IJUE MAMLAKA ILIYOMO NDANI YA MTUMISHI WA MUNGU 2

Bwana Yesu asifiwe, Leo ni siku nyingine  ambapo tunaendelea na mwendelezo wa somo letu la 'MAMLAKA MILIYOMO NDANI YA MTUMISHI WA MUNGU" kwa kupitia makala yetu hii ya  AMKA UKUE KIROHO,. Katika sahemu ya kwanza tulijifunza mambo mbali mbali na huu ni mwendelezo wa somo letu, hivyo kama utapenda kujenga msingi wa kuanzia somo la kwanza waweza kupekua na kujifunza zaidi. Na mimi kama mwandishi wa makala hii ninakushauri uwe na Daftari la kuandika kile utakachokiona kuwa kinafaa na kitakusaidia.


LENGO LA SOMO HILI; Ni kuchochea nguvu ya maombi kwa mkristo anaye hitaji kutenda kazi na Bwana kama Kuani.

Katika sehemu ya kwanza tuliangalia ya kuwa heshima ya Mungu huachiliwa ndani ya makuhani wake kiasi kwamba chochote watakacho kifunga Duniani na Mungu anakifunga Mbinguni na Chochote watakacho kifungua Duniani na Mungu anakifungua Mbingu, na kama wewe ni kuhani unatakiwa ukae karibu sana na Mungu kwa maana kila Kuhani huwa na kitu cha kusema Mbele za Mungu, na Mungu humsikiliza sana maana ni mtumishi wake amemuita kwa jina lake.

Unapo kuwa ndani ya Yesu unakuwa na nguvu nyingi sana kiasi kwamba unauwezo wa kuambia mlima huu ng'oka nao ukakutii, si kwasababu ya ujanja wako au ujuwaji wako bali ni kwasababu wewe ni miongoni mwa wale watu walio itwa kwa jina lake, ili wasimame kwa ajili ya watu wake. 

Na ndiyo maana katika Marko neno linatuambia hivi, Marko 16;17-18 " Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio, kwa jina langu watatoa pepo, watasema kwa Lungha mpya... hata wakinywa kitu cha kufisha hakita wadhuru kabisa, wataweka mikono juu ya wagojwa nao watapata afya". Kama wewe ni kuhani wa Mungu unakuwa na nguvu ndani yako ya ya kutoa pepo, kuponya wagojwa, na unakuwa na nguvu ya Mungu kiasi  kwamba hata ukinywa vitu vya kukudhuru havita kudhuru, si kwasabau havina madhara bali kwa sabau ya nguvu za Mungu zilizomo ndani yako, ambazo zinakufanya uishi maisha ya tofauti na watu wengine, ambao hata wakijaribu kukudhuru hawata weza.  Ooo Bwana Yesu asifiwe sanaa.. Yesu ni mzuri sana na anakupatia ulinzi ulio imara wewe kama kuhani wake.


        MAMLAKA ILIYOMO NDANI YA MWAMINI KAMA  KUHANI
Kuhani kama mtumishi wa Mungu anayo mamlaka aliyopewa na Mungu ya kutenda mambo mbalimbali ya ki Mungu, Na kutokana na Marko 16;17-18,  inatuonyesha wazi ya kwamba huduma alizopewa Kuhani ni pamoja na kutoa pepo, kuponya wagojwa, kusema kwa lugha mpya( ingawa hii yaweza kuwa karama ya kipekee), na kunywa vitu vya kufisha na visimdhuru.

Na kuhani amepewa Amri ya kutenda hizo huduma kama mtumishi wa Mungu, nakama ni amri inamaanisha ni kitu cha kumshinikiza ya kuwa ni lazima azitende. Ukisoma Luka , neno la Mungu linatueleza kuwa;- Luka 10;19 "Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakacho kuzuru". Neno amri katika andiko hili lina tuonesha ya kwamba ni lazima kwa mtumishi wa Mungu kukanyaga Nyoka na Nge, nyoka na nge ni nguvu zote za Shetani. Kama ni Amesema ni Amri anamaanisha ya kwamba ni lazima mtumshi wa Mungu atekeleze, Kwa mfano. Rais wa Nchi yoyote, anapo toa amri ya kitu chochote katika nchi yake ni lazima kile alicho kisema kitekelezwe haraka, na hii ni kwasabau ya amri na sio ombi. Hivyo kama Mungu katika mstari huu anapo sema Nimewapa amri anakuwa akiwataka watumishi wake watii kile walicho wambia cha kukanya na kuvunja nguvu zote za adui.  Ooo haleluyah...

