ASILI YA MWANADAMU KIBIBLIA (Biblical Anthropology) 2
Bwana yesu asifiwe, nakusalimu katika jina
la Yesu aliye Bwana na mwokozi wa maisha yetu.
Karibu katika makala yetu hii ya AMKA UKUE KIROHO ambapo
leo Tutaendelea na somo Linaloitwa "ASILI YA MWANADUMU KIBLIA",
katika sehemu ya kwanza tulijifunza mambo mengi sana, na si rahisi kuyarudia,
hivyo kama haukujifunza nakuomba ulipitie na kulisoma kwa ajili ya Utukufu wa
Bwana.
Kipidi kilichopita tuliendelea kuangalia namna tulivyoumbwa kwa namna ya ajabu
na ya kutisha sana na Mungu wetu,
lakini pia tukafanikiwa kuanza kuangalia kuhusu kusudi la mwanadamu kuumbwa, nikakuambia tutaangalia kusudi la Mungu kwa upana wake na nikasema kuna kusudi la Mungu kwa mwanadamu ambayo mimi niliamua kiita ngazi ya kwanza na kusudi tena la mwanadamu ambayo niliita ngazi ya pili.
Kabla sijaanza kuongelea mambo ya kkusudi kwa siku ya leo nataka turudi tena nyuma tuangalie uumbaji wako ulivyofanyika kwa namna nzuri nay a kipekee. Bado niko hapo kuna mambo unayoyahitaji kujua mabayo ni msingi mzuri sana wa masomo haya mengine yote yaliyobaki.
Hebu angalia hapa;
Zaburi 139:13-16 “Maana
Wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu, Uliniunga tumboni mwa mama yangu.
Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa Kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni
ya ajabu, Na nafsi yangu yajua sana, Mifupa yangu haikusitirika kwako,
Nilipoumbwa kwa siri, Nilipoungwa kwa ustadi pande za chini za nchi; Macho yako
yaliniona kabla sijakamilika; Chuoni mwako ziliandikwa zote pia, Siku
zilizoamriwa kabla hazijawa bado”
Kumbe umeumbwa kwa namna ya ajabu sana, kama ambavyo tumeona kwenye vipindi vilivyopita wewe ni kiumbe wa ajabu zaidi na wa kutisha kuliko kiumbe yeyote aliyewahi kuumbwa na Mungu tangu Mungu ameanza mradi wake wa uumbaji.
Huko mbeleni tutawaangalia malaika walivyoumbwa, utagundua wanatisha lakini bado ule utiisho wao ukilinganisha na wa kwako bado ni mbali mbali.
Kwa sasa nataka tuendelee kuzama ndani uone namna ulivyoumbwa ili isitokee hata siku moja ukajishusha thamani yako wala kuruhusu kitu chochote kiishushe thamani maisha yako.
Mstari niliyokuonesha hapo juu unatueleza siri ya ajabu sana ya namna tulivyoumbwa; naamini baado unaakumbuka somo lililopita kwamba tuliona umeumbwa ukiwa na UTU WA NJE na UTU WA NDANI ambao ndiyo wewe mwenyewe.
Sasa katika hii mistaari amefafanua vizuri haya maeneo makuu mawili ya mwanadamu;
katika mstaari wa 13 hadi wa 15 hapo utaona akiongelea sana kuhusu utu wa nje ulivyoumbwa tena kwa ustadi kabisa; unapouangalia ule mstari wa 15 unaona kitu cha ajabu pale anaposema niliungwa kwenye pande za chini za nchi akiwa anamaanisha namna mwili wako ulivyoumbwa na viungo vilivyo ndani yake ndani ya tumbo la mama yako.
Lakini mstari ule wa 16 unaelezea namna ulivyoumbwa UTU WA NDANI ambayo ndiyo roho yako; angalia anavyosema;
Zaburi 139:16 “Macho yako yaliniona kabla sijakamilika; Chuoni mwako ziliandikwa zote pia, Siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado”
Hapa alikuwa anaongelea kwa habari ya roho yako; anaposema macho yake yalikuona kabla hujakamilika maana yake kabla hujapewa mwili ulikuwa mahali Fulani ukiwa unasubiri siku zilizoamriwa ndipo upewe mwili uzaliwe hapa duniani.
