenzako, wanafurahia kuendelea
kuishi kwako au upo tu kusukuma siku?
Anza kutafakari mwenyewe tu kama una faida na thamani kiasi gani kwa muda wote
uliyoishi na unakoelekea sasa, maisha yako siyo ya kawaida tu kama unavyoweza
ukafikiri, wala uwepo wako duniani siyo wa kawaida tu kama unavyoweza kufikiri.
KWA NINI NILIZALIWA?
Nataka nikwambie tu
kwamba, kwa taarifa yako fupi; dunia inatambua uwepo wako na inasubiri kwa hamu
uifikishie kile ulichokileta kwao. Cha Kushangaza nakuona bado hutaki kukaa
chini na kujiuliza maswali kama hayo hapo juu.
Kama huamini kwamba dunia inakutambua, we tafuta mtu kama wewe hapa
duniani, na isitoshe jaribu kufanya utafiti kama kuna mtu alishawahi kuishi
aliye kama wewe hapa duniani.
Nataka nikwambie hakuna na hatakuweko; maana yake wewe unautofauti
kuanzia nje mpaka ndani, huko ndani kuna hazina ulizokuja nazo ili kutuletea na
bado tunazisubiri kuzipata kutoka kwako.
Nilipoanza kujiuliza kwanini mimi mwanadamu nilizaliwa, niligundua
nilizaliwa kwa ajili hii;-
HAYA HUWA NAYAITA KUSUDI LA MUNGU NGAZI YA KWANZA AMBAYO HII NI KWA KILA
MWANADAMU….
1.
Ili nishirikiane
na Mungu kuendeleza uumbaji wake kwa kutunza, kusimamia, kuzalisha na kutawala
dunia kwa ujumla…
MWANZO 1:26 “Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu;
wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote
pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi”
2.
Ili niwe furaha ya
Mungu (mimi ni utukufu wa Mungu, ukitaka kumjua Mungu niangalie mimi), Kwa
maneno mengine niliumbwa ili kuonyesha asili ya Mungu, tabia ya Mungu na
maadili ya Mungu hapa duniani.
ISAYA 43:21 “watu wale niliojiumbia nafsi yangu, ili wazitangaze sifa zangu”
3.
Ili niwe baraka kwa
wanadamu wengine (nimeumbwa kuja kufikisha zawadi na hazina alizoweka Mungu
ndani yangu kwa ajili ya wanadamu wenzangu),
4.
Ili niishi milele
(hakika mimi ni roho, nina nafsi na niko kwenye mwili ila mwili huu ni wa Muda
tu)
MHUBIRI 12:11 “Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake; TENA AMEIWEKA
HIYO MILELE NDANI YA MIOYO YAO; ila kwa jinsi mwanadamu asivyoweza kuivumbua
kazi ya Mungu anayoifanya, tangu mwanzo hata mwisho”
Hizo ni baadhi ya
sababu za kila mwanadamu kuumbwa na kuishi kwa majira haya tuliyonayo.
Nilipoanza kugundua hizo sababu hapo juu ya kwa nini nizaliwe, maisha
yangu yalibadilika kabisa kwa sababu nilijiona nina thamani kuliko ambavyo watu
wanafikiri.
Nataka nikwambie hata kama wewe unafikiri huna uthamani fulani, mi
nashawishika kukwambia Mungu yeye anakuona una uthamani kuliko wewe mwenyewe
unavyojiona. Lazima uanze kubadilisha fikra zako kwa namna hiyo…
Somo hili litakuwa na mwendelezo katika sehemu ya pili, hivyo endelea
kufatilia zaidi ili unufaike na mafundisho ya neno la uzima.
Mpendwa maisha matakatifu ni ya muhimu sana, na ndiyo yanayomfanya mtu adumu
kuwa na mahusiano na Mungu kwa ukamilifu wote, na hakuna njia nyingine ya
kuishi maisha matakatifu isipo uwa umeokoka.
Kama bado hauja okoka sali sala hii fupi kwa imani, na utakuwa umekoka na
kumpokea Roho Mtakatifu huku ukitembea kwa kuishi maisha matakatifu;-
Sema "Eeh Bwana
Yesu, ninakuja mbele yeko, mimi ni mwenye dhambi, nimekutenda dhambi kupitia
matendo yangu, kusema kwangu, kuwaza kwangu na kwa dhambi za kujua na za
kutokujua, Eeh Bwana Yesu ninaomba unisamehe, nisafishe kwa Damu yako ya thamani,
nifute jina langu kwenye kitabu cha hukumu na uniandike jina langu kwenye
kitabua cha Uzima wa milele, Eeh Bwana Yesu nakuja mbele zako kuanzia siku ya
leo nifinyange moyo wangu, nafsi yangu na roho yangu kama upendavyo wewe,
maisha yangu yote nakukabidhi wewe uyaongoze kwa Roho wako Mtakatifu, naomba na
kuamini kupitia Jina la Yesu kristo aliye Bwana na mwokozi wa maisha yangu.