Katika mstari huu tunakutane na neno nguvu zote zote za yule adui, neno hili linatuonesha ya kwamba ipo idadi flani ya nguvu za adui, kwa hiyo ndiyo maana ametumia nguvu zote maana yake sio chache wala nusu. Neno nguvu zote za yule adui linampatia Mkristo au kuhani aliye okoka kuvunja na kuharibu nguvu za shetani kwa kiwango chochote kile atakacho kitumia kupapambana na watu wa Mungu Duniani, na unapo endelea kusoma unakuta neno lina mtia moyo kuhani ya kwamba wala hakuna kitu kitakacho kudhuru. kwa hiyo wewe kama kuhani umepewa ulazima wa kukanyaga na kuvunja nguvu zote za shetani katika kila nyanja wala hakuna kitu chochote kitakacho kudhuru. Hakuna kitu chochote kitacho kudhuru kwa sababu wewe ni kuhani na unanguvu za Mungu ndani yako, hivyo unalindwa na Mungu mwenyewe ambaye ndiye chanzo cha nguvu zote Duniani na Mbinguni pia, kwa lolote utakalo litenda wewe lenye kumuwakilisha Mungu, tambua kabisa ya kwamba ni Mungu ndiye katenda ndani yako. Ooo h Bwana Yesu asifiweeee...

Hivyo ni wajibu wako kabisa wewe kama mtumishi wa Mungu, kukanyaga nyoka na Nge na nguvu zote za Yule adui Yetu shetani na wahakuna kitu chochote kutoka kwake kitakacho kudhuru.

Katika mamlaka ya mwamini, Mwamini katika Mathayo, ameambiwa kuwa;- Mathayo 10;8 " Pozeni wagojwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo...". Kwa hiyo wewe ukiwa kama mtumishi wa Mungu licha ya kwamba tu umepewa  malaka ya kukanyaga nge na nyoka, na kutoa pepo kuku ukipoza wagojwa, kipo kitu kingingine cha ziada kabisa ambacho ni kufufua wafu, Watumishi wengi wanapo fikia hatuaa hii ya kufufua wafu hua wanaogopa na kuona kama si kazi yao, kumbuka ya kwamba wewe ni mtumishi wa Mungu na kama ni mtumishi wa Mugu ni lazima uliamini neno lake linalo sema ya kwamba hata kufufua wafu napo ni wajibu wako, na si kuponya tu wagojwa na kutoa pepo kama ulivyo zoea, kumbuka Yesu ni yeye yule jana , leo na hata milele. Kama aliweza kumfufua Razaro na akafufuka huku akikupatia wewe mamlaka, tambua kabisa ya kwamba na wewe  uwezo huo unao wa kufufua wafu walio kufa kiroho na kimwili. Hilo ndilo jukumu lako wewe kama kuhani wa Mungu sikila mtu amepewa kitu hiki  bali wewe tu uliye mwamini Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yako. Bwana Yesu asufiweee.. 

Si kutoa npepo tu kama ilivyo zoeleka bali kipo kitu kingine cha ziada toka kwa Mungu, kumbuka Yesu mwenye alisema katika kitabu kile cha Yohana 14;12,  ya kwamba "Amini, amini, nawaambieni, yeye aniaminiaye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya, naam, na kubwa kuliko hizo atazifanya kwa kuwa mimi naenda kwa Baba".  Kwa hiyo kama Yesu mwenyewe ndiye aliye sema ya kwamba kazi alizo zifanya na wewe utazifanay tena na kubwa kuliko zoke, inamaanisha ya kwamba kwa sasa kipo kiwango kikubwa sana cha nguvu ya Mungu ndani yako , Kumbuka neno linatuambia ya kwamba sisi tu watenda kazi pamoja na Kristo, nakama tu watenda kazi pamoja na Kristo je ni neno gani Gumu lolote la Kumshinda Bwana?. Uwe na uhakika hakuna, hivyo ni wajibu wako kuponya wagojwa, kutoa pepo na kufufua wafu. Ooo Bwana Yesu asifiweeee....

Katika Mamlaka ya mwamini kama kuhani haupaswi kuwa na mashaka katika kumtumikia Mungu, Kwasababu katika kitabu cha Yakobo, tumeambiwa kuwa ;- Yakobo 1;6-7 "...mwenye shaka ni kama wimbi la bahari, linalo chukuliwa na upepo huku na huku, maana Mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana".  Mpendwa nakushauri kabisa acha mashaka unapo kuwa ndani ya Mungu, kwakuwa Mungu hapendi watu wanao mtumikia huku wakiwa na mashaka ndani yao, na amesema katika Yakobo hii 1 ya kwamba mwenye mashaka ni kama wimbi linalo chukuliwa na upepo, na mtumisi kama huyo asidhani ya kuwa atapokea kitu kutoka kwa Mungu.  Kwa nini asipokee kitu kwa sababu hakumwamini Bwana, hivyo aweza kujibiwa akazani ya kuwa ni juhudi zake mwenewe, na ndiyo maana Mungu ansema mtu asiye na imani asizani ya kuwa atapokea kitu kwake.

Kwa maana hiyo yamkini yapo maombi mengi uliyo peleka kwa Mungu na haujajibibiwa kwa sabubu ya kuto kuamini kwako. kumbuka wewe ni kuhani wa Mungu na kama ni kuhani wa Mungu ni lazima uwe kielelezo cha kumwamini kwanza kabla ya wengine.