Lakini ukweli ni kwamba siku ulizozaliwa haimaanishi kwamba ndipo ulipoumbwa, ulikuwa umeumbwa siku nyingi sana lakini ulikuwa ukisubiria tu wakati ambao Mungu aliauona kuwa unafaa kuzaliwa duniani ndipo akarusu uanze kuungwa mtima wako kwenye moyo wa mama yako pamoja na viungo vingine.
Kumbe mama yako alifanya kazi nzuri kushirikiana na Mungu kukuunda mwili wako mama yeye akitumika kama kukuhifadhi huku Mungu akihusika kwa miezi tisa kukuunga kikamilifu ili uzaliwe ukiwa na mwili kabisa.
Sasa baada ya maelezo hayo soma tena haya maneno uone utakaavyoyaelewa;
Zaburi 139:13-16 “Maana Wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu, Uliniunga tumboni mwa mama yangu. Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa Kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, Na nafsi yangu yajua sana, Mifupa yangu haikusitirika kwako, Nilipoumbwa kwa siri, Nilipoungwa kwa ustadi pande za chini za nchi; Macho yako yaliniona kabla sijakamilika; Chuoni mwako ziliandikwa zote pia, Siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado”
Katika sehemu ya kwanza tulifanikiwa kuangalia kidogo kuhusu kusudi la Mungu kwa maisha yetu.
Tuliangalia kusudi ambalo ni kwa kila mwanadamu ambalo nilikuambia mimi huwa naita kusudi ngazi ya kwanza, na pili ni pale unapogundua kusudi binafsi la maisha yako ambalo mimi huwa naita kusudi ngazi ya pili.
Yote unayapata kwa usahihi pale unapoamua kumpa Yesu maisha ili akurejeshe kwenye nafasi yako ya awali tuliyoipoteza bustanini ya Edeni kama ambavyo tumekuwa tukiona. Hebu tuangalie kusudi ngazi ya pili leo;
KUSUDI LA MWANADAMU AMBAYO MIMI NALIITAGA NGAZI YA PILI
Ni pale unapoanza kugundua upekee uliyonao ambao unatokana na wito unaoanza kuugundua kwamba ulisababisha ukazaliwa.
Kila mtu duniani amekuja kwa WITO maalumu kabisa na huo wito unapoujua ndipo tunasema umejua kusudi la Mungu kwa maisha yako binafsi (ambayo naiita kusudi ngazi ya pili)
Yeremia 1:5 “Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa”
Kuna mambo mengi sana yanayoambatana na kusudi la wewe kuzaliwa.
Kadri unavyozidi kulielewa kusudi lako ndivyo maisha yako yanavyoongezeaka thamani.
Unatakiwa ujue kwamba kuna WITO mkuu wa maisha yako ambao ndiyo tunaita KUSUDI la maisha yako, halafu Mungu akakupa KIPAJI/KARAMA/UWEZO Fulani kama kitendea kazi cha huo wito wako.
Najua Mungu atatupa nafasi kule mbeleni kwenye somo la Roho Mtakatifu kujifunza zaidi kuhusu karama mbalimbali pamoja na huduma za Roho mtakatifu. Lakini tunapoongelea kipaji ni ule uwezo uliyozaliwa nao.
Tofauti ya KARAMA na KIPAJI ni kwamba huwezi kuwa na karama za Roho mtakatifu kabla hujaokoka lakini kipaji anakuwa nao mtu yeyote hata kama hajaokoka. Lakini kwakweli vyote hivyo ni vitendea kazi ulivyokabidhiwa kulingana na WITO aliyokuitia Mungu hapa duniani.
KILA MTU ANA UMUHIMU
DUNIANI LAKINI NI WACHACHE WENYE UTHAMANI DUNIANI.
Kwa nini? Kwa sababu watu wengi wanaishi kwa sababu wamepewa pumzi tu na hawajiulizi kwanini wengine wanakufa kila siku halafu wao bado wamebaki hai.
