IJUE MAMLAKA ILIYOMO NDANI YA MTUMISHI WA MUNGU 1
Bwana Yesu asifiwe, namshukuru Mungu kwa ajili ya kukupatia nafasi hii ya kujifunza kupitia makala hii ya AMKA UKUE KIROHO, ambapo leo tuna kwenda kujifunza juu ya mamlaka aliyo nayo mtumishi yeyote anaye mtumikia Mungu kwa uaminifu wote. Nakukaribisha sana, unatakiwa umwombe Roho Mtakatifu akufundishe na kukushirikisha vile vyote alivyo kusudia uvipate kupitia somo hili. Na mimi kama mwandishi wa makala hii ninakushauri uwe na Daftari la kuandika kile utakacho kuwa unakiona kuwa kinafaa na kitakusaidia.
Karibu tuanze somo letu hili;-
Mamlaka , ni uwezo au amri aliyonayo mtu kwa ajili ya kutenda kitu flani, na uwezo huo unakuwa na nguvu ndani yake kiasi kwamba mwenye mamlaka anaposema kitu hakuna Mtu anaye weza kupinga. Kwa mfano, kila nchi huwa na kiongozi mkuu aweza kuwa Mfalme au Rais, na viongozi hao kutokana na katiba hua na mamlaka katika nchi wanayo iongoza, na hao ndio huwa sauti ya mwisho. Hivyo katika somo hili tutakwenda kujikita zaidi katika mamlaka aliyonayo Kuani(Mtumishi wa Mungu)
LENGO LA SOMO HILI; Ni kuchochea nguvu ya maombi kwa mkristo anaye hitaji kutenda kazi na Bwana kama Kuani.
Katika Biblia tunaona watumishi mbalimbali wa Mungu wakishirikiana naye katika kufanya mambo mbalimbali ambayo yalikuwa ni makubwa sana kiasi cha kuushangaza ulimwengu, baadhi yao walimwamini sana kiasi kwamba hata walipo tishiwa na kutupwa katika tanuru la moto na katika tundu la simba hawakuogopa chochote. Kwa nini hawakuogopa, kwasababu walikuwa pamoja na Mungu na walimuamini Mungu kiasi cha kutomtenda dhambi na hatimaye wakawa washindi.
Katika maisha ya wokovu unatakiwa kuwa karibu sana na Mungu ili uweze kutembea sawasawa na mapenzi yake kwa kumzalia matunda mema ambayo yataongeza thamani yako kwake.
Tunapo soma Biblia tunaona Mungu anaweka ushirika wa karibu na Mwanadamu kaisi kwamba anaamua kuwapiga wengine kwa sababu ya mtumishi wake anaye kuwa karibu naye. Mungu amekuwa akiwatetea na kuwalinda huku akiwapigania zidi ya adui wanao watafuta. Tena amekuwa akiwahaidi ulinzi timilifu ndani ya maisha yao. Tunapo soma katika
Isaya 43;1-3 "Lakini sasa, Bwana aliye kuhuluku, Ee Yakobo, yeye aliye kuumba,Ee Israel asema hivi, usiogope, maana nimekukomboa, nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu, upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe, na katika mito haita kugharikisha, uendapo katika moto hutateketea, wala mwali wa moto hauta kuunguza, maana mimi Bwana, Mungu wako, Mtakatifu wa Israel..."
Hii ni ahadi ya ulinzi ambayo Mungu alikuwa anampatia Yakobo, yaani Israel kwa sababu Isreal ndiye Yakobo. Katika ahadi hii tunaona ana weka ahadi ya ulinzi katika nyanja zote ya kwamba hata atakapo pita katika Maji au moto hata weza kuzurika.
Swali linakuja Kwa nini Mungu amuhaidi hivi Yakobo na asiwahaidi watu wengine, maana Biblia inatuambia Dunia na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana, sasa kama ni mali ya Bwana kwanini Mungu amejikita na Yakobo katika ahadi ya ulinzi kwa Mstari huu wa Isaya 43;1-3?. Bwana Yesu asifiwe
Ukweli ni kwamba hua kuna watu maalumu ambao Mungu huwa tumia ili kuachilia Baraka kwa wengine, hata utakapo litazama taifa la Isreal katika agano la kale, utatambua ya kwamba si watu wote waliweza kusogea mbele za Mungu, bali ni wale walio wapatinishi na Makuhani ndio walio ruhusiwa kusogea mbele za Mungu na kusema kitu kwa ajili ya watu wengine.
Tunapo msoma Musa pamoja na kabila la Lawi, tuna tambua hili ya kwamba Mungu alikuwa akimtumia Musa kufikisha ujumbe wake kwa taifa la Israel, vilelive Mungu alilichagua taifa la Lawi kuwa watumishi wake katika maisha yao yote, na kutokana na hili hawakuweza kupewa urithi kwa tiafa la Israel isipokuwa walikaa Madhabahuni pa Bwana kwa ajli ya Kufanya kazi yake. Sikila Mtu aliruhusiwa kusogea Madhabahuni pa Hekaru, hapana bali ni wale tu walioitwa kwa na Bwana kama Makuhani. Nakama Mtu analizamika kuingia ndani ya Hekaru adhabu yake ilikuwa ni Moja tu ambayo ni kifo, Hivyo hata Makuhani walitakiwa kuwa watakatifu ndiyo waweze kusogea Mbele za Bwana. Bwana Yesu asifiwee..