Na ndiyo maana ukiwa mtumishi wa Mungu kama kuhani unatakiwa kuwa hodari sana kama ilivyo andikwa katika Waefeso 6;10-11 ya kwamba Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake huku ukivaa siraha zote za Mungu katika kumpinga shetani.
 Ni nguvu za Mungu tu ndizo zenye kukutenga na mishale ya mwovu shetani.
Ni nguvu za Mungu tu ndizo zitakazo kuwezesha wewe kumshinda shetani na kutembea katika mapenzi ya Mungu.
Ni nguvu za Mungu tu ndizo zinazo kupatianwewe heshima ya kusimama madhabahuni pa Bwana huku watu wakikusikilza ili wapatu kitu cha ki Mungu.

Kumbuka kuhani huwa na kitu cha pekee anacho weza kukiachilia  kwa Bwana kwa ajili ya watu flani anao waombea na Mungu akamsikia na kumjibu, na yeye ndiye anaye weza kusogea mbele za Mungu hata katika toba ya Nchi sawasawa na 2Nyakati 7;14.

Na ndiyo maana Biblia inatueleza  katika Waebrania 6;10 ya kwamba Yesu amefanyika kuwa kuhani mkuu mfano wa Melkisedeki, kwa hiyo kama Yesu ni kuhani mkuu inamaanisha kuwa na yeye nanatuombea sisi na kutusogeza mbele za Mungu. Kumbuka katika sehemu ya kwanza tulijifunza jinsi ambavyo katika agano la kale kuhani alivyo kuwa anawasogeza watu mbele za Mungu na mtu mwingine hakuruhusiwa. Kwa maana hiyo basi sisi tunao mwamini Mungu ni lazima tupite katika Kuhani wetu mkuu ambaye ni Yesu Kristo ili atupeleke kwa Mungu.

Unapo soma maandiko katika kitabu kile cha  Yohana 14;6, Yesu anatueleza wazi kabisa ya kwamba yeye ndiye njia ya kweli na uzima, na mtu hawezi kwenda kwa Baba pasipo kupitia njia yake, na njia  njia yake ni moja tu ni kuoakoka, yaani Kumkubali yeye kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako. Kwahiyo kama umesoma makala hii na haujakoka tambua kabisa ni mapenzi ya Mungu wewe usome ujumbe wake huu. na Mimi kama mtumishi wa Mungu ninayo sana shauku ya kukuona umeokaka na kumpatia Yesu maisha yako kuwa Bwana na Mwokozi wako ili siku utakapo taoka hapa Duniani uka urithi uzima wa milele.

Kwa hiyo kama haujaokoka fuatana na mi katika ombi hili linalo fuata, omba kwa imani na kwa kumaanisha;-
Sema "Eeh Bwana Yesu, ninakuja mbele yeko, mimi ni mwenye dhambi, nimekutenda dhambi kupitia matendo yangu,  kusema kwangu, kuwaza kwangu na kwa dhambi za kujua na za kutokujua, Eeh Bwana Yesu ninaomba unisamehe, nisafishe kwa Damu yako ya thamani, nifute jina langu kwenye kitabu cha hukumu na uniandike jina langu kwenye kitabua cha Uzima wa milele, Eeh Bwana Yesu nakuja mbele zako kuanzia siku ya leo nifinyange moyo wangu, nafsi yangu na roho yangu kama upendavyo wewe, maisha yangu yote nakukabidhi wewe uyaongoze kwa Roho wako Mtakatifu, naomba na kuamini kupitia Jina la Yesu kristo aliye Bwana na mwokozi wa maisha yangu. Amina. 


Mpendwa kama umesali sala hii fupi kwa kumaanisha tayari umeupokea wokovu, unatakiwa utafute kanisa lililo karibu yako lenye kumuabudu Mungu wa kweli na uungane nao kwa ajili ya kukua kiroho. 

Kama umeguswa chochote kupitia makala hii , naomba uandika ujumbe wako hapo chini na nitakapo soma nitafurahia sana.

Na kama utahitaji maombi na ushauri wowote wa kiroho, wasiliana nami kupitia namba na emeil yangu kwa njia ya sms. mwishoni nitatoa namba na email,  lakini kama umeokoka kupitia makala hii waweza kunitumia ujumbe kwa njia ya simu , kwa watsapp, au kwa kawaida , au kupitia email yangu nitakayo itoa hapo chini.



            Wako mpendwa katika Kristo, 
                           Daniel Mbugu.

Kwa mwendelezo wa mafundisho zaidi ya neno la Mungu tembelea  AMKA UKUE KIRIHO. www.amkaukuekiroho1.blogspot. Na kwa ushauri kuhusiana na maisha ya wokovu tuma ujumbe katika email yangu. www.mbugudaniel@gmail.com. Au wasiliana nami kwa kutuma ujumbe kwa njia ya sms au whatsApp kwa 0758505174/ 0655505173. Mungu akubariki.

Comments

Popular Posts