Nimeiona mara nyingi sana hii, Watu wanakuwa wamaongea sana kila wakati kwamba, “mimi na wewe tumebaki, si kwamba ni wema ila ni neema za Mungu tu, inatupasa kumshukuru yeye”
Sasa angalia, unamshukuru Mungu tu kwa sababu amekuacha ili uendelee kuishi bila faida yeyote duniani? Suala la kushukuru hata ukifa inakupasa ushukuru tu maana ndivyo biblia inasema tushukuru kwa kila jambo. Lakini wengi hawajiulizi kwa sura hii,
“Mimi nimebaki bado ulimwenguni, ee Mungu nisaidie kujua kwa nini bado mimi umeniacha wakati wenzangu kabisa nao walikuwa kama mimi ila wao wamekufa” Hilo ndo angalau swali lenye mantiki kwa Mungu.
USHUHUDA MFUPI WA MAISHA YANGU .
Nakumbuka siku moja
nikiwa naendesha pikipiki kwenye lami (highway) nilipata ajali mbaya sana
ambayo kama si Mungu sijui kingetokea nini hapo.
Dakika kama saba au tano
kabla ya ajali kutokea nikiwa kwenye mwendo nilianza kujisikia kama nguvu za
Mungu zimenifunika halafu nikaanza kunena kwa lugha, baadaye kidogo tu ajali
hiyo ikatokea mbaya sana siwezi hata kuielezea sana.
Kilichonishangaza ni baada ya kuokotwa na watu waliopita wakiwa kwenye gari yao, nikiwa niko njiani kwenye gari nilisikia sauti iliyonihamasisha kufanya kazi ya Mungu kama kichaa, kwa sababu nilimsikia Mungu ndani yangu akisema,
“nimekizuia kifo kwa ajili ya kitu ulichokibeba na kwa sababu bado hujamaliza kazi yako, bado unayo sababu ya kuendelea kuishi duniani na lile kusudi ulilobeba ndilo linalokulinda”
Nakumbuka nilitokwa na machozi nikamshukuru Mungu, nikaanza kujiona kwa namna ya tofauti zaidi ya hapo mwanzo huku nikimuuliza tena kwa undani kusudi langu kuwepo duniani ili nilitimize kwa ukamilifuumbuka nilitokwa na machozi nikamshukuru Mungu, nikaanza kujiona kwa namna ya tofauti zaidi ya hapo mwanzo huku nikimuuliza tena kwa undani kusudi langu kuwepo duniani ili nilitimize kwa ukamilifu wake.
Tangu kipindi hicho Mungu alinisaidia zaidi nikaendelea hadi leo ninajua neno moja tu kwamba kuishi kwangu ni kwa sababu kusudi na wajibu wangu bado haujaisha na najua siyo kifo, wala shetani wala yaliyopo, wala yatakayokuja, ambayo yataweza kunitoa kwenye kusudi la maisha yangu.
NATAKA NIKUHAKIKISHIE.
Mungu amekupa bado muda
wa kuishi maana anajua anakuhitaji kwa kiasi gani, labda alikuwa anasubiri
upate hili somo kama utaanza kubadilika na kujigundua na kua nza kuufanyia
wajibu wako kazi kabla ya muda wako kuisha.
Ndiyo maana mtu aliyelijua kabisa kusudi na ameanza kulifanyia kazi, tayari Mungu anamlinda sana mpaka haakikishe amelikamilisha hilo kusudi.
MAISHA YENYE THAMANI.
Maisha yenye thamani
yanalenga kuishi kwa kusudi la Mungu kweye maisha yako ambayo yanaanza na
kuokoka kwanza. Namna pekee ya kuweza kurudishwa kwenye kusudi la Mungu
inaanzia na wewe kuamua kuokoka maana Yesu ndiye alitumwa kukurudishia nafasi
yako.
- Maisha yenye thamani ni kufanya wajibu wako kama ilivyo
kusudi lako
- Maisha yenye thamani ni kuishi kwa kuwa baraka kwa
jamii yako, na dunia kwa ujumla.
- Maisha yenye thamani ni kuishi kwa utakatifu kama Mungu
atakavyo.