Amina.
Mpendwa kama umesali
sala hii fupi kwa kumaanisha tayari umeupokea wokovu, unatakiwa utafute kanisa
lililo karibu yako lenye kumuabudu Mungu wa kweli na uungane nao kwa ajili ya
kukua kiroho.
Kama umeguswa chochote
kupitia makala hii , naomba uandika ujumbe wako hapo chini na nitakapo soma
nitafurahia sana.
Na kama utahitaji maombi na ushauri wowote wa kiroho, wasiliana nami kupitia
namba na emeil yangu kwa njia ya sms. mwishoni nitatoa namba na
email, lakini kama umeokoka kupitia makala hii waweza kunitumia
ujumbe kwa njia ya simu , kwa watsapp, au kwa kawaida , au kupitia email yangu
nitakayo itoa hapo chini.
Somo hili limeandaliwa na Noeli Pallangyo, na kuandikwa na
mwandishi Daniel J Mbugu wa makala ya AMKA
UKUE KIRIHO.
Karibu katika sehemu ya
pili ambayo itawekwa kupitia blogu hii. Mungu akubariki sana.
Wako mpendwa katika
Kristo,
Daniel Mbugu.
Kwa mwendelezo wa
mafundisho zaidi ya neno la Mungu tembelea AMKA
UKUE KIRIHO. www.amkaukuekiroho1.blogspot. Na
kwa ushauri kuhusiana na maisha ya wokovu tuma ujumbe katika email
yangu. www.mbugudaniel@gmail.com. Au wasiliana nami
kwa kutuma ujumbe kwa njia ya sms au whatsApp kwa 0758505174/ 0655505173. Somo
hili litaendelea katika sehemu ya 2.
Ni somo muhimu sana kwa sababu linatupa maana halisi ya mwanadamu kwa sababu tulivyofundishwa kule shuleni tuliambiwa kwamba mwanadamu alitokana na sokwe, na wanasayansi huwa wanamtaja mwanadamu kuwa kwenye ufalme/jamii ya wanyama (Animal kingdom).Lakini si kweli kwamba sisi ni ufalme mmoja na wanyama, hatupo kabisa kwenye viwango vyao kwa sababu sisi ni viumbe wa kipekee ambao tumeumbwa kuusimamia uumbaji mwingine wote wa Mungu.
Hili ni somo muhimu sana ambalo siyo mimi na wewe tu uliyeokoka tunapaswa kujua haya, bali hata wengine wasiyookoka kwa sababu wakijua haya watarudi kwa Yesu haraka mno kulingana na tofauti kubwa iliyopo kati ya uongo wa wanadamu kuhusu mwanadamu dhidi ya kweli ya Mungu kuhusu mwanadamu.
TUANZE KUYAJIBU,
Mungu alipokuwa akiumba vitu vingine vyote alikuwa akitamka tu vikatokea; kwanza aliumba mbingu na nchi na maji kisha akaanza kuongea na maji akisema itoe viumbe vyote vya majini, kisha akaiambia ardhi itoe mimea na wanyama wanaotembea juu ya nchi.
ANAPOSEMA KWA SURA NA MFANO WAKE;
UHARIBIFU ULIYOTOKEA KWA MWANADAMU.
Hapo ndipo mwanadamu alianza kupoteza asili ya Mungu, tabia na ,madili ya Mungu moja kwa moja kwenye maisha yake, akaanza kufanya mambo ambayo yanamwangamiza mwenyewe tena akaleta kila aina ya uharibu kwa dunia nzima.
Baada ya haya ndipo mwanadamu akapoteza kabisa hadhi na ile nafasi aliyokuwa nayo mbele za Mungu, akafukuzwa bustanini kabisa.
Kama ujuavyo mwanadamu ni roho anayo nafsi lakini anaishi kwenye kasha linaloitwa mwili.
Ukisoma biblia yako kwa makini utashangaa kwamba Mwanzo sura ya kwanza unamuona Mungu akiongea kuhusu mpango wake wa kumuumba mwanadamu lakini pia Biblia ikaeleza kwamba alifanikiwa kuwaumba mwanamume na mwanamke, kwenye hiyo hiyo sura ya kwanza.
Katika sura ya pili utaona Mungu akimfinyanga mwandamu kutoka kwenye mavumbi ya ardhi na kumpuizia puani pumzi ya uhai mtu akawa nafsi hai.
MAANA YAKE NI NINI?
Ile baada tu ya kumfinyanga kutoka kwenye mavumbi ya ardhi akampulizia puani pumzi ambayo ndiyo roho yenyewe ambayo ndiye mwanadamu halisi.