Kumbuka si kila Mtu tu aweza kufanya hivi ya kwamba asogee mbele za Mubgu kwa ajili ya watu wengine, hapana bali ni Kuhani aliye itwa kwa jija la Bwana. Na katika agano jipya kila Mtu aliye Mpokea Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake, amefanyika kuwa kuhani kwa ajili ya wengine wote ambao hawaja okoka, na hivyo anapata wajibu wa kuomba kwa ajili yao ili Mungu atende kitu flani cha wokovu.
Tunapo soma 2Nyakati 7;12 "Ikiwa watu wangu walio itwa kwa jina langu, watajinyenyekesha na kuomba na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya, basi nitasikia Kutoka Mbinguni, na kuwasamehe dhambi zao na kuiponya nchi yao". Oooh Bwana Yesu asifiwe.., Si kila Mtu tu anauwezo wa kusogea mbele za Bwana, hapana kabisa bali ni wale tu walio itwa kwa Jina lake ndiyo wanao takiwa kunyenyekea mbele za Mungu kwa ajili ya wemgine, kumbuka katika Dunia hii wapo watu wengi lakini walio watumishi wa Mungu ni wachache sana kiasi kwamba hata wakisimama mbele ya Mungu kwa ajilia ya Tifa au kitu chochote na kuombea, Mungu huwajibu maombi yao. Na ndiyo maana leo hii kuna Wachungaji, Wainjilisti, Manabii, Maaskofu, na wewe unaye soma ujumbe huu kama umeokoka, nk. hawa wote hawapo kwa ajili ya maonyesho bali wameitwa na Bwana kama Makuhani kwa ajili ya kusema Kitu mbele ya Mungu.
Kumbuka si kila Mtu anaweza kufanya hivi, bali ni wale tu walio itwa kwa jina la Bwana ndiyo wanao takiwa kufanaya hivi, na ndiyo maana wanapo ingia mbele za Mungu kwa ajili ya kuombea wagojwa na kutoa mapepo wachafu ama kuombea chochote kile , Mungu huwasikiliza sana na kuwajibu maombi yao. Ingiawa wapo wale wanao vaa vazi la kondoo lakini ni Mbwa mwitu yaani watumishi wa uongo, mimi sitaki kuongelea hao, bali mimi ninaongelea wewe uliye itwa kwa jina la Bwana ya kwamba unahitajika kujinyenyekesha mbele zake, na yeye amekuhaidi kukusikiliza na kuiponya Nchi yako. Ooo Bwana Yesu asifiweee....
Na ndiyo maana Marko maandiko yanatuonesha kuwa, Marko 16;17-18 "Na ishara hizi, zitafuatana na hao wa aminio, kwa jina langu watatoa pepo, watasema kwa lugha mpya, watashika nyoka, hata wakinywa kitu cha kufisha hakita wazuru kabisa, wataweka mikono yao juu ya wagojwa, nao watapata afya". Ooo Bwana Yesu asifiwe, kama wewe ni kuhani mstari huu unakuhusu ya kwamba unatakiwa kutoa pepo, kusema kwa Lungha mpya, kushika nyoka na isikidhuru, na hata utakapo kunywa vitu vya kufusha, havita kudhuru, na uweke mikono juu ya wagojwa nao wapate afya. Hii ni ahadi ya ajabu sana aliyo kuhai Mungu wewe kama Kuhani wake, nazidi kukumbusha ya kwamba si kila Mtu naweza kufanya hivi, bali ni wewe amabye umeitwa kwa jina la Yesu Kristo ndiyo unatakiwa usimame kwa ajili ya wengine.
Kumbua si kila Mtu anaye muombe Mtu mwenye mapepo aweza kuyatoa ndani yake, bali ni wale walio itwa kwa Jina la Bwana ndio ambao hata mapepo yana watii, Kwahiyo ile kwamba unaombea waogojwa wanapona na mapepo yanakukimbia nia heshima Tosha ambayo Mungu amekupia kama kuhani wake na si kila Mtu anaweza kufanya hivi bali ni wewe uliye itwa kwa jina la Bwana.