- Maisha yenye thamani ni kutokufanya mambo kwa ajili ya
faida yako tu, umeumbwa kwa ajili ya wengine.
- Maisha yenye thamani ni kujitunza na kujiepusha na kila
aina ya uharibifu wa mwili, nafsi na roho yako.
- Maisha yenye thamani ni kuishi maisha yako, na si
kuishi kwa kuiga wengine. Unapoiga maisha ya watu maisha yako unayapoteza
kabisa “imitation is limitation” --John Mason
kila mtu anatakiwa ajue
kwamba maisha yake yanahitajika sana hapa duniani kwa ajili ya ufalme wa Mungu
pamoja na wanadamu wenzake.
Tunapojifunza hili somo maana yake tunarejea kwenye wazo la awali la Mungu kuhusu maisha yetu kabla ya dhambi kuingia kwenye historia ya mwanadamu.
Biblia nzima inahusu vitu vinne usije ukasahau hata siku moja;
1.
Uumbaji wa Mungu
2.
Anguko la Mwanadamu
3.
Ukombozi wa
Mwanadamu
4.
Urejesho
Haya mambo yote ukisoma
kuanzia kitabu cha mwanza hadi ufunuo vitabu vyote 66, vinaongelea vitu hivi tu
vinne.
Sasa hili somo letu ni la muhimu sana kwa sababu linaanza kukurejesha kwenye asili na msingi kabisa wa kusudi la Mungu kumuumba mwanadamu ndiyo tunaita wazo la awali la Mungu (God’s original idea)
Katika yale maswali matano niliyokunesha siku ya kwanza kabisa, naamini kama umekuwa ukinifuatilia vizuri umeanza kupata majbu yay ale maswali kwa ufasaha kabisa.
NB; Kumbuka hakuna sehemu nyingine ya kupata majibu sahihi ya maisha yako zaidi ya kutoka kwa muumba wako pekee ambaye ni Mungu wetu wa pekee na wa kweli. Na namna rahisi ya kujua wazo la awali la Mungu kwa maisha yako ni kwenye neno lake pekee yaani biblia.
Sasa leo nataka tuangalie kidogo kuhusu hatma ya maisha ya mwanadamu, kwamba baada ya maisha haya kweli kuna maisha mengine au laa!
Kama umenifuatilia vizuri utakuwa umeona kwamba kumbe sisi wanadamu siyo tu miili hii inayoonekana kwa nje kumbe kuna utu wa ndani ambao ndiyo mtu halisi.
Na tuliona pia kwamba
wakati Mungu anaumba wanyama wa kwenye maji aliongea na maji akiyaambia yatoe
wanyama wa aina yake, pia akaongea na ardhi akaiambia itoe wanyama pamoja na
mimea ikawa hivyo.
Lakini alipofika kwenye kumuumba mwanadamu hakuongea na kitu chochote zaidi ya yeye mwenyewe kujisemesha (nafsi zote tatu), yaani walikuwa wanajadiliana Mungu Baba, Mungu mwana na Mungu Roho mtakatifu (Somo liko mbele yetu utaelewa vizuri kuhusu huu utatu mtakatifu). Namaanisha Mungu katika nafsi zake tatu walipofika kumuumba mtu wakasema watamfanya kwa sura na mfano wao na siyo kwa kitu kingine.
Nilikufafanulia pia maana ya SURA YA MUNGU na MFANO WA MUNGU na mojawapo ya maana yake ilikuwa kwamba kumbe Mungu alitupa pumzi yake ambayo ni sehemu ya roho yake akamfanya mwanadamu.
MWANZO 1:7 “Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai”
Kwa sababu hiyo wewe ni roho na kwa sababu ni roho hautakufa, ujapokufa mwili wako bado roho yako lazima irudi kule ilikotoka.
Kama vile mmea
unavyonyauka na kurudi kuoza ambako ndiko asili yake, au mnyama anaapokufa
anarudi kwenye asili yake; vivyo hivyo na wewe unapokuwa umetwaliwa kwenye
maisha haya ya mwili lazima mwili wako urudi kwenye mavumbi ulikotoka na roho
yako irudi kwa Mungu ilikotoka.