Sasa Mungu akampa mwanadamu nafsi ili aweze kutafsiri mambo ya kimwili kupeleka rohoni na kuyatafsiri mambo ya mwilini kwenye rohoni.
Lakini kwenye roho yako imebeba vitu vitatu vya muhimu ambavyo ni dhamiri, ibada na utambuzi, Mungu akitupa neema tutavisoma kwa undani mbeleni.
Kwa tafsiri nyingine ni kwamba wewe umeshiriki sehemu ya uhai ya Mungu ndiyo ikakufanya wewe kuwa mwanadamu.
Hapo ndipo unaanza mchakato wa kujitambua wewe ni nani baada ya Yesu kukurudisha bustanini, na baada ya kujitambua (kujua kusudi lako) lazima ujue namna ya kuyaongeza thamani.
Kusudi kamili la maisha ya mtu kwakweli linanzia pale anapookoka, maana ndipo tunasema amerudishwa kwenye asili yake ya zamani kama tulivyoona kwenye kipindi kilichopita kwamba mwanadamu baada ya kukosea alipoteza nafasi yake.
Ile nafasi ndiyo kusudi la maisha ya mtu, na namna pekee ya kuipata ni kwa kuokoka (kumpa Yesu maisha yako) kisha ndipo inapofuatiwa na michakato mingine.
WAEFESO 1:11-13 “na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake. Nasi katika huyo tupate kuwa sifa ya utukufu wake, sisi tuliotangulia kumwekea Kristo tumaini letu. Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu”
MAISHA YA KUSUDI NDIYO MAISHA YENYE THAMANI DUNIANI.
Maswali ya msingi kujiuliza,
Anza kutafakari mwenyewe tu kama una faida na thamani kiasi gani kwa muda wote uliyoishi na unakoelekea sasa, maisha yako siyo ya kawaida tu kama unavyoweza ukafikiri, wala uwepo wako duniani siyo wa kawaida tu kama unavyoweza kufikiri.
KWA NINI NILIZALIWA?
Kama huamini kwamba dunia inakutambua, we tafuta mtu kama wewe hapa duniani, na isitoshe jaribu kufanya utafiti kama kuna mtu alishawahi kuishi aliye kama wewe hapa duniani.
Nataka nikwambie hakuna na hatakuweko; maana yake wewe unautofauti kuanzia nje mpaka ndani, huko ndani kuna hazina ulizokuja nazo ili kutuletea na bado tunazisubiri kuzipata kutoka kwako.
Nilipoanza kujiuliza kwanini mimi mwanadamu nilizaliwa, niligundua nilizaliwa kwa ajili hii;-
HAYA HUWA NAYAITA KUSUDI LA MUNGU NGAZI YA KWANZA AMBAYO HII NI KWA KILA MWANADAMU….
MWANZO 1:26 “Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi”
ISAYA 43:21 “watu wale niliojiumbia nafsi yangu, ili wazitangaze sifa zangu”
MHUBIRI 12:11 “Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake; TENA AMEIWEKA HIYO MILELE NDANI YA MIOYO YAO; ila kwa jinsi mwanadamu asivyoweza kuivumbua kazi ya Mungu anayoifanya, tangu mwanzo hata mwisho”
Nilipoanza kugundua hizo sababu hapo juu ya kwa nini nizaliwe, maisha yangu yalibadilika kabisa kwa sababu nilijiona nina thamani kuliko ambavyo watu wanafikiri.
Nataka nikwambie hata kama wewe unafikiri huna uthamani fulani, mi nashawishika kukwambia Mungu yeye anakuona una uthamani kuliko wewe mwenyewe unavyojiona. Lazima uanze kubadilisha fikra zako kwa namna hiyo…
Somo hili litakuwa na mwendelezo katika sehemu ya pili, hivyo endelea kufatilia zaidi ili unufaike na mafundisho ya neno la uzima.
Mpendwa maisha matakatifu ni ya muhimu sana, na ndiyo yanayomfanya mtu adumu kuwa na mahusiano na Mungu kwa ukamilifu wote, na hakuna njia nyingine ya kuishi maisha matakatifu isipo uwa umeokoka.
Kama bado hauja okoka sali sala hii fupi kwa imani, na utakuwa umekoka na kumpokea Roho Mtakatifu huku ukitembea kwa kuishi maisha matakatifu;-
Na kama utahitaji maombi na ushauri wowote wa kiroho, wasiliana nami kupitia namba na emeil yangu kwa njia ya sms. mwishoni nitatoa namba na email, lakini kama umeokoka kupitia makala hii waweza kunitumia ujumbe kwa njia ya simu , kwa watsapp, au kwa kawaida , au kupitia email yangu nitakayo itoa hapo chini.
Comments
Post a Comment