Na ndiyo maana wana wa Skewa walipo jaribu kwenda kuyatoa mapepo yaliwapiga na kuwajeruhi, kwa nini ya wajeruhui? kwa sababu walizani Heshima aliyo nayo Paulo katika ulimwengu wa Roho na wao wanayo. Kumbuka kuwa hawa walikuwa ni watoto wa Mtumishi wa Mungu tena kuhani mkuu, na pepo halikuwaogopa kwa wa sababu ya wao kuwa watoto wa kuhani mkuu bali liliwatandika kisawasawa na wakakimbia. Katika historia hii ya wana wa Sikewa tutajifunza neno lingine la kwanini pepo liliwa ambia Paulo niniamjua na Yesu nina Mfahamu na likawa uliza ninyi ni kina nani?. Tusome kwanza maandiko haya;-
Matendo 19;14-17 "... walikuwa wana saba wa mtu mmoja Skewa, Myahudi, Kuhani mkuu, walifanya hivyo. Yule pepo mchafu akawajibu, Yesu na mjua na Paulo namfahamu lakini ninyi ni kina nani?. Yule Mtu aliye pagawa na pepo mchafu akawarukia wawili, akawaweza akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile hali wa Uchi na kujeruliwa..." Kwanini pepo liliwauliza maswali hayo, kwa sababu lilitaka kujua nafasi yao walio simamia ili liwatii na liomtoke yule mtu, na ndiyo maana kama Mtu hana nguvu ya Mungu ndani yake si rahisi kwake kupambana na pepo, na asipo kaa makini pepo laweza kumjeruhi kama jinsi lilivyo wafanya wana wa Skewa. Pepo halikuuliza tu kwa kubahitisha bali lilikuwa linatambua kabisa nafasi walio kuwa wasimama watoto wa Skewa na halikuogopa kama hao ni watoto wa Mtumishi wa Mungu na kuhani mkuu bali liliwashughulikia ipasavyo. Unatakiwa utambue kuwa ile kuwa tu Mtoto wa Mchungaji au Mwinjilisti si kigezo cha kwamba pepo litakuogopa, bali litakuogopa tu kama wewe ni miongoni mwa wale watu walio itwa kwa Jina la Bwana. Ooo Bwana Yesu asifiweee....
Kumbuka heshima ya Mungu huachiliwa ndani ya makuhani wake kiasi kwamba chochote watakacho kifunga Duniani na Mungu anakifunga Mbinguni na Chochote watakacho kifungua Duniani na Mungu anakifungua Mbingu, na kama wewe ni kuhani unatakiwa ukae karibu sana na Mungu kwa maana kila Kuhani huwa na kitu cha kusema Mbele za Mungu na Mungu huwa anamsikiliza sana maana ni mtumishi wake na amemuita kwa jina lake.
Katika mwendelezo wa somo hili, tutajifunza zaidi mamala aliyoa nayo Mtumishi wa Mungu nkama kuhani, hivyo ni vyema sana kama utalifuatlia somo hili kwa ukaribu.
Mpenmdwa napenda nikushauri kitu kimoja , nacho cha husu Wokovu, katika maisha ya hapa Duniani ili uweze kuishi maisha ya amani na Furaha, unatakiwa Kuokoka yaani Kumpatia Yesu maisha yako kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako. Na utakapo Mpokea yeye si kwamba tu anakupa amani bali pia analifuta jina lako katika kitabu cha hukumu na kuliandika katika kitabu cha uzima wa milele huku akikuokoa na ziwa la moto ambalo limendali kwa ajili ya wafuasi wa shetani.
Kwahiyo unacho takiwa ni kumpatia Yesu maisha yako kama Bwana na Mwokozi wa Maisha yako, Kama hauja okoka au haujampatia Yesu maisha yako kama Bwana na Mwokozi wa Maisha yako, fuaatana nami mkatika sala hii na utaokoka;-

Sema "Eeh Bwana Yesu, ninakuja mbele yeko, mimi ni mwenye dhambi, nimekutenda dhambi kupitia matendo yangu, kusema kwangu, kuwaza kwangu na kwa dhambi za kujua na za kutokujua, Eeh Bwana Yesu ninaomba unisamehe, nisafishe kwa Damu yako ya thamani, nifute jina langu kwenye kitabu cha hukumu na uniandike jina langu kwenye kitabua cha Uzima wa milele, Eeh Bwana Yesu nakuja mbele zako kuanzia siku ya leo nifinyange moyo wangu, nafsi yangu na roho yangu kama upendavyo wewe, maisha yangu yote nakukabidhi wewe uyaongoze kwa Roho wako Mtakatifu, naomba na kuamini kupitia Jina la Yesu kristo aliye Bwana na mwokozi wa maisha yangu. Amina.
Mpendwa kama umesali sala hii fupi kwa kumaanisha tayari umeupokea wokovu, unatakiwa utafute kanisa lililo karibu yako lenye kumuabudu Mungu wa kweli na uungane nao kwa ajili ya kukua kiroho.

vile nakuomba ujitahidi kuepuka maisha ya Dhambi, maana ni dhambi pekee ndiyo itakayo kutenga na uso wa Mungu. Nakutakia maisha mema ya wokovu na Mungu akubariki,
Wako mpendwa katika Kristo,
Daniel Mbugu.
Kwa mwendelezo wa mafundisho zaidi ya neno la Mungu tembelea AMKA UKUE KIRIHO. www.amkaukuekiroho1.blogspot. Na kwa ushauri kuhusiana na maisha ya wokovu tuma ujumbe katika email yangu. www.mbugudaniel@gmail.com. Au wasiliana nami kwa kutuma ujumbe kwa njia ya sms au whatsApp kwa 0758505174/ 0655505173. Mungu akubariki.

Comments
Post a Comment