Mauti ni nini?
Mauti kwa tafsiri
rahisi sana ya neno mauti ni KUTENGWA.
Sasa Kuna aina mbili za mauti;
- Mauti ya Kwanza – hapa maana yake ni kutengwa na
wanadamu wenzako waliyo hai.
- Mauti ya pili – ni kutengwa na Mungu milele na milele
Mauti ya kwanza
unashughulikia mwili wako tu lakini mauti ya pili unashughulikia roho yako. Na
mauti ya kwanza siyo shida kwa sababu kila mwanadamu aliyezaliwa hapa duniani
maana yake amepewa mwili na namna pekee ya kurudi kwenye asili yetu ni kwa
kutoka kwenye huu mwili kwa njia ya mauti ya kwanza.
AYUBU 14:1-2 “Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke Siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu. Yeye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa; Hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe”
Lakini mauti ya pili ni ya wale tu ambao watatengwa na Mungu milele na milele kwa sababu ya kutokumwamini Yesu na kumkubali kama mwokozi wa maisha yao.
Ndiyo maana Mungu alihakikisha kwa gharama yeyote anailipa ili ahakikishe wokovu umepatikana kwa yeyote atakayeuhitaji, ili baadaye ambao hawatamkubali Yesu wahukumiwe hii adhabu mbaya sana ya Kutengwa na Mungu milele na milele.
Hebu angalia;
Yohana 3:16-18 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu,
hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima
wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali
ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini
amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu”
Sasa mauti ya pili ni mbaya kwa sababu unaatengwa kutoka kwenye chanzo chako ambacho ni Mungu tena milele na milele vibaya zaidi ni kwenye ziwa la moto ambalo wanadamu wataunguzwa huko milele na milele.
Ufunuo 21:8 “Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili”
Haya tutayaongea vizuri tukifika kwenye somo la siku za mwisho, lakini kwa sasa nataka nikuonyeshe kwamba hatma ya maisha yako imekaaje.
Mwanadamu kwa sababu ni
roho kama tulivyokwisha kuona, tafsiri yake ni kwamba mwanadamu hawezi kufa
roho yake kabisa, ajapokufa mwili lakini kwakweli yeye halisia ambaye ni roho
hawezi kufa kamwe.
Kuna mambo mawili mbele ya kila mwanadamu ama uzima wa milele au Jehanam ya milele (ziwa la moto) unaposikia ziwa la moto ni moto kweli lakini ni moto usiyo wa kawaidi kwa sababu siyo wa kuunguza mwili bali wa kuunguza na kuiadhibu roho ya mtu.
Kama kanisa lingejua
kwamba maisha yao ya hapa duniani ni sehemu ndogo sana ya maisha yao
(ukilinganisha na vile walivyoumbwa) lakini yana thamani kubwa na madhara
makubwa kwa yale yajayo; wangefanya kila linalowezekana kuongeza thamani maisha
yao sasa. Kumbuka kanisa ninamaanisha mtu aliyeokoka tayari.
Maisha haya ni machache sana ya hapa duniani kama ukiweza kulinganisha naya umilele yajayo lakini pamoja na uchache wa haya maisha ndiyo yataamua hatma yako ni wapi kwa habari ya umilele ujao.
Mtu mmoja alisema hivi;
“Ukilinganisha na
umilele, muda wetu wa kuishi hapa duniani ni sawa na mtu kufunga na kufungua
macho” (Rick Warren).
Angalia maandiko yanavyozidi kutusaidia hapa;
2Wakoritho 4:18 “tusiviangalie vinavyoonekana (vya
kimwili), bali visivyoonekana (vya kiroho). Kwa maana vinavyoonekana ni vya
muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele”
Ukifika kwenye viwango hivi vya kujua kuweka vipaumbele vya maisha yako kwa kuzingatia vitu vya milele na vitu vya muda utakuwa umefikia kwenye kiwango kikubwa sana cha kumjua Mungu.
Kwa hiyo kumbe hili somo
pia linakusaidia kukufungua macho ujue namna ya kuweka vipaumbele vya msingi
kwenye maisha yako kwa namna ilivyokupasa.
Yesu aliongea jambo la msingi sana hapa usije ukasahau hata siku moja;
MARKO 8:36-37 “Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata
ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake? Ama mtu atoe nini badala ya nafsi
yake?”
Kwa maneno mengine ukishaelewa vizuri namna ulivyoumbwa itakusaidia kuwekeza sana kwenye utu wako wa ndani kuhakikisha unaujenga vizuri na kuuimarisha sana kwa sababu ndiyo utakaodumu milele.
Hebu angalia huu mstari;
“……………….tena
ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao; ila kwa jinsi mwanadamu asivyoweza
kuivumbia kazi ya Mungu anayoifanya tangu mwanzo hata mwisho” Mhubiri
3:11.
Somo hili litakuwa na mwendelezo katika
sehemu ya Tatu , hivyo endelea kufatilia zaidi ili unufaike na mafundisho
ya neno la uzima.
Furaha nzuri sana maishani ni kuishi maisha matakatifu yenye kumpendeza Mungu, na njia rahisi ya kuweza kuishi maisha matakatifu ni kumpatia Yesu maisha yako, yaani kuokoka. Unapo okoka Yesu anakuwa anayatazama maisha yako kwa ushindi ulio mkuu, huku akikutakasa kwa ajili ya uzima wa milele.
Kama bado hauja okoka sali sala hii fupi kwa imani, na utakuwa umekoka na kumpokea Roho Mtakatifu huku ukitembea kwa kuishi maisha matakatifu;-
Sema "Eeh Bwana Yesu, ninakuja mbele
yeko, mimi ni mwenye dhambi, nimekutenda dhambi kupitia matendo yangu,
kusema kwangu, kuwaza kwangu na kwa dhambi za kujua na za kutokujua, Eeh
Bwana Yesu ninaomba unisamehe, nisafishe kwa Damu yako ya thamani, nifute jina
langu kwenye kitabu cha hukumu na uniandike jina langu kwenye kitabua cha Uzima
wa milele, Eeh Bwana Yesu nakuja mbele zako kuanzia siku ya leo nifinyange moyo
wangu, nafsi yangu na roho yangu kama upendavyo wewe, maisha yangu yote nakukabidhi
wewe uyaongoze kwa Roho wako Mtakatifu, naomba na kuamini kupitia Jina la Yesu
kristo aliye Bwana na mwokozi wa maisha yangu. Amina.
Mpendwa kama umesali sala hii fupi kwa
kumaanisha tayari umeupokea wokovu, unatakiwa utafute kanisa lililo karibu yako
lenye kumuabudu Mungu wa kweli na uungane nao kwa ajili ya kukua kiroho.
Kama umeguswa chochote kupitia makala hii
, naomba uandika ujumbe wako hapo chini na nitakapo soma nitafurahia sana.
Na kama utahitaji maombi na ushauri wowote wa kiroho, wasiliana nami kupitia namba na emeil yangu kwa njia ya sms. mwishoni nitatoa namba na email, lakini kama umeokoka kupitia makala hii waweza kunitumia ujumbe kwa njia ya simu , kwa watsapp, au kwa kawaida , au kupitia email yangu nitakayo itoa hapo chini.
Somo hili limeandaliwa na Noel Pallangyo, na kuandikwa na mwandishi Daniel J Mbugu wa
makala ya AMKA UKUE
KIRIHO.
Karibu katika sehemu ya Tatu ambayo
itawekwa kupitia blogu hii. Mungu akubariki sana.
Wako mpendwa katika Kristo,
Daniel Mbugu.
Kwa mwendelezo wa mafundisho zaidi ya neno
la Mungu tembelea AMKA
UKUE KIRIHO. www.amkaukuekiroho1.blogspot. Na kwa ushauri
kuhusiana na maisha ya wokovu tuma ujumbe katika email yangu. www.mbugudaniel@gmail.com. Au
wasiliana nami kwa kutuma ujumbe kwa njia ya sms au whatsApp kwa 0758505174/
0655505173. Somo hili litaendelea katika sehemu ya 3.
Comments
Post a Comment